crunkstaa
JF-Expert Member
- Aug 4, 2012
- 331
- 159
there is no such a Thing as Uchawi
Mkuu una roho ngumu,yaani bado huamini kwamba uchawi upoo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
there is no such a Thing as Uchawi
Root hii si kweli uchawi upo tena live kabisa hata vitabu na misahafu vimeelezea uwepo wa uchawi ningejua uko wapi na una nafasi ningekualika uje huku niliko ujionee....niko field ya utambuzi wa kiroho na nguvu za kishirikina karibu sana
Dogo nilimkuta butimba mwanza,nienda kumuona rafikiyangu ila ameisha yoka kuwa hana hatia
Mkuu una roho ngumu,yaani bado huamini kwamba uchawi upoo?
sasa kwa nini wasizifiche kimazingara ili askari wasizione? au uchawi huwa unafanyika usiku tu?wanshindwa kwasababu ndumba zao huwa wameziacha nje si unajua jera huingii na kitu chochote ndo maana wanavuliwaga nguo zote na kusachiwa hadi matakoni sow hawawezi toroka lakini kama wangengia nazo wangesepa tu maana hamna namna
Mbona naskia hata wao pia ni wanga tena sana tume ningesikia mzungu karogwa hapo ningeamini uchawi upo..usichokiamini hakiwezi kuwepo!
me ningesikia mzungu karogwa hapo ningeamini uchawi upo..usichokiamini hakiwezi kuwepo!
Mbona naskia hata wao pia ni wanga tena sana tu
wanapo kuwa gerezani kumbuka wanakuwa hawana tunguli,hirizi wala ungo..kabla ya kuingia lazima usachiwe.kwa ufupi wanakuwaga hawana vitendea kazi
Nimekutana na wawili walioweza kutoka gerezani kwa nguvu za kichawi.
Mmoja alifungwa kama leo, kesho yake asubuhi askari wakakuta kinyesi mbele ya mlango huku kufuri zito bado lipo mlangoni, walipofungua wakauliza, ni nani kanya mbele ya mlango na huku ulikuwa umefungwa, jamaa akajibu ni yeye. Akaulizwa alitokaje mpaka akaenda kunya kwa nje akajibu "niliamka usiku nikajikuta tu nimetoka nje ya gereza na kujisaidia kisha nikarudi ndani tena"
Siku hiyo hiyo akaachiwa huru asitoroshe wafungwa wengine. Alipoachiwa alienda kituo cha polisi na gunia la nyoka kulipiza kisasi kwa waliomkamata...ilikuwa patashika
Osale Otango alikuwa ni mwizi maarufu enzi za wakoloni huko Tanga yeye alikuwa anaibia wazungu halafu anaenda kuwagaiya waafrika maskini, na ilikuwa akitaka kwenda kuwaibia alikuwa anawapa taarifa kwanza kwa kupiga simu zile za kukoroga kwamba ataenda muda fulani kuiba au kula nao
Wazungu walikuwa wanaweka ulinzi wote wa wakati huo lakini ukipita ule muda aliosema anawapigia simu na kuwaambia kuwa keshachukua kitu fulani