Tabia mojawapo kubwa sana ya Wachawi ni kuwa na husuda yaani wivu wa Hali ya Juu sana kutopenda kuona Mtu mwingine alifanikiwa , akiendelea , hapendi kuona Mtu amekula vizuri akashiba, hapendi kuona Mtu kavaa vizuri na kupendeza, hapendi kuona wana ndoa wakielewana na kustawi, hapendi kuona Mtu anafaulu shuleni, hapendi kuona Mtu ana Gari au Nyumba nzuri, n.k mbaya zaidi yani kubwa kuliko uchawi ni dhambi yenye kurithiwa toka kizazi hata kizazi, Mtu aweza kuwa mlevi au mwizi lakini siyo lazima kuwepo na mrithi wa ulevi au Wizi , lakini familia/Ukoo ukiwa na mchawi basi lazima urithiwe na Mtu wa karibu ! Au mnasemaje akina Mshana jr, mzizi mkavu etc? Je hili ni Kweli au siyo Kweli? Na kiukweli jaribu kufuatilia maeneo yenye kusifika Kwa uchawi angalia Kama kuna maendeleo [emoji87][emoji87][emoji87] maana kila Watu wakijaribu kuinuka ktk Nyanja mbalimbali wanarudishwa nyuma ! Angalia Bagamoyo iko karibu na Dar, Tanga n.k ndo maana wengine hawathubutu kujaribu kujenga makwao