Wachawi wanavyoiba nyota za watu wanafanyaje?

Wachawi wanavyoiba nyota za watu wanafanyaje?

habari za uchawi ni uongo na utapeli . Tuanze zungumzia nyota , nyota na binadamu wanamahusiano yapi sijaona uhusiano kati ya hydrogen za kwenye nyota na binadamu duniani.
tuje kwenye uchawi, mchawi anawezaje kuzuia binadamu mwenzaje asifanye jambo tena kwanamna ambayo sio kisheria wala kimafizikia. Habari za wachawi ni zakusimuliwa hamna mtu huja kusema amemshuhudia mchawi bali husema amesimuliwa.
ndugu zangu watanganyika tuwekeze kwenye sayansi ya kweli tuachane na hekaya hizi mambo hayo ni yazamani sana hayana ukweli wala uhalisia
nyie mnaojkutaga n waelewa sana et sayans na tcnlogia ndio ua mko empty box hata ao wazungu unao waamn kwa kutofatilia hayo mambo uwez kufanya nao kaz kama awajachek astronolgy yako kujua ww n mtu wa aina gan ndio mana kama unanyota kubwa sahau kula shavu na wazungu utaskia yule jamaa alkua housboy tu leo yuko mbele na wale wazungu wa kanisa flan, Weka akil yako katika mapokeo ya kujfunza vtu vipya sio kile unachokijua tu jfunze na usvyo vjua dunia n zaid ya uijuavyo
 
*Una nyota ya kuwa mtu maarufu hasa kwa upande wa burudani

*Wewe ni kiongozi

*Unaweza kuwa wa kwanza kwenye chochote kama ukiweza kutambua madhaifu yako na kuyatendea kazi

*Mchawi wako mkubwa anayekuloga ni EGOISM

Nikipata muda nitakuandikia zaidi

Weekend njema kwako
Tangu 3rd july
 
Niliwahi kushauriwa baada ya kuona nilikuwa na bahati sana kila kitu mbaka marafiki wengi walikuwa wananionea wivu, mfano tu hata mademu walikuwa wananigombania kabisa unashuhudia unakuta demu anaacha anakoenda naenda kula tena simjui hanijui nimekutana naye road tu, ukija kila nachofanya kinaenda, ikaja kuharibika kila kitu hovyo tu mbaka nikawa napiga punyeto mademu sina kabisaa nikitingoza nazungushwa nawakati nilikuwanatongozwa mimi yaan true kabisaa hapo ndipo nikahisi uchawi upo na nyota ya mtu huaribiwa kabisaa
 
Niliwahi kushauriwa baada ya kuona nilikuwa na bahati sana kila kitu mbaka marafiki wengi walikuwa wananionea wivu, mfano tu hata mademu walikuwa wananigombania kabisa unashuhudia unakuta demu anaacha anakoenda naenda kula tena simjui hanijui nimekutana naye road tu, ukija kila nachofanya kinaenda, ikaja kuharibika kila kitu hovyo tu mbaka nikawa napiga punyeto mademu sina kabisaa nikitingoza nazungushwa nawakati nilikuwanatongozwa mimi yaan true kabisaa hapo ndipo nikahisi uchawi upo na nyota ya mtu huaribiwa kabisaa
Mbona umeishia njiani?
 
Umeeleweka sana mkuu. Mimi juzi kwenye kundi la Whatsapp la ofisi niliwachana na mtu niliyekuwa ni target yangu ujumbe aliupata na baada ya siku moja tukawa na kikao akawa hana amani.Uchawi wa kuiba nyota upo na huwa wakishindwa, wanaichafua .
Kuna jamaa nilimlea (alisomea) kwangu hadi akapata kazi. Akaja kutamani cheo kazini kwao, akaenda Tanga kwa Mandondo eti mganga (mimi naita mchawi) amfanyie maarifa apande cheo. Mchawi akamwambia mtoe ndugu yako kafara, harakaharaka akanitoa mimi, mchawi akahangaika kweli bila mafanikio, jamaa akamwambia mbona hakuna matokeo, mchawi akamwambia huyu uliyemtoa ni ndugu yako wa damu kweli? Mbona mizimu inamkataa? Inataka ndugu yako wa damu! Akasema siyo ndugu yangu wa ndani, mchawi akasema kama siyo ndugu yako wa damu kafara haitakubali, wakamalizana bila mafanikio. Siku moja huyu jamaa akakosana na mpwa wake aliyemsindikiza kwa Mandondo; hadi akamtia ndani Polisi, huyu Mpwa kikamuuma ni kwanini mjomba anitie Polisi? Natoa siri zake, ndiyo mimi kuambiwa kuwa nilitolewa kafara lakini mizimu ya mchawi ikagoma. #Kikulachokiinguonimwako.
 
Kuna jamaa nilimlea (alisomea) kwangu hadi akapata kazi. Akaja kutamani cheo kazini kwao, akaenda Tanga kwa Mandondo eti mganga (mimi naita mchawi) amfanyie maarifa apande cheo. Mchawi akamwambia mtoe ndugu yako kafara, harakaharaka akanitoa mimi, mchawi akahangaika kweli bila mafanikio, jamaa akamwambia mbona hakuna matokeo, mchawi akamwambia huyu uliyemtoa ni ndugu yako wa damu kweli? Mbona mizimu inamkataa? Inataka ndugu yako wa damu! Akasema siyo ndugu yangu wa ndani, mchawi akasema kama siyo ndugu yako wa damu kafara haitakubali, wakamalizana bila mafanikio. Siku moja huyu jamaa akakosana na mpwa wake aliyemsindikiza kwa Mandondo; hadi akamtia ndani Polisi, huyu Mpwa kikamuuma ni kwanini mjomba anitie Polisi? Natoa siri zake, ndiyo mimi kuambiwa kuwa nilitolewa kafara lakini mizimu ya mchawi ikagoma. #Kikulachokiinguonimwako.
Umemaliza.! Case closed!
 
Fanya Sanaa na utakuja kunishukuru

Wewe ni msanii wa kuzaliwa, Angalia hata jina lako hapa JF

UNA Nyota kubwa ya kuwa mtu maarufu mkubwa

Una nyota kama ya SIMBA

Pia una tabia ya ubishi na unaweza kumbishia mtu yoyote

Kuna wengi wanaokuloga na mkuu wa hao wachawi kwako anaitwa EGOISM
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Inaibiwa kwa msaada wa majini,na waganga uiza kwa wenye pesa wahitaji.
Nyota ni biashara kubwa Sana kwa waganga na uwapatia pesa nyingi Sana.Nyota ni kipawa kipaji alichokuwekea Mwenyezi Mungu ,kwa maana kila anaezaliwa tayari Mungu ana mpango naye, wakati huo Mungu kampa mwanadamu akili ya kuchagua mema na mabaya maana Mungu sio dikteta.Ukimuacha Mungu nae anakuacha,ukimuita nae uitika,so unachagua nani awe boss wako.
Kwahiyo majini wanaichukua kutoka kwako wanaipeleka kwa mganga?
 
Kwa maono yangu ni mambo ya imani. Ila amini usiamini nyota huibwa kwa njia ya Kujamiiana, kushare vitu kiundani na ukaribu wa zaidi. Na nyota hizo hizo hupandishwa kwa dua na sala. Kama hujaelewa uliza hapa
Nyota zinapandishwaje?

Kupandishwa kwenda wapi?
 
Nijuavyo nyota ni kama karama ambayo mtu amebarikiwa nayo tangu kuzaliwa kwake. Sio kila mtu anaweza kua nayo. Wenye hizo karama hua ni watu tofauti na karama tofauti kama mtu ana karama ya uongozi akisimama tu kila mtu anafurahi kumsikiliza. Au mwingine anachokishika chochote kinakua kitu kizuri.

Penye uzuri napo shetani naye anapenda kuingia ndio hapo anaweza tumia uwezo wake wa kuiba nyota ya mtu on which kama mtu ana kitu rohoni mwake kiimani huyo shetani awez kuchukua.
Kwahiyo nyota inakaa rohoni? sio mwilini?

Mchawi anaweza kufika kwenye roho mtu?

Kumbuka roho ya mtu ina nguvu za kimungu! Mchawi anaweza kuingia huko? Kwa namna gani?
 
Umeeleweka sana mkuu. Mimi juzi kwenye kundi la Whatsapp la ofisi niliwachana na mtu niliyekuwa ni target yangu ujumbe aliupata na baada ya siku moja tukawa na kikao akawa hana amani.Uchawi wa kuiba nyota upo na huwa wakishindwa, wanaichafua .

Washenzi sana
Dawa yao ni Kumuomba Mungu sana na Dua kwa wingi
 
Mambo ya nyota ni mambo ya kiroho na yako katika ulimwengu wa roho. Ni kweli mtu au watu uweza kuiba au kuchukua nyota ya mtu. Yaweza kuwa kwa njia za kichawi, majini, au nguvu zozote zile za giza katika ulimwengu wa roho. Haya mambo yamekuwepo enzi na enzi.
Katika Biblia Mathayo 2:1, 2. Kuna wise men( wenye hekima au Watabiri nyota) waliuliza

"yu wapi mfalme mpya alozaliwa, maana tumeona nyota yake tulipokuwa mashariki".

Hii haikumaanisha nyota kama nyota ya mwonekano. Na utajiuliza kwa nini hawa wisemen watatu ndo waliona hii nyota si wengine. Herode alituma watabiri wakaangalie yu wapi huyu Yesu alozaliwa. Hawa jamaa baada ya kufika kule walimwona Yesu na Mamake. Walipotaka kuondoka waliona nyota ya yule mtoto Yesu imechafuka ikionesha mauaji ya mtoto mdogo asie na hatia. Ndipo Mungu akawambia wasirudi kwa Herode. Mathayo 2:12.

Nimenukuu kutoka katika Biblia kuonesha binadamu tunanyota na nyota ndo muongozo wa maisha. katika nyota unaweza mjua mtu ni nani na atakuwa nani. Haya mambo yapo katika Ulimwengu wa roho. Hawa watabiri wa nyota tayari walishaona nyota ya mtoto aliezaliwa na walisema mfalme mpya alie zaliwa. Hivyo nyota ya Yesu ilionesha ni mfalme. Hii ilimuuzi Mfalme Herode na kuamru watoto wadogo miaka 2 hadi 0 kuuwawa.
Maswala ya wizi wa nyota ni somo refu saana. Kwa kifupi!
Viganja vya mkono uonesha nyota ya mtu. Hii ni pamoja na nyayo.
Paji na macho uonesha nyota ya mtu.

Kuwa makini na mtu anae kutazama sana katika paji lako au machoni huku kakaza macho yake. Na hasa anaweza kukuangalia wakati weye umeyumbisha macho umuoni uzuri. Kuna uchawi wa macho. Nchini Ethiopia, uchawi huu hutumika hasa mtu anapokuwa na kinyongo nawe, au kijicho. Hivyo uchukua nyota yako nawe kubaki unaangaika sana.

Kuna kitabu kinaitwa "Mind of an Eye" kama sijakosea ni kikubwa kwa wingi wa page. Na pia ni kipana. Kimeeleza mengi juu ya nguvu za jicho. namna binadamu unavyoweza kubadilika hata ukatoweka mfano upo Dar lakini ukafika Mwanza hata arabuni. kinafundisha uponyaji na mambo mengi katika ulimwengu wa roho.

Hivyo jicho linaweza chukua nyota ya mtu. Ndo maana mtu anaweza sema fulani kaniangalia kwa jicho baya. Jicho linanguvu za ajabu kwani uweza kuona hata yalofichika.
Nyayo au kiganja kimebeba mwili wa mwanadamu. Taswira ya mtu unaipata katika nyayo au kiganja chake. Ndo maana wengine, uchota nyayo za mtu ili kummaliza. Au uchukua maandishi ulioandika kwa viganja vyako. hata kama ni karamu ilikamatwa na kiganja hivyo ni rahisi katika ulimwengu wa roho kuchukua reflection yako.

Kuna kuchukua nyota yako kupitia jina la ukoo wako, jina la ukooo linanguvu na hasa kama ni la babu yako. haya majina hutumika kukujua vizuri wewe na ukoo wako. Nguvu zenu kiroho na nyota yako.
Mchawi hawezi kuroga kama yupo kawaida, mpaka ajibadili aingie katika ulimwengu wa roho. ndiyo maana huwezi mshika au hata kumuona.

Anapoamua kuonekana kuna jambo au pia wewe katika ulimwengu wa roho unanguvu. Hivyo kuichukua nyota yako itahitajika kwanza aifahamu, na afahamu ukoo wako kisha katika ulimwengu wa roho anaiiba au kuichukua nyota yako.

Na mara nyingi hawaichukui wawe nayo wao lah asha. Wanaiondoa tu kwako ili pengine usifanikiwe, uteseke, au tu uangaike. Kwani ni ngumu nyota ya mtu kutumika kwa mwingine. Hivyo wakiichukua maana yake wanaondoa baraka zako, wanakufunga. isipokuwa hawawezi kuitumia nyota yako.

Narudia tunatumia tu neno nyota uchukuliwa, si kwamba wanaichukua waitumie hapana. Uwezi tumia nyota ya mtu mwingine kwa sababu kila mtu anapozaliwa uzaliwa na nyota yake. Kikubwa wanaiondoa ile nyota kwako, kwa sababu za husuda, roho mbaya, na mengineyo ili ubaki ukiteseka na usifikie ambacho nyota yako inaonesha hapa duniani ungekuwa nani, au mtu wa namna fulani.
Hivyo nyota yako ufichwa mahala. Ndo maana katika maisha omba, ombea wanako au familia. Ili Mungu akulinde weye na familia yako. Unajua kuna watu wa ajabu ktk hii dunia, mtu akiona weye ni mzuri ktk jambo fulani au umefanikiwa kiasi fulani basi anakumaliza kwa ulimwengu wa roho.
Japo kuna watu wanajifanya hawaamini haya mambo lakini yapo. Yana nguvu sana. Kuwa makini na watu ulionao karibu. Hao ndo wakwanza kwa kijicho na husuda. Mtu hata kama si mchawi atakuendea kwa wataalamu au waganga ili waiharibu nyota yako. Usifanikiwe! Kila siku utajiona ni mtu wa mikosi na balaa. Au unajitahidi kufanya hiki hakiendi. Wanafunga nyota yako!
Angalau hapa naanza kuelewa.

Wanaifunga nyota kwa namna gani?

Ni kitu kinachoweza kuonekana kwenye roho? Wanakifungaje?
 
NILICHOJFUNZA NDANI YA UZI HUU
-> Nlahisi kdogo kupambana na roho
Unayoihisi kuliko kupambana
na roho Ambayo hata kuihisi uhisi

"Ngoja NIJARIBU kuelezea nlicho jfunza katika uzi huu NIONE kama NTAWEZA"

Hapo juu ni mstari wa kwanza nilioanza kuandika ila kipindi nilpo fka kuandika neno NIJARIBU akili yangu ikani alert hapa kwamba umevamiwa na mchawi wa kutojiamini ... nkasema ngoja niandike mstari ambao hautokuwa na nguvu Za kutojiamini na mstari wa pili ambao umekamilika ukiwa umejawa na nguvu ya kujiamini ndani yake ni huu apa ( nyota safi kabis)...

"Ngoja nielezee nilicho jifunza katika uzi huu".

Tunaendele na nilichojfunza sasa..
Ambacho nlikuwa sina picha nacho juu ya tabia/nyota ni kwamba tabia ni roho au watu kabisaa

Nmesema ni watu kwa sababu roho katika ulimwengu wa roho ni sawa na watu katika ulimwengu wa wanyama

Apo mwanzo kabla ya uzi huu na wakufunzi kufundisha juu ya nyota nlkuwa sina hii alert ya kuona kwamba saiv roho gani au mchawi gani kanivamia katika hisia zangu,


Kwa mfano nlpokuwa naandika paragraph ya kwanza unconsciously nlkuwa sioni mlango ambao roho/mchawi wa kutojiamini anaingilia..
Ila baada ya kupata picha ya wachawi wangu ni kutojiamini,tabia kubadilika badilika nk... sasa mentality nawaona ,
kwa sababu nimezchukulia hizo tabia kama watu .
Hiyo inamaana kwamba unapojisikia au unapo hisi kutojiamin maana yake kwamba mchawi wako kawasili mwilin mwako au kwenye nyota yako au kwenye tabia yako

Uzuri ni kwamba hisia zote Za kutojiamini au uvivu nk.. ukzchukulia kama watu wachawi wako unaziona znavyokuvamia kwenye mwili wako

Kingine nahisi.... Hisia ni njia ya kukuonesha mchawi gani kakuvamia
Ukijihisi uvivu jua kabisa wanyamwez wa kutotaka usifanikiwe wAnafanya kazi yao , au kbuyu walichokuwekea kmetkisika uko .. hahah

Nilitaka kumalizia na mstari
"Sijui nmeeleweka", ila nmegundua kuwa huo ni mlango wa mchawi kutojiamini anao ingilia

............. ........... ....... ........... ..........


shukrani kwa walimu wote wanao hakikisha jamii inapata uelewa sahihi wa nyota
Eleza kwa lugha rahisi.
 
Back
Top Bottom