Mambo ya nyota ni mambo ya kiroho na yako katika ulimwengu wa roho. Ni kweli mtu au watu uweza kuiba au kuchukua nyota ya mtu. Yaweza kuwa kwa njia za kichawi, majini, au nguvu zozote zile za giza katika ulimwengu wa roho. Haya mambo yamekuwepo enzi na enzi.
Katika Biblia Mathayo 2:1, 2. Kuna wise men( wenye hekima au Watabiri nyota) waliuliza
"yu wapi mfalme mpya alozaliwa, maana tumeona nyota yake tulipokuwa mashariki".
Hii haikumaanisha nyota kama nyota ya mwonekano. Na utajiuliza kwa nini hawa wisemen watatu ndo waliona hii nyota si wengine. Herode alituma watabiri wakaangalie yu wapi huyu Yesu alozaliwa. Hawa jamaa baada ya kufika kule walimwona Yesu na Mamake. Walipotaka kuondoka waliona nyota ya yule mtoto Yesu imechafuka ikionesha mauaji ya mtoto mdogo asie na hatia. Ndipo Mungu akawambia wasirudi kwa Herode. Mathayo 2:12.
Nimenukuu kutoka katika Biblia kuonesha binadamu tunanyota na nyota ndo muongozo wa maisha. katika nyota unaweza mjua mtu ni nani na atakuwa nani. Haya mambo yapo katika Ulimwengu wa roho. Hawa watabiri wa nyota tayari walishaona nyota ya mtoto aliezaliwa na walisema mfalme mpya alie zaliwa. Hivyo nyota ya Yesu ilionesha ni mfalme. Hii ilimuuzi Mfalme Herode na kuamru watoto wadogo miaka 2 hadi 0 kuuwawa.
Maswala ya wizi wa nyota ni somo refu saana. Kwa kifupi!
Viganja vya mkono uonesha nyota ya mtu. Hii ni pamoja na nyayo.
Paji na macho uonesha nyota ya mtu.
Kuwa makini na mtu anae kutazama sana katika paji lako au machoni huku kakaza macho yake. Na hasa anaweza kukuangalia wakati weye umeyumbisha macho umuoni uzuri. Kuna uchawi wa macho. Nchini Ethiopia, uchawi huu hutumika hasa mtu anapokuwa na kinyongo nawe, au kijicho. Hivyo uchukua nyota yako nawe kubaki unaangaika sana.
Kuna kitabu kinaitwa "Mind of an Eye" kama sijakosea ni kikubwa kwa wingi wa page. Na pia ni kipana. Kimeeleza mengi juu ya nguvu za jicho. namna binadamu unavyoweza kubadilika hata ukatoweka mfano upo Dar lakini ukafika Mwanza hata arabuni. kinafundisha uponyaji na mambo mengi katika ulimwengu wa roho.
Hivyo jicho linaweza chukua nyota ya mtu. Ndo maana mtu anaweza sema fulani kaniangalia kwa jicho baya. Jicho linanguvu za ajabu kwani uweza kuona hata yalofichika.
Nyayo au kiganja kimebeba mwili wa mwanadamu. Taswira ya mtu unaipata katika nyayo au kiganja chake. Ndo maana wengine, uchota nyayo za mtu ili kummaliza. Au uchukua maandishi ulioandika kwa viganja vyako. hata kama ni karamu ilikamatwa na kiganja hivyo ni rahisi katika ulimwengu wa roho kuchukua reflection yako.
Kuna kuchukua nyota yako kupitia jina la ukoo wako, jina la ukooo linanguvu na hasa kama ni la babu yako. haya majina hutumika kukujua vizuri wewe na ukoo wako. Nguvu zenu kiroho na nyota yako.
Mchawi hawezi kuroga kama yupo kawaida, mpaka ajibadili aingie katika ulimwengu wa roho. ndiyo maana huwezi mshika au hata kumuona.
Anapoamua kuonekana kuna jambo au pia wewe katika ulimwengu wa roho unanguvu. Hivyo kuichukua nyota yako itahitajika kwanza aifahamu, na afahamu ukoo wako kisha katika ulimwengu wa roho anaiiba au kuichukua nyota yako.
Na mara nyingi hawaichukui wawe nayo wao lah asha. Wanaiondoa tu kwako ili pengine usifanikiwe, uteseke, au tu uangaike. Kwani ni ngumu nyota ya mtu kutumika kwa mwingine. Hivyo wakiichukua maana yake wanaondoa baraka zako, wanakufunga. isipokuwa hawawezi kuitumia nyota yako.
Narudia tunatumia tu neno nyota uchukuliwa, si kwamba wanaichukua waitumie hapana. Uwezi tumia nyota ya mtu mwingine kwa sababu kila mtu anapozaliwa uzaliwa na nyota yake. Kikubwa wanaiondoa ile nyota kwako, kwa sababu za husuda, roho mbaya, na mengineyo ili ubaki ukiteseka na usifikie ambacho nyota yako inaonesha hapa duniani ungekuwa nani, au mtu wa namna fulani.
Hivyo nyota yako ufichwa mahala. Ndo maana katika maisha omba, ombea wanako au familia. Ili Mungu akulinde weye na familia yako. Unajua kuna watu wa ajabu ktk hii dunia, mtu akiona weye ni mzuri ktk jambo fulani au umefanikiwa kiasi fulani basi anakumaliza kwa ulimwengu wa roho.
Japo kuna watu wanajifanya hawaamini haya mambo lakini yapo. Yana nguvu sana. Kuwa makini na watu ulionao karibu. Hao ndo wakwanza kwa kijicho na husuda. Mtu hata kama si mchawi atakuendea kwa wataalamu au waganga ili waiharibu nyota yako. Usifanikiwe! Kila siku utajiona ni mtu wa mikosi na balaa. Au unajitahidi kufanya hiki hakiendi. Wanafunga nyota yako!