Wachezaji 12 wageni kwenye timu ni sumu kwa Taifa stars

Wachezaji 12 wageni kwenye timu ni sumu kwa Taifa stars

Kaka exposure ni jambo kubwa katika kufanilisha mission. Wachezaji wetu hawapi exposure kubwa ndani ya timu kutokana na wageni wengi na hawakupata exposure AFCON, wameachwa nyumbani, watakuwa lini? Tanzania kwasasa hatuna mshambuliaji mzawa zaidi ya Mzize, ambae nae ameachwa AFCON hii, unadhani AFCON ijayo atakawa Bora kutoka wapi?
Kuwa na wageni wengi wanao cheza ligi si tatizo, Inatakiwa wachezaji wetu waongeze Level za kiwango.
Samata, Msuva, Novatus Dismas n.k wote walitokea katika ligi hii kwenda nje na wageni walikuwepo.
Tatizo mpira/michezo ili ufanikiwe ucheze katika Top level Inatakiwa ujitoe na kuacha kila starehe na wengi Wana shindwa hasa wakianza kupata jina.
 
Brother , Naamini kungekuwepo na combination ya mzize na kibu plus msuva tungepata matokeo .
Mzize amefundishwa hata kukaba.

Hata France , Giroud alionekana Hafungi au kufanya kitu kikubwa lakini alikuwa na kazi maalumu ya kupunguza mabeki wawe busy kwake ili nafasi ipatikane .
Mzize ni mpambanaji na siku akiwa Kwenye form ni hatari.
mpaka siku akiwa kwenye form?
 
Yaani mtu akiwa anacheza nje ya TZ hata kama huko anacheza rede tayari utashangaa anaitwa timu ya Taifa-Taifa Stars
 
mpaka siku akiwa kwenye form?
Asipikuwa Kwenye form asingefunga lakini bado angetoa mchango kwa kupambana .
Wachezaji walioenda Afcon asilimia kubwa walionyesha kutopambana asilimia 100 walikuwa wavivu na wachovu.

Mechi ya Zambia ndiyo ilikuwa imetuvusha.
Wanakuja kushituka kujifunika jana wakati kumeshapambazuka .
 
Nini kilimtoa huyu Amahl Kwenye kikosi ??
Halafu wanawekwa wachezaji daraja la 5 na 7?


 
Kimsingi idadi ya wachezaji wa nje ilitakiwa kubakia ile ya wachezaji 7! Mambo ya kuruhusu wachezaji 12, ndiyo yanayobabisha timu kama Yanga kusajili wachezaji kutoka nje, kwa ajili ya burudani tu!
 
Pelekeni Vijana wadogo wakutosha kwenda Ulaya kucheza Mpira...!

Haya mawazo mfu ya kuzuia Team kusajiri wachezaji 12 ni Ujinga, Ushamba na kutoona wenzetu wanafanya nini...!

Hivi Wachezaji wa Simba na Yanga watafanya nini kushindana na Team za Mataifa mengine ya West Africa!?

Asilimia 90℅ ya Team zinazoshiriki Afcon, Nusu ya First eleven ni Wachezaji ambao hawakuzaliwa hata kwenye Mataifa yao, Means wote hao wamezaliwa Ulaya na wanacheza Ulaya, then wachezaji 3 ama 4 ndo wamezaliwa kwenye Nchi zao na wote wanacheza Ulaya, then Mchezaji mmoja tu nd anacheza Africa, na kweyewe kucheza tu Africa haitoshi, utasikia Al ahly, Mamelodi, Wydad etc, Hawa Akina Mzinze na Bajana watakusaidia ninj dhidi Wachezaji wanaocheza Ligi kubwa za Ulaya...!?

Tunataka tupambane na West africa, tupite Njia zile zile, leo Cape Verde imewatoa Jasho Miamba ya Soka la Africa,nchi yenye watu Mil. 1 tu, ila Team nzima inacheza Ulaya, wakirudi Africa, wanaonyesha Ubora wao.....!

Unataka kushindana na Waliofanikiwa, pita njia yao..
 
12 timu zimetoka tena zingne timu kumbwa na zenye historia kubwa afrika zmetoka na tena zimetoka zikiwa na point 2 sawa na taifa stars

Ila hatuoni kua uwo ni mchozo sasa tunatafta wakumtupia walawa ebu tuache tabia za Wana Simba ndo huwa hawana uvumilivu na awapendi kukubali matokeo

Algeria point2
Ghana point2
Tunisia point2
Mm sio mtu wa mpira yawezekana nachangia point au pumba na yawezekana takwimu zisiwe za ukwel ila tuache lawana na tukubali kushindwa tujipange upya AFCON ipo sana one day yes tutafka final
 
Timu kubwa ilizotaja zina wachezaji wageni zaidi ya asilimia 80% ktk first 11 zao hao wazawa watatoka wapi
 
Kwa wale wenye kufahamu soka letu si Dhani kama wanaweza kuwatupia lawama Tff.
Mimi nawapongeza wote, Tff, wachezji, wadau Kila mmoja kwa kupambania na kufanikisha kupata point 2 katika michuano hii ya AFCON.
Tangu tumeanza kushiriki AFCON hatujawahi kupata point 2.

Tunawachezaji wengi wa ndani ambao hawapati ushindani wa kutosha kuwezesha kushindana AFCON, atakama tunge waongeza wakina Mzize, Kibabage, Kijiri, Islael Mwenda n.k wasinge kuja na matokeo zaidi ya Aya tuliyo yapata.

Kwasasa kwakua hatuna njia ya kuwapeleka wachezaji nje na hatuna uraia pacha unao zibeba nchi nyingi kwenye AFCON, TFF kwa kushirikiana na wadau wakae pamoja na kutafuta njia ya kupata ushindani wa kutosha katika ligi yetu uku tukiangalia namna ya kuwezesha vijana wengi watoke na kwenda kwenye ligi zenye ushindani.
Tuanze na makocha wa kufundisha vijana, viwanja na vifaa vya michezo.

Tupunguze kasoro kwa waamuzi, Tupunguze upendeleo wowote kwa baadhi ya vilabu, tuache mpira uchezwe bila mbeleko ili ushindani uonekane.

Wachezaji wetu wajifunze kupitia AFCON kua kipaji pekeyake hakina msaada wowote bila mazoezi makali ya kujiua na kujituma kwa viwango vya juu ili wale mema ya Nchi.
Point 2 zinafaida gani!? TFF mnajielewa kweli!!!
 
Comfort zone sawa na ile kwamba hata new york umeme unakatika.
Maendeleo ni hatua, hii ni mara yetu ya 3 tu kushiriki unataka hapohapo ufike hadi robo ama nusu fainali? Huwezi kupaa kabla hujajifunza kukimbia.
 
12 timu zimetoka tena zingne timu kumbwa na zenye historia kubwa afrika zmetoka na tena zimetoka zikiwa na point 2 sawa na taifa stars

Ila hatuoni kua uwo ni mchozo sasa tunatafta wakumtupia walawa ebu tuache tabia za Wana Simba ndo huwa hawana uvumilivu na awapendi kukubali matokeo

Algeria point2
Ghana point2
Tunisia point2
Mm sio mtu wa mpira yawezekana nachangia point au pumba na yawezekana takwimu zisiwe za ukwel ila tuache lawana na tukubali kushindwa tujipange upya AFCON ipo sana one day yes tutafka final
Uko sahihi mkuu. Tatizo watz ni watu wa lawama sana. Mie ninawapongeza sana Stars kwa hatua hii kubwa walofikia. Ni mwanzo mzuri sana. Timu kubwa tu zimeshindwa kufaulu hatua ya mtoano na zingine zimepita kwa bahati nasibu mfano Ivory Coast mwenyewe.
 
12 timu zimetoka tena zingne timu kumbwa na zenye historia kubwa afrika zmetoka na tena zimetoka zikiwa na point 2 sawa na taifa stars

Ila hatuoni kua uwo ni mchozo sasa tunatafta wakumtupia walawa ebu tuache tabia za Wana Simba ndo huwa hawana uvumilivu na awapendi kukubali matokeo

Algeria point2
Ghana point2
Tunisia point2
Mm sio mtu wa mpira yawezekana nachangia point au pumba na yawezekana takwimu zisiwe za ukwel ila tuache lawana na tukubali kushindwa tujipange upya AFCON ipo sana one day yes tutafka final

Kwa hivyo Taifa Stars ilienda AFCON kupata point mbili?
 
Lawama la kushindwa kwa Taifa stars AFCON kwanza liende kwa TFF kabla ya sehemu nyingine. Timu zetu kubwa kwenye ligi haziandai Wachezaji wa kuichezea timu ya taifa kwakuwa wamepewa ruksa ya kutafuta wachezaji 12 nje ya nchi. Hii inasababisha vijana kama Mzize na wengine wasipate muda wa kukosea na kusahihisha makosa Yao ndani ya timu zao. Timu za Simba, Yanga na Azam Zina miundombinu na mabechi mazuri ya ufundi, ndizo zingepaswa kutoa washambuliaji wazuri kwenye timu Yao ya Taifa lakini wapi wee, wanawatumia wageni ambao wanatufunga tunapokutana nao kwenye mashindano ya CAF.

Lawama ingine kubwa iende kwenye uteuzi wa timu, tumeteua wachezaji kutoka nje wengi ambao hatuwajui vizuri na kuwaacha tunaowajua vizuri akina Mwenda, Mzize, kyombo na wengine. Hawa vijana wangeenda kule wangejifunza mengi sana.

Lawama ingine ni wizara ya michezo, inaonekana zaidi wakati wa mashindano zaidi kuliko wakati wa maandalizi ya wachezaji. Hi serikali haioni kuwa wachezaji 12 kila timu inaiua timu ya Taifa? Viwanja vyetu vingi ni vya CCM na vibovu, viwanja vya serikali vizuri viko wapi? Kwanini serikali haihoji timu kubwa kukosa viwanja au kwaajili ya conflict of interest ña viwanja vya CCM na uwanja wa taifa dhidi ya viwanja vya timu? Maana wanajua kama kila timu ikimiliki uwanja wake viwanja vya CCM vitabaki vya kichezea magwaride ya sherehe za muungano. Vijana wa makocha wazuri? Vitaru vya watoto viko wapi? Sera ya michezo ipo? shule Zina viwanja?
Lawama kubwa ni kwa Serikali, hizi Nchi zetu changa bila mkono wa Serikali hakuna kupiga hatua. Inategemea kweli Simba, Yanga, Ruvu wawe na Academy za kueleweka wakati hata udhamini haupo. Tuwe siriasi kama Uganda, michezo iwe sehemu ya Shule. Hakuna kucheza Mpira hadi uandikishwe Shule. Huko wawepo walimu wa michezo.
 
Viongozi wa juu wanaofanya maamuzi huko TFF wote ni Watanzania ? inabidi ile kauli ifanyiwe kazi !
sio tff tuu kwani dotto yule jamaa aliyepewa cheo kipya kisichokuwepo kwenye katiba ni mtanzania??
 
Back
Top Bottom