Wachezaji 12 wageni kwenye timu ni sumu kwa Taifa stars

Wachezaji 12 wageni kwenye timu ni sumu kwa Taifa stars

Brother , Naamini kungekuwepo na combination ya mzize na kibu plus msuva tungepata matokeo .
Mzize amefundishwa hata kukaba.

Hata France , Giroud alionekana Hafungi au kufanya kitu kikubwa lakini alikuwa na kazi maalumu ya kupunguza mabeki wawe busy kwake ili nafasi ipatikane .
Mzize ni mpambanaji na siku akiwa Kwenye form ni hatari.
Mzize, Kibu, Msuva ingekuwa combination hatari sana, wana vimo na nguvu kama za wachezaji wa Afrika Magharibi, Kongo na Waarabu, wanakimbia na wanapenda kujaribu golini kila wakati. Wachezaji 6 tu wa kigeni wangetosha sana kwenye timu.
 
ghana na tunisia ni failures? Tanzania tuna nini kuwazidi hao jamaa?
Ghana na Tunia, Algeria kule kuna nyota ambao wanacheza kwa kubakiza miguu yao na nguvu zao kwaajili ya timu zao ulaya, wanacheza kwa kujisikilizia maana tayari wanayo mafanikio, lakini Mzize bado anajitafuta angekuwa tayari kufia uwanjani pale kuipambania timu na kujipambania yeye mwenyewe, kwa vyovyote vile angeongeza juhudi kumzidi Samatta ili atoke. Ona pale kwenye mashindani wachezaji wanaocheza kwenye ligi zao za ndani na ndani ya Afrika ndio waliokuwa wanacheza kwa nguvu na bidii kubwa kuliko mafather wa Ulaya. Salah anajifanya kuwa ameumia lakini ni uongo mtupu, hakuumia sana kivileee bali anaiwazia Liverpool.
 
Kuwa na wageni wengi wanao cheza ligi si tatizo, Inatakiwa wachezaji wetu waongeze Level za kiwango.
Samata, Msuva, Novatus Dismas n.k wote walitokea katika ligi hii kwenda nje na wageni walikuwepo.
Tatizo mpira/michezo ili ufanikiwe ucheze katika Top level Inatakiwa ujitoe na kuacha kila starehe na wengi Wana shindwa hasa wakianza kupata jina.
Hiyo sio kweli, bila kumpatia kijana nafasi mara kwa mara dk 90 hawezi kutoboa. Hawa makocha wakubwa wanaokuja Simba, Yanga, Azam, nk hawataki kujaribu wachezaji wadogo ili kulinda heshima na vibarua vyao. kwakuwa ana wachezaji 12 (zaidi timu) mahiri tayari kutoka nje anaamua kuchezesha hao hadi hapo watakapoumia, kuugua au kuwa na adhabu . Hata hawa akina Nondo, Bacca Ibrahimu, Fei, Mzize, Kibu walitokana na huruma ya Nabi na Robertihno tu kuwaamini dhidi ya wageni.
 
Hivi Tanzania kwenye viwango vya fifa wanashika nafasi ya ngapi? Timu ya Angola ilikuwa na wachezaji walioshiriki michuano ya vijana ya afcon iliyofanyika Tanzania, je wale wacheza wa Tanzania walioshiriki hiyo michuano wako wapi? Tanzania tuna academy ngapi? Wekezeni kwanza kwenye mpira hakuna matokeo ya shortcut.
 
Lawama la kushindwa kwa Taifa stars AFCON kwanza liende kwa TFF kabla ya sehemu nyingine. Timu zetu kubwa kwenye ligi haziandai Wachezaji wa kuichezea timu ya taifa kwakuwa wamepewa ruksa ya kutafuta wachezaji 12 nje ya nchi. Hii inasababisha vijana kama Mzize na wengine wasipate muda wa kukosea na kusahihisha makosa Yao ndani ya timu zao. Timu za Simba, Yanga na Azam Zina miundombinu na mabechi mazuri ya ufundi, ndizo zingepaswa kutoa washambuliaji wazuri kwenye timu Yao ya Taifa lakini wapi wee, wanawatumia wageni ambao wanatufunga tunapokutana nao kwenye mashindano ya CAF.

Lawama ingine kubwa iende kwenye uteuzi wa timu, tumeteua wachezaji kutoka nje wengi ambao hatuwajui vizuri na kuwaacha tunaowajua vizuri akina Mwenda, Mzize, kyombo na wengine. Hawa vijana wangeenda kule wangejifunza mengi sana.

Lawama ingine ni wizara ya michezo, inaonekana zaidi wakati wa mashindano zaidi kuliko wakati wa maandalizi ya wachezaji. Hi serikali haioni kuwa wachezaji 12 kila timu inaiua timu ya Taifa? Viwanja vyetu vingi ni vya CCM na vibovu, viwanja vya serikali vizuri viko wapi? Kwanini serikali haihoji timu kubwa kukosa viwanja au kwaajili ya conflict of interest ña viwanja vya CCM na uwanja wa taifa dhidi ya viwanja vya timu? Maana wanajua kama kila timu ikimiliki uwanja wake viwanja vya CCM vitabaki vya kichezea magwaride ya sherehe za muungano. Vijana wa makocha wazuri? Vitaru vya watoto viko wapi? Sera ya michezo ipo? shule Zina viwanja?
Siyo sababu ya msingi yaani mchezaji wa Tanzania Yuko mwenyewe na kipa anapiga puuuu kwakifupi hawajitumi ukiwa na wachezaji wengi wa kimataifa ndiyo vizuri maana unapokutana nao utaongeza uwezo wako ama mnataka tusubiri twenda kuongeza ujuzi kwenye timu za kimataifa? na ndiyo maana Tanzania hatuna namba 9 ya uhakika labda John B ambaye kwa sasa hawezi kutubeba,kumbukeni hizi club zinawekezwa na wanachama na wanachama wanataka matokeo haziwezi kusuburi watu wasio na uwezo
 
Ukiangalia shida kubwa ya hii Team ni kuanzia full back 2 winga zote mbili kiungo No 6 na 8 na Striker hakuna...Yule Msuva kibongo bongo ana miaka 37 umri huo mpirani ni shida Samata nae kachoka na ukizingatia kiungo Mao Mkami ana miaka 43 sasa huyo atachezesha timu???? Kwa hiyo Shida kubwa ni Hao mashabiki wa Simba na Yanga wanaoshambikia tu Ooh Jigi diaraa ooh Chama Ooh Okrah hao wachezaji hawaji kutusaidia team za Taifa baadae bora tungekua na Vijana wa Kitanzania wazuri wanawaunderstudy hao watu kwenye team hizo mana hizo ndio zina makocha wazuri na huduma nzuri angalau.

Game kama ya Zambia ukimuona Kibu Denis alishindwa kufunga Nafasi kama 3 za wazi yaani hajui hata afanye nn kwa level kubwa ile so shida iko Kwetu watz talalila kila pahala ujanja ujanja hatuna tunaloweza zaidi ya uongo unafiki kila sehemu....

Team inabeba mwijaku eti anamwmabia Fei Toto piga ya mbali ipi???? LAKINI madaraka seleman au Leodgar Tenga angeenda pale ana cha kuwambia hawa kiufundi..Mihamed Mwameja ana.cha kusema..Peter Tino ana cha kusema sasa unapeleka Baba Levo yaani nchi ina Ujinga hii sijaon duniani humu.
 
Mwinjaku na Mwana FA walicheza namba gani uwanjani, maana walikuwa huko Ivori
 
Lawama la kushindwa kwa Taifa stars AFCON kwanza liende kwa TFF kabla ya sehemu nyingine. Timu zetu kubwa kwenye ligi haziandai Wachezaji wa kuichezea timu ya taifa kwakuwa wamepewa ruksa ya kutafuta wachezaji 12 nje ya nchi. Hii inasababisha vijana kama Mzize na wengine wasipate muda wa kukosea na kusahihisha makosa Yao ndani ya timu zao. Timu za Simba, Yanga na Azam Zina miundombinu na mabechi mazuri ya ufundi, ndizo zingepaswa kutoa washambuliaji wazuri kwenye timu Yao ya Taifa lakini wapi wee, wanawatumia wageni ambao wanatufunga tunapokutana nao kwenye mashindano ya CAF.

Lawama ingine kubwa iende kwenye uteuzi wa timu, tumeteua wachezaji kutoka nje wengi ambao hatuwajui vizuri na kuwaacha tunaowajua vizuri akina Mwenda, Mzize, kyombo na wengine. Hawa vijana wangeenda kule wangejifunza mengi sana.

Lawama ingine ni wizara ya michezo, inaonekana zaidi wakati wa mashindano zaidi kuliko wakati wa maandalizi ya wachezaji. Hi serikali haioni kuwa wachezaji 12 kila timu inaiua timu ya Taifa? Viwanja vyetu vingi ni vya CCM na vibovu, viwanja vya serikali vizuri viko wapi? Kwanini serikali haihoji timu kubwa kukosa viwanja au kwaajili ya conflict of interest ña viwanja vya CCM na uwanja wa taifa dhidi ya viwanja vya timu? Maana wanajua kama kila timu ikimiliki uwanja wake viwanja vya CCM vitabaki vya kichezea magwaride ya sherehe za muungano. Vijana wa makocha wazuri? Vitaru vya watoto viko wapi? Sera ya michezo ipo? shule Zina viwanja?
wala hio sio issue hata kidogo,issue ni miundo mbinu ya kulea na kukuza vipaji kwa watoto wetu,ambako ndiko watakapofunzwa sayansi ya uchezaji mpira.makocha wazawa ukimuacha oscar mirambo,hakuna kocha mzawa mwenye elimu ya sayansi ya mpira,hao wote wengine ni wababaishaji tu,kuhusu hizo pointi 2 tulizopata haikuwa kazi ya kocha wazawa,bali adel amrouche ndiye aliyefanya hayo yote,hao makocha wetu walidandia tu mafanikio
 
Watanzania football sio fani yetu labda wachache sana waliojaliwa kipawa maalum. Watanzania labda BAO na MCHIRIKU. Tuwe wakweli, hata hao kina Samatta mapro, wamefanya Nini japo kimoja tu kilichoacha kumbukumbu afcon hii?
 
Tatizo tanzania kila kitu ni siasa, mtaani huku kuna madogo wanaupga mwingi sana hata ulaya hawakosi timu, tena 1st eleven. Utashangaa kila siku wachezaji ni wale wale nyumri zinaenda wamekalia uchawi wkt miguuni hamna kitu.
 
Leo Ihefu inacheza na Kagera sugar ikiwa na wachezaji 2 wazawa TU uwanjani, wengine 9 ni wageni. Tunaiua taifa stars.
 
Leo Ihefu inacheza na Kagera sugar ikiwa na wachezaji 2 wazawa TU uwanjani, wengine 9 ni wageni. Tunaiua taifa stars.
Pelekeni upumbavu wenu huko....Nyie wachezaj w kitanzania tunawajua tabia zenu mbovu...au kama vipi nendeni nyie mkacheze nje kwani mmezuiwa mafala ninyi....wachezaji wa kitanzania ni wachache sana wanaishi kama profesionals........yaani tukiandika matabia ya wachezaji wa kitanzania hapa tutataapika.......anyway ukiliangalia bunge la tanzania na viongozi waliopo serikali ni mfano wa tabia za wachezaji wa tanzania.....au tabia za shirika kama tanesco la kitanzania....au angalia reli....ukiona hujaelewa nenda hospitali za uma uone uozo wa watanzania....
 
Back
Top Bottom