Wachezaji Bongo waliovuma kwa muda mfupi kisha wakapotea kwenye soka

Wachezaji Bongo waliovuma kwa muda mfupi kisha wakapotea kwenye soka

Abubakary Mkangwa alicheza soka lake vizuri tu mpaka mwisho
Alitwaa ubingwa na Mtibwa Sugar mara mbili mara ya mwisho mwaka 2000 alichukua ufungaji bora mtibwa sugar ikiwa chini ya mwalimu Thom Olaba kama sijakosea.
Abubakari mkangwa
Salihina mjengwa
Athuman Machupa
Abuu mtiro
 
Hujamtendea haki Echesa, Huyu alicheza misimu mingi sana pale kenya baadae alienda Malaysia akacheza misimu miwili ndipo aliposajiliwa na Simba akacheza misimu miwili pia alipoondoka alirejea kenya tena akaendelea kucheza ligi kuu ya kenya kama sijakosea .
Hilary Echesa
 
Pale Mtibwa Sugar, kuna nahodha kiongozi Shaban Nditi. Amecheza soka la kiwango cha juu kwa muda mrefu bila kuchuja. Amedumu sana kwenye soka la ushindani hapa Bongo.

Ukifika kwenye kikosi cha Kagera Sugar wanankurukumbi, utakutana na George Kavila Master. Ni karibia miaka 20 sasa anacheza ligi kuu ya Tanzania. Ni moja kati ya wachezaji wakongwe na wenye nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja.

Lakini habari ni tofauti kwa baadhi ya wachezaji wengine. Kuna wachezaji wa kibongo waliovuma kwa muda mfupi kisha wakapotea kabisa katika ramani ya soka.

Leo, tujikumbushe list ya wachezaji hao.

Mimi naanza na hawa wafuatao...
Rashid Gumbo

Said Bahanuzi

Jerry Tegete

Endelea na wewe...



Sent using Jamii Forums mobile app
Ali Mohammed SHIBOLI.
 
Credo Mwaipopo aliwahi sana kutoka kwenye mainstream

Pia kuna kipa mmoja Mengi Matunda
 
Back
Top Bottom