Wachezaji wa kuchungwa kuelekea Derby ya Kariakoo, Yanga Vs Simba

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Derby ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba ni moja ya mechi kubwa zaidi nchini, ikijaa ushindani ndani ya uwanja na tambo kutoka kwa mashabiki wa timu hizo mbili za mtaa wa Kariakoo.

Hapa ni nyota wa kutazama kwenye derby hii.

Kibu Denis

Tangu ajiunge na Simba, Kibu amekuwa mwiba hasa kwenye mechi za watani wa jadi. Katika derby alizocheza, amefanikiwa kufunga mabao mawili. Katika mchezo wa mwisho, alichezewa faulo nyingi kuliko mchezaji yeyote uwanjani.
Gk9nt3kWEAA-pBF.jpg

Pacome ZouZoua

Mmoja wa wachezaji hatari anapopata nafasi ya kushambulia. Mikimbio yake na uwezo wa kupunguza wachezaji zaidi ya mmoja huleta tishio langoni kwa wapinzani.

GkeyprzXkAALWNx.jpg
Elie Mpanzu

Hii itakuwa derby yake ya kwanza tangu ajiunge na Simba dirisha dogo. Ameonyesha uwezo mkubwa na anatarajiwa kuwa mwiba kwa wapinzani kutokana na uwezo wake wa kupandisha mashambulizi.

GkkiP-JWQAAeB_u.jpg

Max Nzengeli

Tayari ameshafunga bao katika mechi za watani wa jadi. Uchezaji wake umekuwa bora sana, na anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji hatari katika mchezo huu.

Gk4QPyaXcAACQ13.jpg

Prince Dube

Hajacheza derby nyingi, lakini ni mchezaji mwenye rekodi nzuri ya kufunga dhidi ya Simba, akiwa amewafunga alipokuwa Azam FC. Anaweza kuleta tofauti katika mchezo huu.

GkuPwNmWEAAbcgm.jpg

Desse Mukwala

Si mchezaji anayeimbwa sana, lakini ana uwezo mkubwa. Kasi yake na pressing zinaweza kuleta kitu tofauti. Katika derby yake ya kwanza hakufunga, lakini alionekana kuwa tishio kubwa.

1741008902356.png

Stephane Aziz Ki

Kipaji kikubwa na mchezaji muhimu wa kuichezesha timu. Uwezo wake wa kupiga mashuti na kutoa pasi za mwisho unamfanya kuwa hatari anapokaribia eneo la 18 la mpinzani.

Gk4etmMXsAAG9XZ.jpg

Charles Ahoua

Si mchezaji anayezungumziwa sana, lakini ni hatari katika mipira iliyokufa. Anaweza kuadhibu wapinzani au kusababisha timu yake kuadhibiwa.

GkkjgFHWAAAc5xp.jpg

Lionel Ateba

Katika derby yake ya kwanza, alikosa nafasi ya wazi ambayo ingeweza kumweka kwenye rekodi ya wafungaji wa mechi za watani wa jadi. Uwezo wake wa kusimama na mabeki zaidi ya wawili unaweza kufungua mianya kwa wachezaji wenzake.

ATEBA-1-1024x819.jpeg
 
Kwa nini inaitwa derby ya Kariakoo wakati kati ya hizo timu mbili, iliyopo Kariakoo ni moja tu? Hili tutalijadili lini?
 
Ongezea kibu kafunga Derby 3 ya juzi kayoko alilikataa goli...
 
Jangwani wala Mchafukoge hazipo Kariakoo

Kumbe wewe mkongwe Dsm!!!
Nimekaa Dsm zaidi ya miaka 20.
Sikuijua kama kuna sehemu inaitwa mchafukoge.

(Nilielekeelzwa na Daktari wa Aghakan ya Morogoro road ilinishangaza sana kusikia kama hiyo sehemu.

Anyway Mchafu Koge ni moja kati ya kata za wilaya ya Ilala
 
Derby ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba ni moja ya mechi kubwa zaidi nchini, ikijaa ushindani ndani ya uwanja na tambo kutoka kwa mashabiki wa timu hizo mbili za mtaa wa Kariakoo.

Hapa ni nyota wa kutazama kwenye derby hii.

Kibu Denis

Tangu ajiunge na Simba, Kibu amekuwa mwiba hasa kwenye mechi za watani wa jadi. Katika derby alizocheza, amefanikiwa kufunga mabao mawili. Katika mchezo wa mwisho, alichezewa faulo nyingi kuliko mchezaji yeyote uwanjani.

Pacome ZouZoua

Mmoja wa wachezaji hatari anapopata nafasi ya kushambulia. Mikimbio yake na uwezo wa kupunguza wachezaji zaidi ya mmoja huleta tishio langoni kwa wapinzani.

Elie Mpanzu

Hii itakuwa derby yake ya kwanza tangu ajiunge na Simba dirisha dogo. Ameonyesha uwezo mkubwa na anatarajiwa kuwa mwiba kwa wapinzani kutokana na uwezo wake wa kupandisha mashambulizi.

Max Nzengeli

Tayari ameshafunga bao katika mechi za watani wa jadi. Uchezaji wake umekuwa bora sana, na anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji hatari katika mchezo huu.

Prince Dube

Hajacheza derby nyingi, lakini ni mchezaji mwenye rekodi nzuri ya kufunga dhidi ya Simba, akiwa amewafunga alipokuwa Azam FC. Anaweza kuleta tofauti katika mchezo huu.

Desse Mukwala

Si mchezaji anayeimbwa sana, lakini ana uwezo mkubwa. Kasi yake na pressing zinaweza kuleta kitu tofauti. Katika derby yake ya kwanza hakufunga, lakini alionekana kuwa tishio kubwa.

Stephane Aziz Ki

Kipaji kikubwa na mchezaji muhimu wa kuichezesha timu. Uwezo wake wa kupiga mashuti na kutoa pasi za mwisho unamfanya kuwa hatari anapokaribia eneo la 18 la mpinzani.

Charles Ahoua

Si mchezaji anayezungumziwa sana, lakini ni hatari katika mipira iliyokufa. Anaweza kuadhibu wapinzani au kusababisha timu yake kuadhibiwa.

Lionel Ateba

Katika derby yake ya kwanza, alikosa nafasi ya wazi ambayo ingeweza kumweka kwenye rekodi ya wafungaji wa mechi za watani wa jadi. Uwezo wake wa kusimama na mabeki zaidi ya wawili unaweza kufungua mianya kwa wachezaji wenzake.

Wanapaswa kuchungwa na nani?
 
Angalau derby hakuna shabiki atakayeenda na matokeo yake! Sio wa Simba Wala Yanga!

Matokeo tutayakuta uwanjani!
3-1 in favour of Yanga. Simba will be first to score through a defender. Aziz Ki will equalize for Yanga. Then Dube will score two goals
 
Umeandika kubalance mzani, hii list ilitakiwa itawaliwe na wachezaji wengi wa Yanga, wa Simba ni only two Kibu kwa mbaali Mpanzu kwa Yanga ni Mzize,Max,Pacome,KI,Chama.
 
Back
Top Bottom