Tetesi: Wachezaji watano wa Simba wasimamishwa kupisha uchunguzi kwa kichapo kikali cha goli 5 kutoka kwa Yanga

Ila Inonga ni kama simuelewi siku hz toka aje huyu Chemalone amekua anacheza kizembe zembe...au macho yangu..

Onyango alikuwa anafunika makosa ya Inonga. Onyango alikuwa anajilipua hata kucheza rafu isiyo na maumivu kutetea makosa ya walinzi wenzake.

Sasa Onyango hayupo Inonga anaonekana makosa yake
 
Badala ya kujifukuza wao viongozi eti wanawafukuza wachezaji ili wanachama wao wasione uzembe wa viongozi wao kwa kusajili hovyo .

Chama alitaka kusawazisha kwa free kick Diarra akafanya save ya maana ikawa kona iliyoleta goli !

Dakika 20 za mwisho wachezaji wa simba walikuwa hoi poor fitness maanake maandalizi yalikuwa duni uwezo wa mwili ulikuwa umefika Kikomo zingeongezwa dakika 30 wangepigwa 5 nyingine jumla ikawa 10!, lakini hapo sio kosa la mchezaji ni kosa la Mwalimu wa viungo.

Kwahiyo mwalimu wa viungo sawa ni halali kufukuzwa.
 
Wacha washupaze shingo umbwa Hawa,Badala ya kujikita kwenye ubora wa scauting Yao Ili kupata usajiri bora.yapo na jazba ya 🖐️yanapaluana.
 
Yanga tulifungwa na Ihefu Kwa makosa ya kocha kupanga timu mbovu lakini tulivumilia. Kwa hiyo Simba isifungwe wao ni Nani ? Kweli madunduka ni shida
 
Moderators waniombe Radhi kwa kufuta Uzi wangu wa Juzi kuwa Inonga, Kapombe, Manula, Chama na Baleke Wameihujumu Simba SC na Kufungwa 5 kwa 1 na Yanga SC
Moderator hawawezi kukuomba radhi wewe . Sema Uongozi wa Simba ndio Ukushukuru kwa kutoa wazo litakalosaidia KUWAAMINISHA MASHABIKI KUWA SIMBA ILIHUJUMIWA.

KIMSINGI SIMBA WAMECHUKUWA JUNGU LAKO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…