Tetesi: Wachezaji watano wa Simba wasimamishwa kupisha uchunguzi kwa kichapo kikali cha goli 5 kutoka kwa Yanga

Tetesi: Wachezaji watano wa Simba wasimamishwa kupisha uchunguzi kwa kichapo kikali cha goli 5 kutoka kwa Yanga


Wachezaji watano wa Simba Sc akiwemo Enock Inonga na Clatous Chota Chama wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yao baada ya kufungwa na Yanga SC mabao 5-1 siku ya Jumapili.

Wachezaji hao wanatuhumiwa kuihujumu timu kitendo kilichopelekea kupoteza kwa idadi kubwa ya mabao.

Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao cha bodi ya Wakurugenzi ya Simba kilichofanyika jana jijini Dar es salaam.

Chanzo cha uhakika kutoka Simba SC kimeiambia Kishamba Media kuwa uongozi umeshapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma dhidi ya wachezaji hao na sasa imeanza uchunguzi wa kina ili kujiridhisha.

Wachezaji hao watakua nje ya kambi ya timu mpaka hapo maamuzi mengine yatakapofanyika.

Chanzo hicho kimesema huwenda leo klabu ya Simba ikatoa taarifa ya wazi kwa Umma juu ya maamuzi waliyofikia kuhusu wachezaji hao au wasitoe ila wahusika wamepewa taarifa.

Maamuzi mengine yaliyofikiwa na bodi ni kufutwa kazi kwa kocha mkuu Robertinho, msaidizi wake pamoja na kocha wa viungo.

Kishamba Updates
Duh..
Things are falling apart..
 
Kama wamesimamishwa kweli na uliowataja ndo wahusika mods wanapaswa kukuomba radhi hadharani na kukupa heshima yako ya kuiinua JF kwa kuleta taarifa kabla ya habari rasmi.
Na kama ipo hivyo, kocha yeye kafukuzwa kwa kosa lipi?
 
Ahmed Ally alisema mkifungwa mjifungie ndani mlieeeeeee weeee...mkitoka nje hasira zimeisha...

Sasa jamaa wamejifungia hotelini baada ya kulia, hasira bado hazijaondoka vifuani mwao...
 
Ila Inonga ni kama simuelewi siku hz toka aje huyu Chemalone amekua anacheza kizembe zembe...au macho yangu..
Inonga kawa hovyo sana siku hizi , hii mechi ya juzi kacheza chini ya kiwango sana...huenda alivuta chake mapema.
 
Kama ni kweli wachezaji wamesimamishwa basi Simba ndio timu yenye viongozi wa vilaza kuliko timu yoyote nchini. No wonder kila mtu anayeujua mpira alishaona na wengi walishataahadharisha hapa kuwa Simba ina tatizo kubwa la kukata moto kuanzia dakika ya 60/65 na ilikuwa ni suala la muda tu kukutana na dhahama kama waliyokutana nayo juzi. Mechi na Al Ahly hapa kama wangekuwa makini Simba alikuwa anakufa 7 kama sio uzembe wa Al Ahly na Mungu kuwa upande wa Simba. Viongozi wa Simba waache kumtafuta mchawi na sababu zisizo na msingi na kuwaonea wachezaji bure kwa uzembe wao wa kutotambua mapems mapungufu ya timu yao na kuyafanyia kazi kwa wakati. K

Kama kweli wana ushahidi usio shaka basi busara ilikuwa kuvipa vyombo vya dola ushahidi huo kwa siri na kuviachia vifanye kazi yake. Hii ingesaidia mbele ya safari iwapo wataonekana hawana hatia. Kwa kitendo cha kuwasimamisha kama ni kweli ikitokea wachezaji wakaonekana hawana hatia je viongozi hawaoni kuwa watakuwa wameharibu morali ya hao wachezaji. Je vipi na wachezaji wengine waliobaki watacheza kwa moyo kweli?
 
Inonga kawa hovyo sana siku hizi , hii mechi ya juzi kacheza chini ya kiwango sana...huenda alivuta chake mapema.
Nadhani anataka amshushe chemalone maana aliona ana jina kumzidi..so analikishq tuu magoli ni bora wangemuweka che malone na kennedy juma mbona huyu Kennedy ni mwamba sana...
 
Rudisha Onyango Mtu kazi weka na Kennedy Juma moto uwake..huyu Inonga ashajichanganya mwenyewe.
 
Hebu tuache uswahili Tanzania!!
1. Chama anayetuhumiwa si ndo amepiga faulo ambayo ilizaa kona na baadae goli la simba?
2. Inonga amefanyaje?
3. Ukitazama magoli yote matano simba wanapokwa mipira/intercepted passes watu wanaenda kufunga

Mzee Rudia tena ile mechi angalia vizuri usoni hasa Manula, Kapombe na Chama utagundua kitu.

Kuna kipindi tuliambiwa Manara anahujumu team hatukuamini. Though lipo tatizo kubwa sana ka kiuongozi hivyo uwajibishwaji usiishie kwa wachezaji tu ila hata ndani ya viongozi kuna virusi wengi.
 
Shida kubwa Simba iko kwa Mangungu, hata huyo Robertinho ni bangusilo tu, wale walioshindwa uchaguzi na Mangungu wataihujumu timu hadi aachie nafasi hiyo, Mangungu ananikumbusha enzi za akina marehemu Juma Salum, kabla ya hapo marehemu Jimmy David Ngonya, kulikuwa ni Vita tu ile ya Israel na Hamas ni cha mtoto.Shahidi ni Kassim Dewji vs Juma Salum.

Mangungu sio mtu wa mpira, watu wa friends of Simba hawampendi na hawako tayari kufanya kazi naye, sasa mm najiuliza mbona wenzetu Yanga wamemuachia timu GSM, hamuoni maendeleo hayo.

Haya mambo ya kijinga kijinga ndani ya timu yetu huwa hayaishi na hayataisha, katika mazingira kama haya mjinga gani atakubali kuweka bilioni 20?
 
Back
Top Bottom