Mwishokambi
JF-Expert Member
- Nov 23, 2020
- 390
- 1,425
Aziz Ki ni mchezaji mzuri sana lakini akipata watu haonekani, ni mchezaji ambaye ukimwekea watu wenye kazi ya kukaba, humuoni, atabaki kulalamika tu kuwa anachezewa rafu.
Wachezaji watatu niliowashuhudia wakihangaika na Aziz Ki na akashindwa kabisa kufurukuta kwao ni kama ifuatavyo.
1. Kevin Nashon kiungo wa Ihefu. Huyu dogo balaa na nitafurahi mno akivaa jezi ya Simba msimu ujao. Anakaba sana, halafu hana masihara hata kidogo, ni moja ya viungo ambao wanacheza kama marehemu Idd Seleman Kibode.
2.Yussuf Kagoma, hii ni mashine nyingine ambayo ina uwezo wa kumzima kabisa Aziz Ki. Nimemshuhudia mara kadhaa akimdhibiti Aziz Ki bila matatizo yoyote. Nitafurahi sana nikimuona akiwa dimbani. Kagoma na Nashon hawapotezi pasi hovyo kama Mzamiru.
3.Yahya Zayd, hii mashine nimeikubali sana. Mashine hii ikisimama pale middle ya chini Simba aisee kila siku ntakuwa sikosi dimbani kumwangalia mnyama.
Hao ndio wanaume wanaoweza kutembea na yule raia wa Burkina Fasso.