ASKOFU AZUNGUMZIA UWEPO WA POLISI UCHAGUZI WA CHADEMA MLIMANI CITY.
Polisi wamejaa Mlimani City kwenye Uchaguzi wa CHADEMA. Lakini ni Polisi hao hao waliojaa Mahakama Kuu wakimzuia Askofu Mwamakula asiingie kusikiliza Kesi ya Ugaidi ya Mbowe. Ni mawakili Peter Kibatala, Jeremiah Mutobesya, Dickson Matata na wengine waliosisitiza kuwa Kesi haitaendelea bila Askofu kuingia. Kelele za wafuasi wa CHADEMA ziliongeza nguvu na Askofu akaingia mahakamani na aliendelea pia kihuhudhuria kila siku ya Kesi.
Ni Polisi hao hao walizuia magari wa BAVICHA mwaka jana yasifike Mbeya kwenye Mkutano wao na ni Polisi hao hao waliowapiga vijana na viongozi wa CHADEMA kule Mbeya wakiwemo Mnyika na Sugu. Pia walinyanyasa wanawake na kuwapiga bila aibu pia wakamuumiza kijana mmoja. Askofu Mwamakula alikuwa miongoni mwa watu waliopazia sauti jambo hili.
Ni Polisi hao hao waliozuia msafara wa Lissu pale Kibamba/Kiluvya Oktoba 2020 na nusura wamtandike kwa risasi Askofu Mwamakula alipoenda kumuona Lissu akuwa amezingirwa. Mungu hakuruhusu hilo litokee. Ni Polisi hao hao waliotuhumiwa kuua baadhi ya Wagombea wa CHADEMA katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na kuwasaidia Wagombea wa CCM watangazwe washindi hata kama pia hawakushinda. Polisi hao hao ambao walipiga mabomu Mbezi Luis kushinikiza mgombea wa CCM atangazwe, tukio lililomliza mtanganzaji wa kike.
Viongozi, wagombea, wajumbe na wanachama na wafuasi wa CHADEMA wawe makini na Nia ya uwepo wa Polisi wakiwa na silaha za moto katika Uchaguzi wao hapo Mlimani City kwani wasiwasi ni tahadhari nzuri. CHADEMA wasije wakafikiri kuwa Polisi, dola, Serikali na CCM wanajali sana usalama wao hao Mlimani City, bali wajue kuwa kuna maslahi yao wanalinda.
Kwa vyovyote vile, Askofu Mwamakula anatoa ushauri huu: Wajumbe wasiwaruhusu kuingia katika sehemu ya kuhesabia kura. Wajumbe wakipiga kura wasiondoke katika ukumbi hadi mshindi ametangazwa. Wanachama wengine wazunguke eneo lote la Mlimani City wakisubiri matokeo. Wasikubali kutishwa na Polisi au pia watu wengine kuwataka waondoke. Hii ni sauti ya Askofu aliyekuwa yuko karibu na CHADEMA wakati wa shida zao, hivyo inawatahadharisha.
Kama hilo Jeshi la Polisi lilishiriki kuwatangaza kwa nguvu wagombea wa CCM wakati ule wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 uwezekano pia upo wa kumtaganza kwa nguvu mgombea wa CHADEMA anayetakiwa na Serikali au CCM! Sisi Askofu tumekwisha kutimiza wajibu wetu wa kuwatahadharisha CHADEMA na umma pia!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 21 Januari 2025; saa 4:25 asubuhi