Wachinjanji wa wanyama, si busara kuchinja mnyama wengine wakiangalia mwenzao akichinjwa

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Nimesikitika sana kuona unyama wanaofanyiwa wanyama na wachinjaji wa Ng'ombe.

Nimeona jamaa wakichinja huku Ng'ombe wengine wakiangalia ajabu kuna Ng'ombe walikuwa wanahalisha na kulia machozi kabisa wengine wakikojoa.

Hakika nimejifunza kitu siku zote nilijua wanyama hawana akili kumbe wanazo na wanajua kabisa hatari iliyoko mbele yao.

Sitaelezea sana ila si ungwana kabisa kuchinja mnyama huku wengine wakiwa kwa foleni wanaangalia Daaah inahudhunisha sana.

Kama huamini nilicho kiona leo nenda machinjioni kwa wazo la kwenda kuwaangalia yaani hofu inatawala na wengine wanapiga uyowe kabisa lakini majamaa hayajari.

Nitaiomba mamlaka yetu hapo machinjioni iweke uzio walau Ng'ombe wengine wasione wenzao wakichinjwa.

Nimesikitika mno
 
Nimesikitimnyama akifanyiwa utu sio sawa Bali afanyiwe unyama maana ndo haki yake
 
Daah, kweli inaonyesha umeumia sana mkuu!
Lakini hujasema ni machinjio ya wapi!
Kimsingi hapo inaonyesha wazi ukiukwaji wa haki za wanyama (animal welfare). Tena inatakiwa uchinjaji ufanyike kibinadamu (humane slaughter) bila kumletea mnyama maumivu.
Haya mambo yote yapo kisheria kabisa (Animal welfare Act).
 
Mkuu sikuwahi Note hiki kitu leo ndo nimeona inahitaji uwe mkatili sana
 
Huu si utu?
Hapana. Huu ni utu.

Labda tuseme 'huu si unyama'.
 
Animal welfare bado tuko nyuma sana kama taifa.
Japo sijajua umeonea katika machinjio gani ila karibia machinjio yote nchini process ya kuchinjwa wanyama inafanyika kikatili sana.
Yaani kuanzia namna wanavyo sombelewa na kubebwa kwenye malori hadi kufika eneo machinjio ni ukatili mtupu.
 
Kabisa mkuu.Jamaa anachinja then anatupa kichwa kando huku wanaona
 
Hata mimi huwa sipendi mnyama apitie mateso.

Kuna hao wachinjaji, wakata miti/wapasua mbao, wachoma mkaa.
Hao watu pamoja na kua hawamuui binadamu ila kuna kanamna roho zao zinakua ngumu kweli, hao kuua mtu sio kazi kwao.

Kila kiumbe kinahisi hatari mkuu, ila ndo hivyo kuongea hawawezi na hawawezi kumzidi maarifa binadamu.
 
Nikweli siku moja ukiona machinjio ya uwazi kama nilivyo sema angalia hao ng'ombe wanavyo angalia utawahurumia.
Mimi kweli wanyama na kuku na chinja ila niliacha kabisa kujika majike ya mbuzi baada ya kuchinja na kukuta kiumbe bado vipo hai tena mapacha aisee nilimua na sikuendelea kabisa.

Hadi leo siwezi chinja jike la mbuzi au ng'ombe siwezi
 
Nimesikitika sana kuona unyama wanaofanyiwa wanyama na wachinjaji wa Ng'ombe.

Nimeona jamaa wakichinja huku Ng'ombe wengine wakiangalia ajabu kuna Ng'ombe walikuwa wanahalisha na kulia machozi kabisa wengine wakikojoa.

Hakika nimejifunza kitu siku zote nilijua wanyama hawana akili kumbe wanazo na wanajua kabisa hatari iliyoko mbele yao.

Sitaelezea sana ila si ungwana kabisa kuchinja mnyama huku wengine wakiwa kwa foleni wanaangalia Daaah inahudhunisha sana.

Kama huamini nilicho kiona leo nenda machinjioni kwa wazo la kwenda kuwaangalia yaani hofu inatawala na wengine wanapiga uyowe kabisa lakini majamaa hayajari.

Nitaiomba mamlaka yetu hapo machinjioni iweke uzio walau Ng'ombe wengine wasione wenzao wakichinjwa.

Nimesikitika mno
Uko sahihi lakini umekosea kitu kimoja tu kusema eti siyo utu! Ng'ombe ana utu gani? Kwa nini wanawachinja bila kuwafanyia stunning? Tulishawazuia sijui kwa nini hawasikii! Kawaida mnyama hatakiwi kuona wenzake wanapochinjwa maana hiyo hali huchangia pakubwa kupoteza quality ya nyama! Ndiyo maana nyama zetu hazipati soko la Ulaya!
 
Wanaoua binadamu je ,? Mtu anapigwa chuma live ? Ama ile mtu anateswa mpaka umauti !

Sembuse ng'ombe? Ambaye maandiko yanaruhusu tuwatumie kama kitoweo ?
 
Daah, kweli inaonyesha umeumia sana mkuu!
Lakini hujasema ni machinjio ya wapi!
Kimsingi hapo inaonyesha wazi ukiukwaji wa haki za wanyama (animal welfare). Tena inatakiwa uchinjaji ufanyike kibinadamu (humane slaughter) bila kumletea mnyama maumivu.
Haya mambo yote yapo kisheria kabisa (Animal welfare Act).
Umchinje bila maumivu? Kama unataka asipate maumivu usimchinje kabisa
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom