Wachinjanji wa wanyama, si busara kuchinja mnyama wengine wakiangalia mwenzao akichinjwa

Wachinjanji wa wanyama, si busara kuchinja mnyama wengine wakiangalia mwenzao akichinjwa

Nimesikitika sana kuona unyama wanaofanyiwa wanyama na wachinjaji wa Ng'ombe.

Nimeona jamaa wakichinja huku Ng'ombe wengine wakiangalia ajabu kuna Ng'ombe walikuwa wanahalisha na kulia machozi kabisa wengine wakikojoa.

Hakika nimejifunza kitu siku zote nilijua wanyama hawana akili kumbe wanazo na wanajua kabisa hatari iliyoko mbele yao.

Sitaelezea sana ila si ungwana kabisa kuchinja mnyama huku wengine wakiwa kwa foleni wanaangalia Daaah inahudhunisha sana.

Kama huamini nilicho kiona leo nenda machinjioni kwa wazo la kwenda kuwaangalia yaani hofu inatawala na wengine wanapiga uyowe kabisa lakini majamaa hayajari.

Nitaiomba mamlaka yetu hapo machinjioni iweke uzio walau Ng'ombe wengine wasione wenzao wakichinjwa.

Nimesikitika mno
Isile nyama ili kuonyesha masikitiko yako
 
Back
Top Bottom