Mbona ni kama kuna kitu hujakiweka wazi mkuu?. Huyo jamaa yako aliyedakwa saa 2 usiku alikuwa ktk. mazingira gani? Katika kuhojiwa kabla ya kuambiwa upo chini ya ulinzi alikuwa anatoa majibu gani kwa maswali ya polisi waliokuja kumkamata?
Watu wengi tuna feli hapa. Tunadhani polisi aliyekuja kukamata ni Adui na huenda ana maslahi binafsi dhidi yako. La Hasha. Sivyo kabisa. Yupo kazini.
1. Tukumbuke unapokamatwa kwa kuhisiwa umetenda kosa ; wewe unaitwa ni Mtuhumiwa tuu. Haijathibitika kwamba wewe umefanya kosa. Hata ukiwekwa rumande/lock-up bado wewe ni Mtuhumiwa.
2. Tukumbuke na Tuzingatie kwamba Polisi anayekuja kukukamata yupo kikazi zaidi na hajaja kwako kupiga story. Ukimpa ushirikiano i.e. usimsumbue na kuifanya kazi hiyo kuwa ni ngumu kwake bila sababu za msingi.
3. Unapokuwa Kituo cha polisi kama Mtuhumia, kumbuka upo tayari chini ya ulinzi. Jitahidi kufanya/kutii kile polisi anachokuamuru ufanye. Kuonesha Ukaidi, Ujeuri au Kujitetea ndo hapo utafunguliwa vikombe. Zingatia kwamba yale yooote yote watakayokuamuru cjui andika hapa, weka saini hapa n.k. n.k; Usiogope fanya tu - Ukifika Mahakamani unaweza na uko Huru kuyakana/kuyakataa yote na ngoma inaanza upya mbele ya Mahakama (Hakimu).
BTW: Mm sio Polisi wala Mwanasheria - I stand to be corrected.