Wachokonozi: Polisi wanakuja kukukamata wanasema, "Tumeagizwa"; ukiuliza kosa, wanajibu, "Utajulia mbele

Nawao wanajua sio lazima kukubali kusaini kila wanachosema..ikiwa watanipiga kilazima sawa..ila wahakikishe sitoki nje😁😁😁
Hawaawezi kukupiga ivi-vi; just like that hapana. Lazima pawe na pa kuanzia. Kumbuka hata wao kama binadamu wanalijua hilo na wanachukua tahadhari pia. Wanatafutaga kijisababu fulani ivi ndo kinakuwa kisa na wanakupiga.
 
Bora ukutane na majambazi usiku kuliko kukutana na policcm.....jambazi anaweza kukuchukulia mali zako alafu akakuacha salama.....
 
Hawaawezi kukupiga ivi-vi; just like that hapana. Lazima pawe na pa kuanzia. Kumbuka hata wao kama binadamu wanalijua hilo na wanachukua tahadhari pia. Wanatafutaga kijisababu fulani ivi ndo kinakuwa kisa na wanakupiga.
Hivi unawajua hawa hayawani wa kuitwa polisi
 
Nawajua, na baadhi yao ni marafiki zangu. Usitumie msemo ule kwamba samaki mmoja kwenye tenga akioza, wameoza wote.
Nina uzoefu wa matukio dhidi ya hawa majangiri nadiriki kusema polisi wa Tanzania wa vinasaba na shetani
 
Mimi nawashangaa wananchi wanavyoidai katiba mpya wakati sheria zilizopo zinavunjwa tu pasipo kuwa na hatua wala adhabu za kuchukuliwa
 
Nina uzoefu wa matukio dhidi ya hawa majangiri nadiriki kusema polisi wa Tanzania wa vinasaba na shetani
Kha! Mkuu, Umeenda mbali mno jamaa yangu. Hivi hakuna jema/zuri hata moja ulilowahi kupokea kutoka kwa polisi Tanzania? au ndugu/jamaa/rafiki yako aliyewahi kutendewa jema na polisi Tz?
 
Kha! Mkuu, Umeenda mbali mno jamaa yangu. Hivi hakuna jema/zuri hata moja ulilowahi kupokea kutoka kwa polisi Tanzania? au ndugu/jamaa/rafiki yako aliyewahi kutendewa jema na polisi Tz?
Kuna matukio kama 8 Niliwahi kutendewa na hawa hayawani mpaka leo hii nikimuona polisi nahisi kifo kiko mbele yangu niliteswa yaani sijui nikuelezee vipi unielewe kosa lenyewe sasa basi tu
 
Hawaawezi kukupiga ivi-vi; just like that hapana. Lazima pawe na pa kuanzia. Kumbuka hata wao kama binadamu wanalijua hilo na wanachukua tahadhari pia. Wanatafutaga kijisababu fulani ivi ndo kinakuwa kisa na wanakupiga.
Yani wanakuseti kwenye mfumoπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kuna matukio kama 8 Niliwahi kutendewa na hawa hayawani mpaka leo hii nikimuona polisi nahisi kifo kiko mbele yangu niliteswa yaani sijui nikuelezee vipi unielewe kosa lenyewe sasa basi tu
OK. usiwabebe moyoni kiasi hicho. Waliokutendea pengine sio hao unaokutana nao They are innocent. Samehe na uwaachilie. Anza ukurasa mpya dhidi ya Polisi Tz.
 
OK. usiwabebe moyoni kiasi hicho. Waliokutendea pengine sio hao unaokutana nao They are innocent. Samehe na uwaachilie. Anza ukurasa mpya dhidi ya Polisi Tz.
Na kwa yaliyotokea mo29 ndiyo kabisa imani na mtu wa kuitwa polisi wa Tanzania haipo mpaka nalala mauti
 
Hao jamaa wana akili sana , akili hizo ni tishio kwa vilaza waliokuwa wamejipachika madarakani.

Hawa jamaa nakumbuka clip ile walivamiwa kama majambazi waliokuwa wakifuatiliwa kwa muda mrefu.
 
Yani wanakuseti kwenye mfumoπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Yeah. Kwa mfano wanaweza kukuuliza swali lile-lile zaidi ya mara nne(4) na kiuhalisia lazima utakereka na huenda ukajibu kwa hasira 'mbona nimeshasema lakini mnajirudia-rudia shida nnini" Hapo tayari wamepata kijisababu na utasikia "eh, we unatujibu jeuri?" kazi inaanza.
 
Simbachawene akiwa waziri wa mambo ya ndani alijaribu kutoa mwelekeo mzuri sana wa utendaji bora wa jeshi la polisi ambao ungerejesha mahusiano na imani ya wananchi kwa jesho lao.

Hata hivyo, Mh. Simbachawene hakudumu katika hiyo nafasi kushuhudia ndoto yake ikitimia, badala yake uteuzi wake ulitenguliwa. Itoshe tu kusema mamlaka za uteuzi huwa haziingiliwi katika maamuzi yake.
 
Na kwa yaliyotokea mo29 ndiyo kabisa imani na mtu wa kuitwa polisi wa Tanzania haipo mpaka nalala mauti
Hilo la mo29 lina makando-kando na mauza-uza mengi. Wapo wanaodai ni watu waliokodiwa(Mercenaries), wengine wanasema ni askari kutoka Uganda/Malawi na wengine ni askari wa Jw ilhali wengine wanasema ni Polisi wetu....... yan haieleweki na ukizingatia magwanda /uniforms za polisi mtu anaweza kujishonea na akavaa kutekeleza lengo ovu.
 
Police hawatakiwi kukamata watu kwa kuhisi wamefanya kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…