Wachungaji hadi lini mtavunja ndoa za watu?

Wachungaji hadi lini mtavunja ndoa za watu?

Wachungaji nao ni watu, wana hisia na zikizidi sana wanapeleka moto kama kawaida...
 
Joseph Moses ambaye ni dereva bodaboda mkazi wa Mbeya anakabiliwa na shtaka la kumtishia kumuua kwa maneno mkewe Irene Mwaikana huku chanzo cha ugomvi huo ni tabia ya mkewe ya kutoa chakula nyumbani na kupeleka kwa mchungaji.

“Mheshimiwa hakimu huyu mwanamke anakera sana, tukichinja kuku, vipaja na vidari vyote anapelekewa mchungaji, alafu mimi ninayetafuta pesa kwa shida napewa vipapatio, Nahisi anatoka naye kimapenzi, kwanza mchungaji hana mke." –Mtuhumiwa Joseph Moses.

Sasa ninachojiuliza kwanini wachungaji wanafanya mazoea na wake za watu? Mchungaji Mmoja wa dhehebu fulani aliambulia kipigo kwa kumtongoza mke wa muumini wake....
Haya mambo hadi lini??View attachment 2332082
Wameshaambiwa "iweni Kama mimi, lakini Kama mkishindwa basi oeni".
Hawa ndiyo wanaifanya injili iwe ngumu kuihubiri kwa sababu ya matendo kama haya. Atawezaje kukemea uzinzi wazi wazi?
 
Utaambiwa Wewe pepo, hawa manabii was kusema leteni kucha na nywele wameshakuwa waganga wa kienyeji
Ni waganga wanaotapeli masikini kupitia jina la Yesu.Kucha na nywele zinawakilishwa kuzimu Ili kuchukua baraka zako na kukufanya msukule we kazi yako ni kuwapelekea pesa .
 
Kwani Mheshimiwa mchungaji anazungumziaje hili suala la kula firigisi za mume mtafutaji?
 
Joseph Moses ambaye ni dereva bodaboda mkazi wa Mbeya anakabiliwa na shtaka la kumtishia kumuua kwa maneno mkewe Irene Mwaikana huku chanzo cha ugomvi huo ni tabia ya mkewe ya kutoa chakula nyumbani na kupeleka kwa mchungaji.

“Mheshimiwa hakimu huyu mwanamke anakera sana, tukichinja kuku, vipaja na vidari vyote anapelekewa mchungaji, alafu mimi ninayetafuta pesa kwa shida napewa vipapatio, Nahisi anatoka naye kimapenzi, kwanza mchungaji hana mke." –Mtuhumiwa Joseph Moses.

Sasa ninachojiuliza kwanini wachungaji wanafanya mazoea na wake za watu? Mchungaji Mmoja wa dhehebu fulani aliambulia kipigo kwa kumtongoza mke wa muumini wake....
Haya mambo hadi lini??View attachment 2332082

Jamaa yuko sahihi kulalamika ila njia aliyotumia kulalamika itamletea shida.

Alichotakiwa kufanya ni kumfata mchungaji tena aende na mkewe mchana jua kali amuonye mchungaji kuacha mazoea na mkewe bila vitisho bila lolote baya. Amchane black and white then akirudi home amchane mkewe
 
Ila hapo mjinga ni mke wala sio mchungaji! Biblia inasema, asiyewajali watu wa nyumbani mwake huyo ni mbaya kuliko asiye amini. Shida watu hawasomi Neno wanataka tu kusikia yale mchungaji anasema!
 
Mtaani kwetu... Jamaa Muislam kagombana na mkewe.

Wakawa wanaenda Kwa Sheikh kusuluhisha

Sheikh akawa anamwambia Jamaa .achana na huyo mwanamke, harakisha sana kuvunja Ndoa

Jamaa akatoa Talaka zake zote 3.

Sheikh akamzunguka jamaa, akamuoa Mke wa Jamaa Sasa Sheikh ana wake wawili
Kuna mke wa Rafika angu amezoeana sana na shekhe mmoja hivi umwambii kitu kuhusu huyo shekhe ,Amejenga hadi Urafiki kwa.familia ya shekhe.
 
Tamaa ya Wanawake na pesa ndo anguko la wachungaji wengi. Shetani uleta wanawake warembo makanisani Ili wawangushe wachungaji.
Kumbe wanawake warembo ni washetani eehh so wabaya ndo wa yesu?
 
Back
Top Bottom