Wachungaji hadi lini mtavunja ndoa za watu?

Mambo kama haya nao wanawake wanaangalia na mwanaume wa kumfanyia hivyo vituko..

Kiufupi kama mwanamke uliyeoa ni Majanga haya ndio matokeo yake kwa sababu haiwezekani vituko hivi vitokee,na mwanamke aliamua kumrekodi na kumshitaki..
 
Kuna mmoja walikuwa wanapeana zamu ya kumpikia na kumsubiria ale ndio waoshe vyombo.Mwanamke wa zamu yake ikifika anaacha genge lake mpaka saa tatu usiku ndio arudi akalale.
Ndio nasema hivi huwa wanaangalia na mwanaume wa kumfanyia vituko,mimi nakutimua mapema kabisa Bora nikae bila mke.
 
Sasa ninachojiuliza kwanini wachungaji wanafanya mazoea na wake za watu? Mchungaji Mmoja wa dhehebu fulani aliambulia kipigo kwa kumtongoza mke wa muumini wake....
Sasa kuna mchungaji hapo? Kwa hiyo hata sangoma akiamua kufungua kijiwe akawa anadai michanga tya miguu waliyokanyaga adui zako, anazini na wake na mabinti za watu au anakusanya kucha bado atakuwa mchungaji kwa kuwa anavaa kola au joho?

Haya hayatakwisha mpaka watu watakapoanza kumheshimu Mungu na Neno lake. Haiwezekani Neno linamwita tapeli ila wewe bila soni unamwita mchungaji!

Dharau kwa Mungu zina gharama!
 
Bora huyo kashtakiwa kwa kutishia kuua, Mi ningekuwa jela kwa kesi ya Mauaji.
 
Ogopa sana wachungaji ambao hawapo chini ya taasisi.. wao pia ni binadamu Tamaa zao za mwili hata wakikosea hakuna wakuwakosoa kwenye uongozi wao..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…