Wachungaji kutaka fungu la kumi kwa lazima

Huo ni utumwa wa hadharani.
Nguruwe amekatazwa agano la kale lakini analiwa tu huku tukisema ni old testament commit.
Zaka iliagizwa kwenye agano la kale lakini mnalazimishwa mpaka sasa na hamshituki kuwa ni maagizo yaliyopitwa na wakati.
Alafu kuna Jamaa anakwambia yeye hajui kuhusu Agano la Kale

ROBERT HERIEL pitia na hapa
 
Hivi huyo mchungaji anajua garama za dialysis Bugado? Anajua kwa wiki mnatakiwa kumpeleka mama mara ngapi?

Kuna watu wanajua kukera. Hapo alitaka hela ya kula.mwaya njoo romani, sisi tuna michango ila hatulazimishi, hutoona padre akikutumia sms ya hivyo.

Mbona kwenye hiyo sms hajauliza hali ya mgonjwa? Au anataka kukutishia usipotoa zaka mungu atamchukua mama? Aisee huyo mtummishi kanikera nimewaza ningekuwa mimi ningemjibu vip dah.
 
Pole sana ndugu,ukweli uko hivi! Sadaka na zaka ni muhimu sana kutoa,ila usitoe kwa kumhofia mchungaji wako,toa kwa hofu ya Mungu tu,kinyume na hapo hiyo sadaka yako na zaka haitakuletea matokeo chanya ,kuhusu huyo mchungaji wako we mpuuze na usijitetee sana kwake,piga kimya,
 
Tatizo ni wewe kucheka cheka na hao wachungaji, wewe amini Mungu wako, nenda kanisani kama kawaida na sadaka unayotoa ibakie kuwa ni siri yako na Mungu, kamwe mtu asijue umetoa kiasi gani na umeitolea wapi (sio lazima utoe hapo kanisani kwako, unaweza kutoa sadaka popote).

Mwisho kabisa kaa kimya, usimjibu chochote huyo pastor wako. Akiendelea kukufuata fuata kuhusu pesa zako, mwambie kwa heshima aachane kabisa kufuatilia pesa zako.
 
Wakati mwingine unaweza ukaamua kuwa unakwenda kanisani lakini usitoe sadaka kabisa, yaani hata senti tano usitoe. Mchungaji wako akiuliza vipi, mwambie utoaji wako wa sadaka ni siri yako na Mungu. Kama hakutaki basi akufukuze, na ukifukuzwa usiondoke hapo!
 
Jamani zindukeni basi

UISLAMU ndio dini ya kweli jamani
ivi kila imamu angekua anadai iyo 10% kwa waumini wake si wangekua washatajirika zamani sanaaa
ila mkiambiwa kuhusu Uislamu mnakataa
hya sasa endeleeni kuliwa pesa zenu na wajanja wa mjini

AM PROUD TO BE MUSLIM
 
Utazoeanaje na mchungaji mpk mnatumiana msg km mnatongozana.
Matokeo ndo hayo.
 
Mchungaji yupo sahihi ki biblia.
Japo ki ubinadamu hajatumia Hekima.

Zaka ni muhimu kwa Kila muumini wa Yesu Kristo.
Sadaka ni muhimu

Lakini matoleo.mengineyo ni Hiyari na Utashi wa mtu
 
Makanisa ya watu binafsi sanasana kuna hiyo michezo ya kufuatiliana japo huyo amezidi..sadaka hailazimishwi .. mtu anapaswa ahiari kutoa toka moyoni mwake.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Hapo hakuna “Mchungaji”. Angekuwa ni Mchungaji sahihi angekuja hospital kumfanyia maombi mzazi wako

Hama kanisa hilo haraka kama hupendi kukwazika. Otherwise komaa hapo na uendelee kutoa matoleo kadri Mungu anavyokujaria na sio kwa shinikizo la mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…