Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Una uhakika ni huyo pasta uchwara kambariki au ni hustling zake mwenyew?KAma kakubariki umenunua kagari why usitoe 10%
Achana na mambo ya dini ni mambo ya kitapeli. Mungu hayupo.
Zaka na sadaka ni agano la mtu na Mungu. Hujui mtu kaongea vipi na Mungu wake so usije ukamlazimisha kitu. Kuna wakati watu wanamkopa Mungu kwa kumuomba kabisa au wanaomba wasamehewe kutokana na wanachopitia. Mungu akimjibu mtu hitaji lake wala padri au mchungaji hautajua unless upo kwenye mchakato huo na Roho Mtakatifu. Acheni kuingilia personal relationship kati ya mtu na Mungu. Wewe fundisha halafu usubirie.Mchungaji yupo sahihi ki biblia.
Japo ki ubinadamu hajatumia Hekima.
Zaka ni muhimu kwa Kila muumini wa Yesu Kristo.
Sadaka ni muhimu
Lakini matoleo.mengineyo ni Hiyari na Utashi wa mtu
Mafundisho ya wapi hayo?Zaka na sadaka ni agano la mtu na Mungu. Hujui mtu kaongea vipi na Mungu wake so usije ukamlazimisha kitu. Kuna wakati watu wanamkopa Mungu kwa kumuomba kabisa au wanaomba wasamehewe kutokana na wanachopitia. Mungu akimjibu mtu hitaji lake wala padri au mchungaji hautajua unless upo kwenye mchakato huo na Roho Mtakatifu. Acheni kuingilia personal relationship kati ya mtu na Mungu. Wewe fundisha halafu usubirie.
Nyie si ndiyo huwa hamziki mtu akifariki asipofanya hayo au unamtania mwenzio nyie ni zaidi ya huyo mchungajiHamia Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume uje ufaidi mema yote ya huu ulimwengu! Huku kwetu hakuna mambo ya kufuatana! Paroko yuko zake busy huko Parokiani!
Uende Kanisani, usiende! Hakuna anayejali! Umetoa zaka, hujatoa! Hakuna atakaye kusumbua! Watu wanamwagilia moyo kwa kipimo! Maana hata Mapadre wenyewe wanamwagilia sana tu!
Hakika ukiwa muumini wa RC migogoro utaisikia kwa majirani tu!
Kristu....!
Tumsifu Yesu Kristu.....!!
Kanisa la Kisinodiii....!
Mpaka itokee hivyo, maana yake wewe hujawahi kabisa kukanyaga Kanisani! Hujawahi kutambulika kwenye Jumuiya yoyote! Una mitala ya waziwazi!Nyie si ndiyo huwa hamziki mtu akifariki asipofanya hayo au unamtania mwenzio nyie ni zaidi ya huyo mchungaji
Kwani wewe ni mke wake mungu hadi uje kumtetea hapa?Ona huyu.
Wewe baba yako alikula ugali maharage akamtafuta mama yako wakajamiiana wakatoa manii ambayo ni ugali maharage ukatoka wewe Leo unasema MUNGU HAYUPO.
Braza kutoa ni wewe na Mungu wako. Haimhusu mchungaji wala kanisa. Mahusiano yako personl na Mungu yanaamua ufanyeje na uchumi wako. Wewe kama unatoa kama ng’ombe utaendelea kutajirisha wachungaji bila kuona matokeo. Sijawahi mpa mchungaji zaka au sadaka toka nijue natakiwa niongee nae kwanza. Nisipokua nayo namwambia namuomba na amani yake ipotayo amani zote inanipa imani amenisikia. Pole unayepelekeshwa.Mafundisho ya wapi hayo?
tatizo la kwenda kwenye makanisa yanayomilikiwa na mtu binafsi.Et kanisa linaitwa la mtu fulani naumia sana.Wakuu habarini
Mimi ni muumini wa kanisa la mahali pamoja ambalo ni T.A.G(X)
Jana nimepokea ujumbe wa kunikwaza kunifedhehesha na kunifanya nione kama natwaga maji kwenye kitu
Jana mchungaji kanitumia msg akiniuliza mbona sijahudhuria jana kanisani? Au na mpango wa kuhama kanisa !!
Nami 'nikamjibu kwa kumpigia simu nikamwambia mbona nilikuandikia msg kuwa nadharula sitahudhuria ibadani hukuupata ujumbe na nilimtumia pia na mzee nikakata simu nikascreen short msg nikamtumia whatsap
Akanijibu kuwa dharula zipo ila kama ni siku ya ibaada utume sadaka na michango , ni muhimu sana nikaa kimya
Leo Asubuhi nimeamka asubuhi nikiwa na ratiba ya kutoka kumpeleka mama yangu mzazi cliniki ya dialysis Bugado wakati natoa kausafiri kwenye chasis number alikuwa anapita tukasalimiana na kumwambia tunaelekea Hospital akasema sawa na hongera nyingi za kunua kausafiri kapya.
Imefika saa nne nipo hospitali naona Msg tena
akiniandikia ujumbe unasomeka hivi"
Leo ni mwisho wa mwezi na jana haukuwepo ibadani Tuma sasa hivi FUNGU LAKO LA KUMI UTUME NA HELA YA KUTOLEA KANISA LINA MADENI MENGI ""
Nikausoma nikatulia nakuvuta pumzi nikamtumia msg KUWA KWA SASA SINA PESA, FEDHA NINAYOBAKIA NAYO NI KWA AJILI YA MATUMIZI MUHIMU YA FAMILIA NAJUA PIA ZAKA UMUHIMU WAKE, nikikaa sawa nitatoa wala haina shida
Akajibu tena wewe unabadili tu magari kwa habari ya zaka hutaki kutoa nikamwambia kwani zaka ni lazima lini sijatoa zaka zaidi ya mwezi huu nimepata msiba, na unanihusu kwa sehemu kubwa sina fedha na ninauguliwa wewe mwenyewe shahidi hali ya mzazi wangu Muda wote gari inapaswa kuwa na mafuta, muda wowote hali inabadilika tukawa tumeachana hivyo
Sasa hebu mnisaidie huu utaratibu unatoka wapi kwanini sadaka na zaka ni lazima au ni vile mtu anavyoguswa kulingana na Vile anavyopata! Maana Mungu anasema nijaribu sasa huku Naona mchungaji anatumia command utadhani kanipa yeye kisa anamadeni.
Hebu nipeni njia itakayoniondoa kanisa mikwaruzo na Mchungaji