Wachungaji kutaka fungu la kumi kwa lazima

Wachungaji kutaka fungu la kumi kwa lazima

mi kuna kipindi nilikuwa kkkt dar usharika wa kongowe mmh,wanalazimisha hiyo fungu la kumi hatari,walianza program ya kujua mshahara wa kila mmoja aloajiri nikasema hali ni tete,alafu sasa mpaka wanaleta mtu atayehubiri mambo ya sadaka jumapili wanaleta muhubiri atayeubiri mambo ya kutoa sadaka
Haaahaaahaaa kanisa gani hilo

Makanisa yamechachamaaa
 
Wakuu habarini

Mimi ni muumini wa kanisa la mahali pamoja ambalo ni T.A.G(X)

Jana nimepokea ujumbe wa kunikwaza kunifedhehesha na kunifanya nione kama natwaga maji kwenye kitu

Jana mchungaji kanitumia msg akiniuliza mbona sijahudhuria jana kanisani? Au na mpango wa kuhama kanisa !!

Nami 'nikamjibu kwa kumpigia simu nikamwambia mbona nilikuandikia msg kuwa nadharula sitahudhuria ibadani hukuupata ujumbe na nilimtumia pia na mzee nikakata simu nikascreen short msg nikamtumia whatsap

Akanijibu kuwa dharula zipo ila kama ni siku ya ibaada utume sadaka na michango , ni muhimu sana nikaa kimya

Leo Asubuhi nimeamka asubuhi nikiwa na ratiba ya kutoka kumpeleka mama yangu mzazi cliniki ya dialysis Bugado wakati natoa kausafiri kwenye chasis number alikuwa anapita tukasalimiana na kumwambia tunaelekea Hospital akasema sawa na hongera nyingi za kunua kausafiri kapya.

Imefika saa nne nipo hospitali naona Msg tena
akiniandikia ujumbe unasomeka hivi"

Leo ni mwisho wa mwezi na jana haukuwepo ibadani Tuma sasa hivi FUNGU LAKO LA KUMI UTUME NA HELA YA KUTOLEA KANISA LINA MADENI MENGI ""

Nikausoma nikatulia nakuvuta pumzi nikamtumia msg KUWA KWA SASA SINA PESA, FEDHA NINAYOBAKIA NAYO NI KWA AJILI YA MATUMIZI MUHIMU YA FAMILIA NAJUA PIA ZAKA UMUHIMU WAKE, nikikaa sawa nitatoa wala haina shida

Akajibu tena wewe unabadili tu magari kwa habari ya zaka hutaki kutoa nikamwambia kwani zaka ni lazima lini sijatoa zaka zaidi ya mwezi huu nimepata msiba, na unanihusu kwa sehemu kubwa sina fedha na ninauguliwa wewe mwenyewe shahidi hali ya mzazi wangu Muda wote gari inapaswa kuwa na mafuta, muda wowote hali inabadilika tukawa tumeachana hivyo

Sasa hebu mnisaidie huu utaratibu unatoka wapi kwanini sadaka na zaka ni lazima au ni vile mtu anavyoguswa kulingana na Vile anavyopata! Maana Mungu anasema nijaribu sasa huku Naona mchungaji anatumia command utadhani kanipa yeye kisa anamadeni.

Hebu nipeni njia itakayoniondoa kanisa mikwaruzo na Mchungaji

Una miliki biblia? Wewe ni mkristo? Una roho mtakatifu? Unafuata nini jamii forum na haya maswali?

1. Mchungaji wako ni mwehu.
2. Na wewe ni mshirika wa mwehu.
 
Una miliki biblia? Wewe ni mkristo? Una roho mtakatifu? Unafuata nini jamii forum na haya maswali?

1. Mchungaji wako ni mwehu.
2. Na wewe ni mshirika wa mwehu.
Hahaha kwa hiyo tumekutana machiz watatu na ww mchangia mada
 
Kudai fungu la 10 kwa stahili hiyo SIO SAWA na haikubaliki,
Kama wameelemewa na madeni hiyo haikuhusu ,
Kanisa linaelemewaje na madeni? Hiko ni kipimo kuwa hawafanyi kazi zao vizuri na hawakai kwenye nafasi zao sawasawa.
Hayo madeni yao yasije yakawanyima kupokea baraka.
Mwisho, namalizia na wale wale wanaopinga fungu la 10, kwa sisi waamini fungu la 10 ni la Mungu na ukila umekula pesa ya Mungu. Katika 100,000 fungu la Kumi ni 10,000 ni ndogo na haikutii UMASKINI. Katika vitu nazingatia ni fungu la Kumi.
Dada zetu wa kinyakyusa hawa wachungaji wanawapiga sana pesa
 
Shida ya madhehebu ya kiroho ni Mchungaji akishakuona una uwezo fulani,Labda una ajira,mfanya biashara,nk,basii!
Na kwa taarifa yako hata ungekimbilia dhehebu gani la kiroho!
Hata hivyo unachotakiwa usiache kulipa Zaka kwa kadiri ya kufanikiwa kwako!
 
Jamani zindukeni basi

UISLAMU ndio dini ya kweli jamani
ivi kila imamu angekua anadai iyo 10% kwa waumini wake si wangekua washatajirika zamani sanaaa
ila mkiambiwa kuhusu Uislamu mnakataa
hya sasa endeleeni kuliwa pesa zenu na wajanja wa mjini

AM PROUD TO BE MUSLIM

Mkuu kwahyo sababu ya sadaka watu ndo wahame ukristo mengine hayahesabiki?sadaka ni hiyari period.
 
Kwanza pole ila kutaka ushauri Kwa watu ambao hawajaokoka sidhani kama ni sahihi biblia inasema mambo ya rohoni yanatambulika Kwa jinsi ya rohoni Wala mtu wa mwlilini hayatambui turudi kwenye mada ktk Malaki 3;8-10 neno linasema lete sio hiyari zaka sio utoaji hiyo ni Kodi ya Mungu tena ansema iwe kamili Kwa maswali zaidi tuwasiliane 0714134004
Hiyo Malaki uliyonukuu na unayotumia kutoa Zaka, Unafahamu ya kwamba Nabii Malaki hapo alikuwa anazungumzia Zaka iliyo Katika Torati?

Unafahamu kwamba Malaki 3:10 inazungumzia Zaka kwa mujibu wa Torati?
 
Hivi huyo mchungaji anajua garama za dialysis Bugado? Anajua kwa wiki mnatakiwa kumpeleka mama mara ngapi?

Kuna watu wanajua kukera. Hapo alitaka hela ya kula.mwaya njoo romani, sisi tuna michango ila hatulazimishi, hutoona padre akikutumia sms ya hivyo.

Mbona kwenye hiyo sms hajauliza hali ya mgonjwa? Au anataka kukutishia usipotoa zaka mungu atamchukua mama? Aisee huyo mtummishi kanikera nimewaza ningekuwa mimi ningemjibu vip dah.
Roman hakuna michango kasema nani? Michango ya ujenzi wa kanisa, zaka, ujenzi wa shule(hapa hata ukiwa mkatoliki hakuna favour yoyote utayopata ukimpeleka mtoto shule hio husika) ujenzi nyumba za mapadri...hapo bila kusahau kama kwenye pc hawaoni michangi yako haupewi huduma yoyote ya kikanisa...michango ipo kila sehemu...😀😀😀😀
 
Wakuu habarini

Mimi ni muumini wa kanisa la mahali pamoja ambalo ni T.A.G(X)

Jana nimepokea ujumbe wa kunikwaza kunifedhehesha na kunifanya nione kama natwaga maji kwenye kitu

Jana mchungaji kanitumia msg akiniuliza mbona sijahudhuria jana kanisani? Au na mpango wa kuhama kanisa !!

Nami 'nikamjibu kwa kumpigia simu nikamwambia mbona nilikuandikia msg kuwa nadharula sitahudhuria ibadani hukuupata ujumbe na nilimtumia pia na mzee nikakata simu nikascreen short msg nikamtumia whatsap

Akanijibu kuwa dharula zipo ila kama ni siku ya ibaada utume sadaka na michango , ni muhimu sana nikaa kimya

Leo Asubuhi nimeamka asubuhi nikiwa na ratiba ya kutoka kumpeleka mama yangu mzazi cliniki ya dialysis Bugado wakati natoa kausafiri kwenye chasis number alikuwa anapita tukasalimiana na kumwambia tunaelekea Hospital akasema sawa na hongera nyingi za kunua kausafiri kapya.

Imefika saa nne nipo hospitali naona Msg tena
akiniandikia ujumbe unasomeka hivi"

Leo ni mwisho wa mwezi na jana haukuwepo ibadani Tuma sasa hivi FUNGU LAKO LA KUMI UTUME NA HELA YA KUTOLEA KANISA LINA MADENI MENGI ""

Nikausoma nikatulia nakuvuta pumzi nikamtumia msg KUWA KWA SASA SINA PESA, FEDHA NINAYOBAKIA NAYO NI KWA AJILI YA MATUMIZI MUHIMU YA FAMILIA NAJUA PIA ZAKA UMUHIMU WAKE, nikikaa sawa nitatoa wala haina shida

Akajibu tena wewe unabadili tu magari kwa habari ya zaka hutaki kutoa nikamwambia kwani zaka ni lazima lini sijatoa zaka zaidi ya mwezi huu nimepata msiba, na unanihusu kwa sehemu kubwa sina fedha na ninauguliwa wewe mwenyewe shahidi hali ya mzazi wangu Muda wote gari inapaswa kuwa na mafuta, muda wowote hali inabadilika tukawa tumeachana hivyo

Sasa hebu mnisaidie huu utaratibu unatoka wapi kwanini sadaka na zaka ni lazima au ni vile mtu anavyoguswa kulingana na Vile anavyopata! Maana Mungu anasema nijaribu sasa huku Naona mchungaji anatumia command utadhani kanipa yeye kisa anamadeni.

Hebu nipeni njia itakayoniondoa kanisa mikwaruzo na Mchungaji
Kwahiyo zaka mnawapelekea wachungaji kumbe??! Si kwamba zinapelekwa kwa masikini hili kupunguza gape la mafukara katika Nchi au mji!

Dah, aisee poleni
 
Roman hakuna michango kasema nani? Michango ya ujenzi wa kanisa, zaka, ujenzi wa shule(hapa hata ukiwa mkatoliki hakuna favour yoyote utayopata ukimpeleka mtoto shule hio husika) ujenzi nyumba za mapadri...hapo bila kusahau kama kwenye pc hawaoni michangi yako haupewi huduma yoyote ya kikanisa...michango ipo kila sehemu...😀😀😀😀
Michango ipo tena mingi sana romani ila hulazimishwi. Hapa kuna bahasha kibao sijapeleka hiyo michango ila sijakumbushwa hata siku moja.
Zaka sijatoa miezi kadhaa hakuna wa kunilazimisha kutoa, nitatoa mwezi nitakao taka nifidie na miezi ya nyuma, na hata nisipofidia hakuna hata wa kuniuliza.
Kuhusu kutoa huduma hilo romani kama hutowi michango huwezi pewa huduma ila hulazimishwi na mtu yeyote. Shida zako zikikipeleka ndo aatakwambia michango yao uamue kutoa au kutotoa.

Michango ya romani hainipi shida, natoa kama ninayo nikifa lazima nizikwe haijarishi wataniombea au la! Ila kuzikwa lazima nizikwe
Hizo huduma nyingine nikizitaka nitalipa wakati huo silazimishwi kuzilipia wakati sijazihitaji.
 
Upo parokia gani mbona Roman nako kumechangamka kwa michango siku hizi?
Hakuna kanisa lenye michango duniani kuliko romani, ila hulazimishi hutooana ukipigiwa simu kama mleta mada sijui peleka zaka.shida zako zikikupeleka na utaulizwa michango yao.
 
Back
Top Bottom