Wachungaji kutaka fungu la kumi kwa lazima

Mambo ya dini ni biashara kama zilivyo biashara nyingine, ingawa serikali inasita kuihalalisha na kuihalalisha kamari! Anafanya kazi kanisani, atakula kanisani! Hili halipingiki, mapadri,maaskofu,masister hayo ndiyo malipo yao halali kwa huduma wanayotoa kueneza maadili mema kwa jamii kupitia injili,bila hao watu tungekuwa kizazi cha ajabu mno!, Ya kaisari mpe kaisari kutimiza maandiko yanavyotaka. Ili itakapowadia ile siku itarajiwayo, isijekutokea yale, mara ngapi nimekukusanya, kama vile vifaranga vya kuku chini ya mabawa lakini ukakataa! Timiza wajibu kama ilivyoandikwa maana hatujui siku wala saa! Tuko nuruni ama gizani! Maana dunia yetu imejaa hadaa nyingi na ni wachache ama hakuna kabisa! Anaejua hatma yetu hapa duniani. Pengine hata mwenyewe alieiumba. Kuna mambo yanakanganya sana
 
Mchungaji yupo sahihi ki biblia.
Japo ki ubinadamu hajatumia Hekima.

Zaka ni muhimu kwa Kila muumini wa Yesu Kristo.
Sadaka ni muhimu

Lakini matoleo.mengineyo ni Hiyari na Utashi wa mtu
Zaka na sadaka ni agano la mtu na Mungu. Hujui mtu kaongea vipi na Mungu wake so usije ukamlazimisha kitu. Kuna wakati watu wanamkopa Mungu kwa kumuomba kabisa au wanaomba wasamehewe kutokana na wanachopitia. Mungu akimjibu mtu hitaji lake wala padri au mchungaji hautajua unless upo kwenye mchakato huo na Roho Mtakatifu. Acheni kuingilia personal relationship kati ya mtu na Mungu. Wewe fundisha halafu usubirie.
 
Hamia Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume uje ufaidi mema yote ya huu ulimwengu! Huku kwetu hakuna mambo ya kufuatana! Paroko yuko zake busy huko Parokiani!

Uende Kanisani, usiende! Hakuna anayejali! Umetoa zaka, hujatoa! Hakuna atakaye kusumbua! Watu wanamwagilia moyo kwa kipimo! Maana hata Mapadre wenyewe wanamwagilia sana tu!

Hakika ukiwa muumini wa RC migogoro utaisikia kwa majirani tu!

Kristu....!

Tumsifu Yesu Kristu.....!!

Kanisa la Kisinodiii....!
 
Mafundisho ya wapi hayo?
 
Nyie si ndiyo huwa hamziki mtu akifariki asipofanya hayo au unamtania mwenzio nyie ni zaidi ya huyo mchungaji
 
Nyie si ndiyo huwa hamziki mtu akifariki asipofanya hayo au unamtania mwenzio nyie ni zaidi ya huyo mchungaji
Mpaka itokee hivyo, maana yake wewe hujawahi kabisa kukanyaga Kanisani! Hujawahi kutambulika kwenye Jumuiya yoyote! Una mitala ya waziwazi!

Kinyume na hapo, hakuna atakaye kutenga.
 
Ona huyu.
Wewe baba yako alikula ugali maharage akamtafuta mama yako wakajamiiana wakatoa manii ambayo ni ugali maharage ukatoka wewe Leo unasema MUNGU HAYUPO.
Kwani wewe ni mke wake mungu hadi uje kumtetea hapa?
 
Mafundisho ya wapi hayo?
Braza kutoa ni wewe na Mungu wako. Haimhusu mchungaji wala kanisa. Mahusiano yako personl na Mungu yanaamua ufanyeje na uchumi wako. Wewe kama unatoa kama ng’ombe utaendelea kutajirisha wachungaji bila kuona matokeo. Sijawahi mpa mchungaji zaka au sadaka toka nijue natakiwa niongee nae kwanza. Nisipokua nayo namwambia namuomba na amani yake ipotayo amani zote inanipa imani amenisikia. Pole unayepelekeshwa.
 
tatizo la kwenda kwenye makanisa yanayomilikiwa na mtu binafsi.Et kanisa linaitwa la mtu fulani naumia sana.
 
Sema waroman wako vizuri, kila unachotoa kinatangazwa idadi yake ili waumini wote mjue kabisa kanisa limeingiza shi ngapi na ata manunuzi wanatangaza, ila madhehebu mengi ya walokole hawatangazi ni kama mali za wahubiri
 
Kudai fungu la 10 kwa stahili hiyo SIO SAWA na haikubaliki,
Kama wameelemewa na madeni hiyo haikuhusu ,
Kanisa linaelemewaje na madeni? Hiko ni kipimo kuwa hawafanyi kazi zao vizuri na hawakai kwenye nafasi zao sawasawa.
Hayo madeni yao yasije yakawanyima kupokea baraka.
Mwisho, namalizia na wale wale wanaopinga fungu la 10, kwa sisi waamini fungu la 10 ni la Mungu na ukila umekula pesa ya Mungu. Katika 100,000 fungu la Kumi ni 10,000 ni ndogo na haikutii UMASKINI. Katika vitu nazingatia ni fungu la Kumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…