Wachungaji kutaka fungu la kumi kwa lazima

Wachungaji kutaka fungu la kumi kwa lazima

Hamia Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume uje ufaidi mema yote ya huu ulimwengu! Huku kwetu hakuna mambo ya kufuatana! Paroko yuko zake busy huko Parokiani!

Uende Kanisani, usiende! Hakuna anayejali! Umetoa zaka, hujatoa! Hakuna atakaye kusumbua! Watu wanamwagilia moyo kwa kipimo! Maana hata Mapadre wenyewe wanamwagilia sana tu!

Hakika ukiwa muumini wa RC migogoro utaisikia kwa majirani tu!

Kristu....!

Tumsifu Yesu Kristu.....!!

Kanisa la Kisinodiii....!
Who's 'Yesu Kristu'? Hayo mema ya nchi ni kama yapi?
 
Watu wa Mungu wengi wana angamia kwa kukosa maarifa. Wanawake ndio wahanga wa hili jinamizi. Mungu hatolewi kwa amri. Mungu anatolewa kwa kuguswa umtolee ajabu makanisa ya leo wachungaji wanashindana na waumini. Tatizo ndio linapo anzia. Umejenga nyumba nzuri unaulizwa why unanyumba nzuri kuliko mch ndio hao akina wachungaji wamakanisa fulani wanasema kwa dakika mbili wamepata mil 300m hujiulizi. Kanisa limeingiliwa...
Kutoa zaka ni AMRI, siyo option. According tu maandiko.
 
Mchungaji anataka Zaka naye akanunue gari mpya yenye usajili wa namba E.
Mchungaji anataka kulipa ada za watoto wake.
Mchungaji anataka kula Sato na mchele wa Kyela.
Hayo yote hawezi kuyafanya bila Zaka zenu tafadhali toeni tu ndio makanisa mliyoyachagua pesa mbele kama kuvaa nguo ya. Ndani.
 
1Wakorintho 9:13-14 "

Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu na wale waihudumio madhababu huwa na fungu lao katika madhahabu? na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwaba wale waihubiriyo injili wapate ridhiki kwa hiyo

//

Mal 3:10-12 SUV

Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.

//

Mungu akubarikini nyote!
Amen
 
Samahani kama nitakuwa nimewakwaza ila FUNGU LA KUMI NI LAZIMA. Ki biblia hyo pesa 10% siyo yako, kwahyo ukiitumia kwasababu zozote zile ambazo kibinadamu ni zinaonekana ni za msingi unakosea, unakuwa kama umeiba (umemuibia muumba wako). FULL STOP!!!
 
Mimi kuna kipindi niliamua kusali makanisa ya kiroho(kilokole), ila kweli nikajiona kama ni kujifunga tu. Yani michango kibao mpaka nikawa nakosa amani.

Mkuu hizi kanisa za kuanzishwa na mchungaji mmoja mmoja ni pasua kichwa bora haya makanisa makubwa.

Mwisho kwenda kanisani ni utumwa
 
Kwani mm nimesema wakale wapi ,wanapaswa kuwa na vyanzo vya mapato vingine nq zaka sio kulazimishana haya ni mambo ya rohoni
Kabisa. Tunaambiwa Mtume Paulo alikuwa mshona mahema, itapendeza wakiwa na kitu kingine cha kuingiza kipato
 
Samahani kama nitakuwa nimewakwaza ila FUNGU LA KUMI NI LAZIMA. Ki biblia hyo pesa 10% siyo yako, kwahyo ukiitumia kwasababu zozote zile ambazo kibinadamu ni zinaonekana ni za msingi unakosea, unakuwa kama umeiba (umemuibia muumba wako). FULL STOP!!!
Kibiblia wapi? Nipe andiko. (Utakuja na andiko la Malaki 3:10 )

Unajua kuwa Malaki 3:10 ni AGIZO LA FUNGU LA KUMI KWA MUJIBU WA TORATI?
 
Mkuu naomba unisikilize kidogo
Wewe kama mkristo imara lazima uwe na yesu wako mwenye nguvu sasa hivi shetani achagui mtu wa kumvamia tuna watumishi wengi wa makanisani wamevamiwa na wamewezwa na shetani.
Sadaka zote unazoziona zimewekwa makanisani nyingi hata kwenye bibilia zilikua za kipindi cha agano la kale [ sheria] na huko zilikuwa.zinatokewa kwa lazima lakini tangu yesu aje na kutukomboa hatupo chini ya sheria kwaio kila kitu kizuri au kibaya unachokifanya tambua unakifanya kwa moyo wa kupenda ndio maana tumetadhaharishwa kutoipenda sana dunia na mambo yake.
Kifupi amani ya kristo iamue ndani yako ila huyo mchungaji kakosea sana tena anakufanya wewe kama mali yake binafsi as a bread win
Usipotoa zaka na sadaka Mchungaji na familia yake wale nini ?
 
Mkuu naomba unisikilize kidogo
Wewe kama mkristo imara lazima uwe na yesu wako mwenye nguvu sasa hivi shetani achagui mtu wa kumvamia tuna watumishi wengi wa makanisani wamevamiwa na wamewezwa na shetani.
Sadaka zote unazoziona zimewekwa makanisani nyingi hata kwenye bibilia zilikua za kipindi cha agano la kale [ sheria] na huko zilikuwa.zinatokewa kwa lazima lakini tangu yesu aje na kutukomboa hatupo chini ya sheria kwaio kila kitu kizuri au kibaya unachokifanya tambua unakifanya kwa moyo wa kupenda ndio maana tumetadhaharishwa kutoipenda sana dunia na mambo yake.
Kifupi amani ya kristo iamue ndani yako ila huyo mchungaji kakosea sana tena anakufanya wewe kama mali yake binafsi as a bread win
Nashukuru kwa ufahamu na mchango wako mkuu amani ya Mungu na iamue ndani yangu barikiwa sana
 
Samahani kama nitakuwa nimewakwaza ila FUNGU LA KUMI NI LAZIMA. Ki biblia hyo pesa 10% siyo yako, kwahyo ukiitumia kwasababu zozote zile ambazo kibinadamu ni zinaonekana ni za msingi unakosea, unakuwa kama umeiba (umemuibia muumba wako). FULL STOP!!!
Lakini unajua lile andiko linalonena ya kuwa yule asiyewajali wa nyumbani mwake ni mbaya kuliko yule asiyeamini ....mambo yamebana option nimeona nikazanie kwanza wa heman mwangu
 
Wakuu habarini

Mimi ni muumini wa kanisa la mahali pamoja ambalo ni T.A.G(X)

Jana nimepokea ujumbe wa kunikwaza kunifedhehesha na kunifanya nione kama natwaga maji kwenye kitu

Jana mchungaji kanitumia msg akiniuliza mbona sijahudhuria jana kanisani? Au na mpango wa kuhama kanisa !!

Nami 'nikamjibu kwa kumpigia simu nikamwambia mbona nilikuandikia msg kuwa nadharula sitahudhuria ibadani hukuupata ujumbe na nilimtumia pia na mzee nikakata simu nikascreen short msg nikamtumia whatsap

Akanijibu kuwa dharula zipo ila kama ni siku ya ibaada utume sadaka na michango , ni muhimu sana nikaa kimya

Leo Asubuhi nimeamka asubuhi nikiwa na ratiba ya kutoka kumpeleka mama yangu mzazi cliniki ya dialysis Bugado wakati natoa kausafiri kwenye chasis number alikuwa anapita tukasalimiana na kumwambia tunaelekea Hospital akasema sawa na hongera nyingi za kunua kausafiri kapya.

Imefika saa nne nipo hospitali naona Msg tena
akiniandikia ujumbe unasomeka hivi"

Leo ni mwisho wa mwezi na jana haukuwepo ibadani Tuma sasa hivi FUNGU LAKO LA KUMI UTUME NA HELA YA KUTOLEA KANISA LINA MADENI MENGI ""

Nikausoma nikatulia nakuvuta pumzi nikamtumia msg KUWA KWA SASA SINA PESA, FEDHA NINAYOBAKIA NAYO NI KWA AJILI YA MATUMIZI MUHIMU YA FAMILIA NAJUA PIA ZAKA UMUHIMU WAKE, nikikaa sawa nitatoa wala haina shida na hapo ndio nilikuwa najiandaa kulipia matibu ya mama kila mwezi natakiwa kulipia Milion 3 .8 kwa ajili ya dialsis ,mwez huu mambo yameyumba kabisa .

Akajibu tena wewe unabadili tu magari kwa habari ya zaka hutaki kutoa nikamwambia kwani zaka ni lazima lini sijatoa zaka zaidi ya mwezi huu nimepata msiba, na unanihusu kwa sehemu kubwa sina fedha na ninauguliwa wewe mwenyewe shahidi hali ya mzazi wangu Muda wote gari inapaswa kuwa na mafuta, muda wowote hali inabadilika tukawa tumeachana hivyo

Sasa hebu mnisaidie huu utaratibu unatoka wapi kwanini sadaka na zaka ni lazima au ni vile mtu anavyoguswa kulingana na Vile anavyopata! Maana Mungu anasema nijaribu sasa huku Naona mchungaji anatumia command utadhani kanipa yeye kisa anamadeni.

Hebu nipeni njia itakayoniondoa kanisa mikwaruzo na Mchungaji
Kwanini ufahamike kanisani? Tuanzie hapo kwanza. Mara nyingi kiherehere ni mbaya
 
Daaa ama kweli wakoloni waliwaweza.

Dini ni upumbavu
Dini ni utapeli
Dini ni kifo cha Roho na akili
Dini ni kificho cha maovu
Dini ni biashara
Dini zote ni uongo mtupu
Dini zote Muanzilishi ni mmoja aliyekuwa na madhumuni tofaut kwa wapumbavu haswa Afrika.

Sadaka ni njama ya wahuni iliyopenyezwa ktk imani haswa ukristo kwa kivuli cha ulazima na Amri ya Mungu kuwa ukitoa unabarikiwa.

Sadaka chanzo chake ni hao waroma waliotunga dini ili kujipatia kodi na kuinua mapato na uchumi wa romani empire, baadaye walihalalisha michango hiyo makanisan na kuiingiza ktk imani na vitabu vya dini ili michango hiyo(sadaka) ionekane ni matakwa ya Mungu kuwataka watu watoe vitu vyao makanisani.

Sadaka hizo zilikuwa kama nyenzo muhimu ys kukuza uchumi wa kanisa na falme inayomilik kanisa.

Baada ya mgawanyiko wa makanisa na mvunjiko wa catholic, vikazaliwa hivyo vijidhehebu vinavyojifanya vinautukufu ilihali vimekopy na kupaste sheria zoote za catholic ikiwepo mafundisho na hata maandiko yenu ya UONGO kutoka ktk BIBLIA.

MUUMBA wa KWELI hana haja ya sadaka na hatowai kuitaka sadaka yako, maana kila kitu ni chake, so how come akudai?

Hata hivyo kwa mujibu wa biblia zenu japo zimechakachuliwa lkn ukwel unabaki kuwa, Maana ya kanisa ni wew mtu mmoja mmoja ama unaitwa hekaru, kwamaana makao ya ROHO MTAKATIFU, hivyo hayo magenge yenu hayana sifa ya kuitwa kanisa, kwakuwa humo ROHO MTAKATIFU hawezi kukaa, na hata hivyo kanisa aliloliacha kristo ilikuwa ni wafuasi wake waliofuata mafundisho yake, na sio madhehebu.

Madhehebu yameibuka juzi tu baada ya uharibifu wa imani yakweli.

Neno sadaka halikutakiwa kuitwa hivyo ktk imani yakweli, labda kama wamaanisha sadaka ktk ushirikina tu,

ktk imani ya kweli kuna MSAADA ambao mtu unautoa kwa hiyari yako tu, napo unautoa kwa watu wahitaji kama vile, wagonjwa, vilema, mayatima, wazee, masikini n.k,

Na kuna sheria kabisa kuwa ukimsaidia mtu kwa uaminifu basi utalipwa kulingana na uaminifu wako haijarishi unaamini uwepo wa Muumba ama, au unashika mafundisho yake, lkn sheria hizi za Kusaidia zina Function bila ubaguzi maana MUUMBA wa kweli hajawai bagua viumbe wake, na sheria zake ni HAKI kwa kila kiumbe.

Hivyo basi utowapo hayo mamichango mnayowapa wachungaji makanisan, juwa kuwa unashiriki ibada za makafara na matambiko ya kishetan kwa kujua ama kutokujua,

Mambo haya hutowai ambiwa na mchungaji yeyote yule, maana yanaharibu biashara zao za kishetani za makanisa.

Mchango kwa wahitaji ni uamuz wa mtu kutoa ama kutotoa, na ukitoa kihalali basi sheria ya GIVE AND RECEIVE itafanya kazi kwako, ndiomaana matajiri wengi wanazidi kutajirika maana wanajua siri ya kutoa kwa masikini vituoni na wagonjwa, na huwezi waona wakiyatolea hayo matapeli yanayojiita wachungaji.

Ukristo na uislam ni imani moja ktk mgawanyo tofauti, haya yote ni makundi yanayofanya kazi ya siri ya kudidimiza maisha ya waafrika, kuwafunga akili na kuwafanya waabudu mashetan badala ya kumuabudu Muumbwa wakweli.

Hama ilo kanisa na achana na mambo ya dini, kazana kuwasaidia masikini FULL STOP.

YEYOTE ATAKAYEFANYIA KAZI MANENO HAYA HAKIKA MATUNDA MAZURI ATAYAONA NA KURUDISHA USHUHUDA HUMU
Yaani hizi biashara za dini ndio zinazidi kuchangamka. Mimi ni muislam, na uislam unaelekeza zaka zilipwe vipi na kina nani wanufaika. Mojawapo ya wanufaika ni ndugu, wagonjwa, watoto yatima, wajane. So zaka yangu naelekeza huku. Kuna watu sijui ni kutoka sehemu gani, wanapita kila asubuhi hospital nyingi za serikali kuwapa wagonjwa chakula. Unakuta wamebeba michupa mikubwa ya chai na vitafunwa wanapita kila wodi. Na wanafanya hivyo kila siku. Hiyo ndio maana ya sadaka na zaka sio tunawapelekea walioshiba
 
Lakini unajua lile andiko linalonena ya kuwa yule asiyewajali wa nyumbani mwake ni mbaya kuliko yule asiyeamini ....mambo yamebana option nimeona nikazanie kwanza wa heman mwangu
Mimi naishi na watoto wa ndugu zangu, nimeamua kuwasaidia ili waweze kujikwamua kimaisha, hiyo nayo ni sadaka kwangu
 
Back
Top Bottom