Wachungaji/Maaskofu/Manabii 10 matajiri sana Tanzania

mkuu namba kumi sikuelewi pamoja na u legend wake unataka kusema kazidiwa adi na namba saba?
 
wanalipa kodi?
hahahahaha hizo ni taasisi za ukwepaji Kodi mkuu,

Anyway mkuu hiyo Avatar Yako ya Marvin Gaye nimeikubali na wewe ni shabiki kindaki ndaki wa nyimbo zake kama Mimi?

Inner city blues
What going on
Sexual healing
Let's get it on
Little darling
NK nazikubali Sana na Kila siku lazima niplay Kwa Saabufa mojawapo!
😁😁😁😁🔥🔥
 
Kuna pia Mercy Mercy me, huyo jamaa alikuwa na nyimbo nzuri sana!!
 
Ninaishi jirani na kakobe, hana nyumba yenye thamani ya bil 4, kwa uzoefu wangu haifiki 150M.
Usifanye mchezo na bil 4 kwa nyumba ya kuishi
 
Hapa nimegundua tajiri namba moja ni mwakasege kwasababu yeye ni mwalimu anawafundisha umati wa watu uchumi halafu wanarudi makanisani kwao . yeye hajamiliki kanisa kwahiyo hajikusanyii sadaka za watu. Hawa wengine wote ni chumba ulete makanisa na sadaka zote ni Mali yao ndio maana wafuasi wao wengi wansfilisika kwa kuuza Mali zao na kuwwapelekea wao
 
Quran 9:34

Enyi mlio amini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa baat'ili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu.


 
Mungu anasema wengi kati wanazuoni wa kikristo na wa kiyahudi wanakula mali za watu (waumini wao) kwa batili na hupenda sana kujilimbikizia dhahabu na fedha huku wakifundisha mafundisho ya kuwapotosha waumini wao wasimuelekee Mungu.
 
ISAYA 56:10

Walinzi wake ni vipofu, wote pia hawana maarifa; wote ni mbwa walio bubu, hawawezi kulia; huota ndoto, hulala, hupenda usingizi.

11 Naam, mbwa hao wana choyo sana, hawashibi kamwe; na HAO NI WACHUNGAJI wasioweza kufahamu neno; wote pia wamegeuka upande, wazifuate njia zao wenyewe, kila mmoja kwa faida yake, toka pande zote.
 
Waarabu wa mbagala wakiiona hi list ya matajiri wapya tanzania..wananuna..wataanza kusema wanahujumiwa..njooni mueneze injili mtajirike...acheni uoga na wivu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Usipo kubali kuliwa kidogo huli..unataka hao wachungaji wakale wapi..halafu unawaonea huruma hao waumini..kunasiku walikuja kwako kuomba msaada wa chakula au malazi..kisa hela zao zimeishia kwa manabii.

Peleke upumbafu wako huko...acha waeneze injili.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wivu tu..wanawazui vipi wakati wanawahubiria habari njema.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…