Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

Watu wameanza kuwastukia !

Mtaanza kukusanya sadaka kwa nguvu kubwa sana maana ni kama vile mlikuwa mnakula na vipofu sasa mkajisahau mkawashika mikono!
Umeambiwa wewe kama hutaki kubarikiwa endelea kuwa mchoyo kwa Mungu, sisi wenzio tunatoa kama kawaida na tunabarikiwa sana tu.
 
Kumbe shida yako ni sadaka kuwa nyingi!??? Yaani unamwonea husda hata Mola!??? Ulitaka apate elfu 10 tu, siyo!???
 
Umeambiwa wewe kama hutaki kubarikiwa endelea kuwa mchoyo kwa Mungu, sisi wenzio tunatoa kama kawaida na tunabarikiwa sana tu.


Mimi natoa na nitaendelea kwa kadiri ya neema za Mungu zinavyozidi kuachiliwa kwangu sababu faida ya kumtolea Mungu nimeiona katika uhalisia wa maisha!

Imeandikwa : kheri kutoa kuliko kupokea!

Kheri = Baraka

Yani kuna Baraka (neema ya uwezesho wa kufanikiwa kiroho na kimwili) kwenye aspects mbalimbali.

Lakini bado hao mabwana kuna mahali wanatakiwa wajirekebishe.
 
Kumbe shida yako ni sadaka kuwa nyingi!??? Yaani unamwonea husda hata Mola!??? Ulitaka apate elfu 10 tu, siyo!???


Ikiwa nyingi maana yake achukue bank afanye atumie kwa haja iliyopo , kwanini tena unawachangisha watu kutoka mifukoni au mikobani mwao?

Kungekuwa na uwazi watu wakijiridhisha kweli bank hela imetumika ipasavyo wangekuwa wanatoa kiroho safi tu.

Kwanini mnaficha taarifa za fedha?
 
Hivi mfano Mwamposa akienda shamba kulima au afungue.genge atauza saangapi na ibada ataifanya saangapi,,!
Kati ya Mwamposa na Mtume Paulo, aliyefanya kazi kubwa ya kitume ni nani? tuanzie hapo kwanza.
 
Kanisani natoa sadaka tu. Misaada mingine napeleka kwa wajane, wagonjwa, watoto na wengine wenye mahitaji.
Kanisani wataambulia sadaka yangu tu tena niliyoipanga mwenyewe.
 
Kuna Mchungaji fulani alimuweka mhasibu , akamwambia Naomba nisaidie maswala ya kihasibu Hapa kanisani .

Sasa yule Mhasibu ni Mweledi.

Basi Mchungaji kila akitaka hela anakwambia Mhasibu nataka kiasi fulani cha fedha, Mhasibu anamwambia sawa lakini naomba niandikie kwenye karatasi au form ili niweze kutunza kumbukumbu kwa usahihi.

Yule Mchungaji akawa hataki jambo hilo hatimae akamuondosha pale kanisani.

Anamwambia kanisa nilianzishe mwenyewe, halafu nikitaka hela unipangie utaratibu? Akamtoa kabisa.

Hivyo ndivyo mambo yanavyofanyika!
 
Wanajifanya hawajui ule mstari wa Matendo ya Mitume 20 35 = "heri kutoa kuliko kupokea" 🙏✝️
 
Huyo muhasibu ni mwaminifu. Mwingine angepata fursa ya kujichotea pesa kiulaini maana zinatoka tu bila record yoyote .
 
Kwa hiyo wewe umeona kutoa mapepo ndiyo ishu?
Hujajibu hoja ya msingi!
Utolewaji wa taarifa umuhimu wake ni zaidi ya unavyoweza kufikiri juu ya hilo swala lako la faida.


Watu wameanza kuwastukia [emoji108][emoji108]
Taarifa za nini unataka kuhakiki nini?Kwani hiyo biashara udai Kodi. Kutoa Mapepo ndiyo taarifa muhimu kuliko zote katika Imani maana Mapepo ndiyo yanyoharibu dira y amwandamu
 

Kwahiyo Dini ni Biashara? Nipe verse ya Bible au Quruani Yesu au Nabii Issa kama alikuwa anaomba sadaka kwa ajili ya kutanua huduma.
 
Taarifa za nini unataka kuhakiki nini?Kwani hiyo biashara udai Kodi. Kutoa Mapepo ndiyo taarifa muhimu kuliko zote katika Imani maana Mapepo ndiyo yanyoharibu dira y amwandamu


Huo sasa ni uhuni!

Kwa ufahamu wako unazani taarifa inatakiwa kwa kwaajili ya kodi tu?

Ndiyo ulivyojifunza?

Waulize wajuvi wa mambo wakuambie!

Halafu kutoa pepo siyo kusudi la msingi wa kanisa kwa taarifa yako!

Yani kuna ujinga mwingi sana unaoendelea huko ila mjue mtadaiwa.

Msitumie ujinga wa watu kama mtaji wa kuwapiga kimtindo!
 
Imani na ulimwengu wa roho Ni mpevu zaidi kuliko upeo wako wa kufikiri. Kanisani kwenyewe unatoa jero au Mia halafu unapiga kelele.Wewe hata hujiulizi ulipata wapi Akili ya kutafuta pesa Ila unajiuliza kwanini unatoa sadaka
 
Taarifa za nini unataka kuhakiki nini?Kwani hiyo biashara udai Kodi. Kutoa Mapepo ndiyo taarifa muhimu kuliko zote katika Imani maana Mapepo ndiyo yanyoharibu dira y amwandamu


Kutoa mapepo naona imekuwa fasheni siku hizi kwa makanisa ya kiafrika!

Kila kanisa ukienda watu ni mapepo, ukifungulia TV channel ni kuangushwa watu mapepo na unabii fake!

Kusudi kuu la kanisa ni Mathayo 28:19 -20 Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu mkiwabatiza kwa jina........na kuwafundisha kuyashika yote..........
 
Kwa kawaida maneno ya yasiyo na maana yakiandikwa kwa kiingereza yanaonekana yana maana. Ndicho ulichofanya hapa:

1. Awali ya yote....tofaut ya waislam na wakristo juu ya yesu sio kutokuwapo yesu hapa duniani bali ni asili ya yesu....je ni nabii au mungu? - kila mmoja ana ushahidi tofauti.


2. Kutovunjika kwa mayai hakumaanishi Mungu yuko in control vinginevyo nieleezee kwanin kuna wanadamu wanakufa kwa njaa....mfano hapo sudani tu....yaan mtu akosa chakula anakufa....wewe unanambia mungu yuko in control kwasabb tu mayai hayakuvunjika.


3. Imani ni dhana isiyokuwa na ushahid kabsa. Haiwez kujitetea yenyewe bila kuingiza woga na dhana sizizothibitika. Mfano. Unaposema kuna: unazungumzia swala la watu waliokwisha kufa hali hawajawah kuskia ukristo wala uislam....hawa watu wataenda motoni au peponi? Unazungumziaje dhana kwamba mungu wa upendo atawachoma wenye dhambi milele na milele?


4. Ukiyachunguza maandiko hasa biblia....basi hutajihusisha nayo tena. Kwanza mungu wa agano la kale ana tabia na hulka za kibinadamu....pia ana mtizamo tofaut wa kiiman ukilinganisha na mungu wa agano jipya. Ukienda mbali zaidi....mungu wa agano la kale alikuwa muuwaji na mpenda visasi kama viongozi wa kiimla.


Kwa vyovyote vile, imani hasa za ya haya makanisa ya kisasa....zinapaswa kupigwa vita na yeyote mwenye akili timamu.
 
Sadaka inaendelea hata kama hakuna mahitaji ya moja kwa moja. Matumizi yake ni endeleeni/endelevu. Halafu unataka uwazi gani kutoka kwangu mm tangu lini nimeshika dollars zako Mr Akilinjema!??? ^Tuulizeni maswali yenye busara, tafadhali jmn^~Prof. J
 
Sadaka inaendelea hata kama hakuna mahitaji ya moja kwa moja. Matumizi yake ni endeleeni/endelevu. Halafu unataka uwazi gani kutoka kwangu mm tangu lini nimeshika dollars zako Mr Akilinjema!??? ^Tuulizeni maswali yenye busara, tafadhali jmn^~Prof. J


Kipimo cha Busara ni kipi [emoji2369]

Tumewastukia!

Ujinga wakati wa kwenda kurudi huwa ni werevu [emoji108][emoji108]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…