Wachungaji mnaosema tukiwapa sadaka tutabarikiwa kuwa wateja wa kwenye ma Mall, mnajiona mko sawa?

2021 ni Mwaka wa upako hallelujah!?!!

Umenisurprise,I'm so excited to see this spiritual msg from you
 
Kuna siku tulikua kanisani, unajua mahibiri ya walokole ni mpaka mchungaji achoke kuongea. Imefika saa saba mahubiri yanaendelea na mke wa mchungaji anakunywa Coca-Cola kupoza koo.
nyinyi inauma njaa mwenzenu anakanda koo
 
Fact
 
Nafuu angetumia kale kawimbo "toa ndugu * 2 ulicho nacho bwana anakuona mpaka rohoni mwako " .watu wakitafakari bakuli linajaa. Kawimbo kananiacha hoi sana! Ila pamoja na bwana kuniona rohoni anatakiwa anipe mimi, yeye pesa ni zake hahitaji!
 
watu inabidi waelekezwe kuwa hawatoi sadaka ili wabarikiwe, maana wakiwa na mtazamo huo itakuwa kama michezo ya betting, lakini wafundishwe kutoa kwa moyo wa kupenda na katika kutoa huko Mungu atawabariki,, lakini wakienda na mtazamo kuwa tunatoa ili tubarikiwe wasipoona baraka hata imani yao itakuwa mashakani juu ya Mungu
 
Kwanza unasalije kwenye kanisa mtu anaongea ujinga huo..yaan mi na elimu yangu mtu aanze nihubiria ujinga..ntatoka nje kwa speed ya ajabu...nakumbuka miaka kadhaa demu wangu alinipeleka kanisa moja linaitwa ECG..makongo kule..kanisa la washua..mademu wa mjin kama wote..parking imeshehen mandinga ya hatar..yule mchungaj akawa anaongea mambo siyaelew..kujisifia kwingiii..mara kafanya biashara hii mara ile..uongo uongo ujanja ujanja mwiingiii..utoto wa mjin mwiing.aisee.nilitoka nje nkaenda msubir demu kwenye gar amalize tuondoke..
 
Sadaka ni matoleo ya hiari ambayo mwanadamu hutoa kwa kile anachoamini kuwa ni Mungu kwake,na mwanadamu kwa kufanya hivyo hukiri kuwa bila huyo Mungu anayetoa kwake yeye hawezi.Kwa maana hiyo kila mwanadamu hutoa sadaka kama hatoi kanisani au mskitini kuna mahali anatoa na huko ndiko moyo wake ulipo.
 
Kitambo nyuma nami nilikuwa mmoja wa wenye hii misimamo ila kwa sasa wacha niendelee kuwapa hizo sadaka maana nikikumbuka jinsi familia yangu na mimi mwenyewe tulivyoteseka kwa miaka karibia 9 na watoto wangu WOTE kuingizwa kwenye UCHAWI na mmoja wao kuanza kupata UCHIZI, sina mabishano kwenye jambo la imani la mtu,,,, halafu sasa ajabu ni kuwa aliyefanya akifanya yote haya ni mama yangu wa kambo akishirikiana na ndugu damu na mimi ,,,,

Nachoamini IMANI ni FUMBO wala mtu yeyote asijione ye ndo msafi saaana, kwa wale ambao wameshapelekwa mputa mputa na ndugu wachawi watakuwa wanajua,,, halafu kwenye UMASKINI ndo kuna shuhuda nyingi za hawa MITUME na MANABII wetu ambao wengine ni FEKI KWELI, maana huku KUROGANA NDO KWENYEWE,... ukifanikiwa kidogo umetengeneza maadui kuanzia ndugu wa damu mpaka majirani..... Siye tutaendelea kutuma shuhuda zetu kwa akina Mwamposa na Kuhani Musa maana tuliyotendewa Mungu ndo anayejua......
 
Ulijuaje ni mamaako wa kambo?
 
aliyeunda iman ya kikristo kuna tatizo kwenye nguzo zake. zinaruhusu mianya ya kuingiza ujinga na kutojitambua hasa katika nchi zenye shida nyingi za kibinadam zinazohitaji majibu ya kibinadam kama umaskin, magonjwa na saikolojia. mi mkristo lakin naona hata katika uongoz wa kisiasa wenye iman za kikristo ndo wamefanya mambo ya ovyo sana na ya kikatili dhid ya watu wao wanaoongoza! hofu ya Mungu inakuwa too low! atakayekwazika anisamehe, labda nimeponzwa na record.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…