Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Nimekuwa napenda sana kuwa kwenye mahusiano na wadada waliofungashia, kiuno nyugwi na sura ya kuvutia; kitu kinachonifanya nikutanapo na yeyote mwenye sifa hizo, najikuta mwili wote unalegea na kukosa amani, na kunilazimu kunadi sera zangu kwake.
Kuna siku nilikuwa Dodoma; ile asubuhi tu naenda mapokezi kukabizi funguo za chumba lodge, nikakutana na bonge la toto ambaye naye alilala pale nilipofikia alikuwa anapata chai. Nilipomtazama tu, nikaanza kuchanganikiwa, ikanilazimu niende kukaa naye meza moja huku nami nikinywa chai.
Nikaanza kumuongelesha maneno mawili matatu, ila akanijulisha aliingia jana na atakuwepo kwa siku kadhaa hapo, ila kwa upande wangu nilitakiwa niondoke siku hiyo. Nikawa nasikitika kumuacha mtoto mzuri huku nafsi ikisononeka. Nilijaribu kumuomba namba ili tuwe tunawasiliana, na alinipatia ila kuja kupiga ikawa haipatikani mpaka leo.
Mpaka leo nafsi yangu inaniuma sana nikimkumbuka huyo mrembo.