Wadada, kwa nini mnatupatia namba feki?

Wadada, kwa nini mnatupatia namba feki?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Nimekuwa napenda sana kuwa kwenye mahusiano na wadada waliofungashia, kiuno nyugwi na sura ya kuvutia; kitu kinachonifanya nikutanapo na yeyote mwenye sifa hizo, najikuta mwili wote unalegea na kukosa amani, na kunilazimu kunadi sera zangu kwake.

Kuna siku nilikuwa Dodoma; ile asubuhi tu naenda mapokezi kukabizi funguo za chumba lodge, nikakutana na bonge la toto ambaye naye alilala pale nilipofikia alikuwa anapata chai. Nilipomtazama tu, nikaanza kuchanganikiwa, ikanilazimu niende kukaa naye meza moja huku nami nikinywa chai.

Nikaanza kumuongelesha maneno mawili matatu, ila akanijulisha aliingia jana na atakuwepo kwa siku kadhaa hapo, ila kwa upande wangu nilitakiwa niondoke siku hiyo. Nikawa nasikitika kumuacha mtoto mzuri huku nafsi ikisononeka. Nilijaribu kumuomba namba ili tuwe tunawasiliana, na alinipatia ila kuja kupiga ikawa haipatikani mpaka leo.

Mpaka leo nafsi yangu inaniuma sana nikimkumbuka huyo mrembo.
 
We unasema ivo tu....hujawahi kutana na binti wa kisukumaa...unakuta ana simu ila ukimuomba namba anakwambia hana simu...yaan wananishangaza sanaa hawa dada zao kina ngosha...na unakuta jibu ni moja kwa wote...hadi unashangaa wanaambizana?
 
Wanakuwa wanaogopa nini mkuu?
 
Kitu ambacho si entertain ni kuomba omba hovyo namba wanawake. Moja kusumbuana kuchati hovyo hovyo, pili ukiomba namba jua wewe ni mzazi mwenza utalipa hadi ada za wajukuu.

Mkuu mnawezaje kuomba namba kwa kuonana na mtu mara moja na mkaweza wasiliana?
 
Tatizo mkuu, moyo unapenda sana
 
Nimekuwa napenda sana kuwa kwenye mahusiano na wadada waliofungashia, kiuno nyugwi na sura ya kuvutia; kitu kinachonifanya nikutanapo na yeyote mwenye sifa hizo, najikuta mwili wote unalegea na kukosa amani, na kunilazimu kunadi sera zangu kwake.

Kuna siku nilikuwa Dodoma; ile asubuhi tu naenda mapokezi kukabizi funguo za chumba lodge, nikakutana na bonge la toto ambaye naye alilala pale nilipofikia alikuwa anapata chai. Nilipomtazama tu, nikaanza kuchanganikiwa, ikanilazimu niende kukaa naye meza moja huku nami nikinywa chai.

Nikaanza kumuongelesha maneno mawili matatu, ila akanijulisha aliingia jana na atakuwepo kwa siku kadhaa hapo, ila kwa upande wangu nilitakiwa niondoke siku hiyo. Nikawa nasikitika kumuacha mtoto mzuri huku nafsi ikisononeka. Nilijaribu kumuomba namba ili tuwe tunawasiliana, na alinipatia ila kuja kupiga ikawa haipatikani mpaka leo.

Mpaka leo nafsi yangu inaniuma sana nikimkumbuka huyo mrembo.
Duh..
 
Back
Top Bottom