Chakorii
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 18,773
- 51,429
Maneno huumba,yatupasa kuwa makini sana na nini tunakitamka..maneno huishi.Watu huwa hawajui kwamba, maneno unayomuambia mtu kama ni ya uongo unapata laana kama huyo mtu atakunenea mabalaa.
Kuna binamu yangu alimpa msichana mimba huko upareni, akakataa ile mimba. Mama yake bint akamuambia, kama mimba ni yako hutakaa upate mtoto mwingine maishani mwako.
Na ikawa hivyo. Ndugu yangu amekufa na miaka 44 bila mtoto mwingine, hata huyo aliyemkataa hakumuona tena maishani mwake. Ndugu yangu huyo tena alikufa kifo cha fetheha mwaka juzi akiwa guest na mwanamke.
Kuna kipindi nilitamka maneno mabaya sana Kwa mtu wa karibu nami..guess what sasa…ilinichukua siku zaidi ya 120 kufunga na kusali nonstop mpka nilipokuja kupata Amani ya moyo ndipo nikaacha.
Ingawa nilikuwa naombea na mambo mengine lakini niliendelea kufunga nikaahidi siku nitakayopata Amani ya moyoni kila nikimkumbuka huyo mtu basi ndipo siku nitakayoacha kufunga.
Maneno na Imani ni vitu muhimu sana