Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

dahh! Tafadhali usiache kumsaidia huyo Mama.. muweke kwenye ratiba yako, ni sadaka kubwa mno! Kusaidia wajane na mayatima... unalipwa malipo makubwa sana! Utaona tu matunda yake hata kwa wanao.


Tafadhali usimuache huyo Mama

Na wewe nikupe namba umrushie chochote
 
Yaani siku hizi hadi vijijini wanaambiana wanawake angalia mfuko wa Mwanaume kama umenona!

Mapenzi yalikuwa zamani siku hizi ni maslahi kwanza!

Unconditional love is rare to find!
Sijui ni nani alianzishaga huu utaratibu kwamba mapenzi lazima yaendane na mali na pesa...🤔🤔🤔



Tukimpata huyo tutamtandika viboko vingi sana! 😅
 
Mwanaume anashida moja..akiona unampenda sana anakutesa..sasa ili kubalance mambo unakuwa na mbadala siku akileta miyeyusho chap unahama unaenda ota sehemu nyingine
We ndo umeona wazo au suluhisho zuri kwa upande wako au sio?!

Huwa nyinyi wenyewe mnajitoa chambo kwa vijana wa mtaani, bodaboda, walinzi, vinyozi na wauza mabucha.... mkijidanganya kuwa mnatafuta tulizo la nafsi au faraja 😅😅😅👍🏾

Vilevile, binafsi naamini wanawake huwa mnaongoza kupelekega ukimwi na maradhi mengine kwenye ndoa zenu kuliko wanaume.

Kutafuta mchepuko sio suluhu ni kuzidisha matatizo na misongo ya mawazo!

Mhenga mmoja alisema "Mwanamke mjinga anavunjaga ndoa yake kwa mikono yake yeye mwenyewe"
 
Unalala na mwanamke unajua kabisa wallet ina sh kazaaa unaamka unakuta kuna pungufuu aisee[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Hawa viumbe shidaa sanaaa ukimuitaa mwizi anaona unamdharauu kumbe tamaa zao ndo zinawaponzaa
 
Iwe mwanamke au mwanaume, tabia ya kuomba omba hela kama huna mikono si nzuri. Kwanza unajishusha hadhi yako, kijana una nguvu zako, kwanini umuombe mtu mwingine?

Umetongozwa unaanza mizinga!
Kabla ya kukutongoza ulikuwa unaishije? akikupenda atakupa kama mpenzi wake, acheni umatonya.
Natumai unayaishi maneno yako.
 
Jana wana JF kadhaa wenye club yetu fulani hivi amazing tulikuwa tumekutana The Wine Coutry kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2023.

Wanawake tulikuwa wawili tu, mimi na bidada mwingine na wanaume idadi yao ilikuwa kumi na kitu.

Jamani miongoni mwa mambo ambayo wanaume wanayaona ni kero ni swala la kupiga mizinga.

Wanawake tena mmetajwa kwa majina ambao mnashinda inbox mki zingalaizi. Mara mama anaumwa, mara dada kagongwa na bodaboda, mara nitumie hela ya kusuka nywele mara sina ada ya watoto.

Jamani kwa kweli mnahoyafanya huko PM aibu nimeona mimi. Ukitongozwa ndio usiseme. Hata kama una kazi ya ajira, tena mwajiriwa wa serikali, unaomba kuanzia vocha hadi hela ya chupi.

Wewe uko Dodoma mwanaume yuko Dar hajawahi hata kukulala zaidi ya kuonana mara moja na tena ulikuwa kwenye siku zako.

Nimekutaja wewe dada wa Dodoma sababu umekuwa na tabia ya kuwatongoza wanaume na baadae unaanza kuwa kero kwao na mizinga unayowapiga.

Jamani nawakaribisha Lindi tulime ufuta mbona kilimo poa tu, unapata hela ya kukukimu na huadhiriki.

2023 tubadilikeni jamani
Aloo yamekuwa hayo tena! Labda hajawapenda,akimpenda mtu mbona fresh tu anampa free tu. Kumbuka huyo ni mtoto wa kihuni wa Kinondoni
 
Back
Top Bottom