Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Jana wana JF kadhaa wenye club yetu fulani hivi amazing tulikuwa tumekutana
The Wine Coutry kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2023.

Wanawake tulikuwa wawili tu, mimi na bidada mwingine na wanaume idadi yao ilikuwa kumi na kitu.

Jamani miongoni mwa mambo ambayo wanaume wanayaona ni kero ni swala la kupiga mizinga.

Wanawake tena mmetajwa kwa majina ambao mnashinda inbox mki zingalaizi. Mara mama anaumwa, mara dada kagongwa na bodaboda, mara nitumie hela ya kusuka nywele mara sina ada ya watoto.

Jamani kwa kweli mnahoyafanya huko PM aibu nimeona mimi. Ukitongozwa ndio usiseme. Hata kama una kazi ya ajira, tena mwajiriwa wa serikali, unaomba kuanzia vocha hadi hela ya chupi. Wewe uko Dodoma mwanaume yuko Dar hajawahi hata kukulala zaidi ya kuonana mara moja na tena ulikuwa kwenye siku zako.

Nimekutaja wewe dada wa Dodoma sababu umekuwa na tabia ya kuwatongoza wanaume na baadae unaanza kuwa kero kwao na mizinga unayowapiga.

Jamani nawakaribisha Lindi tulime ufuta mbona kilimo poa tu, unapata hela ya kukukimu na huadhiriki.

2023 tubadilikeni jamani
Nimekutaja wewe dada wa Dodoma sababu umekuwa na tabia ya kuwatongoza wanaume na baadae unaanza kuwa kero kwao na mizinga unayowapiga.[emoji23]
 
Badilikeni. Baada ya mimi kutoa uzi wa kuzinguana na mke wangu, kuna dada alinifuata PM kwamba ananionea huruma sana kwa hali ninayopitia.

Tukazoeana zoeana baadae akasema ninamvutia kwa ile profile picture yangu ya WhatsApp kwa hiyo kama vipi niwe naye, nikaona poa tu, aisee

Demu anapiga mizinga kichizi. Halafu akiomba vocha, ukimtumia voda ya buku 2 anakutukana, eti mi unanionaje? Mimi vocha ya buku 2 ya nini.
Demu anapiga mizinga kichizi. Halafu akiomba vocha, ukimtumia voda ya buku 2 anakutukana, eti mi unanionaje? Mimi vocha ya buku 2 ya nini.[emoji23]
 
Iwe mwanamke au mwanaume, tabia ya kuomba omba hela kama huna mikono si nzuri. Kwanza unajishusha hadhi yako, kijana una nguvu zako, kwanini umuombe mtu mwingine?

Umetongozwa unaanza mizinga!
Kabla ya kukutongoza ulikuwa unaishije? akikupenda atakupa kama mpenzi wake, acheni umatonya.
 
Iwe mwanamke au mwanaume, tabia ya kuomba omba hela kama huna mikono si nzuri.
Kwanza unajishusha hadhi yako, kijana una nguvu zako, kwanini umuombe mtu mwingine?
Umetongozwa unaanza mizinga!!! Kabla ya kukutongoza ulikuwa unaishije? akikupenda atakupa kama mpenzi wake, acheni umatonya.
💯💯💯💯💯💯💯💯💯%%
 
Afutiwe dhambi zake zote huyu, sanamu lake lijengwe ubungo mataa, aende peponi moja kwa moja na asiulizwe swali hata moja, haya ni maelekezo yataekelezwe.
 
Jana wana JF kadhaa wenye club yetu fulani hivi amazing tulikuwa tumekutana
The Wine Coutry kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2023.

Wanawake tulikuwa wawili tu, mimi na bidada mwingine na wanaume idadi yao ilikuwa kumi na kitu.

Jamani miongoni mwa mambo ambayo wanaume wanayaona ni kero ni swala la kupiga mizinga.

Wanawake tena mmetajwa kwa majina ambao mnashinda inbox mki zingalaizi. Mara mama anaumwa, mara dada kagongwa na bodaboda, mara nitumie hela ya kusuka nywele mara sina ada ya watoto.

Jamani kwa kweli mnahoyafanya huko PM aibu nimeona mimi. Ukitongozwa ndio usiseme. Hata kama una kazi ya ajira, tena mwajiriwa wa serikali, unaomba kuanzia vocha hadi hela ya chupi. Wewe uko Dodoma mwanaume yuko Dar hajawahi hata kukulala zaidi ya kuonana mara moja na tena ulikuwa kwenye siku zako.

Nimekutaja wewe dada wa Dodoma sababu umekuwa na tabia ya kuwatongoza wanaume na baadae unaanza kuwa kero kwao na mizinga unayowapiga.

Jamani nawakaribisha Lindi tulime ufuta mbona kilimo poa tu, unapata hela ya kukukimu na huadhiriki.

2023 tubadilikeni jamani
Yaani, umenena haswa.
Wanawake wamezidi.

Mizinga kwa wengine ndiyo sehemu ya maisha.
Huwezi kusema wanajiuza , lakini kwa mizinga hadi inakera.

Kabla ya Chrismas ilibidi nizime kabisa simu.
Mwanamke hata uliyewahi kumkonyeza analeta furushi la matatizo yake.

Mwingine anataka umlale hata kwa yeye bibie kukutongoza ili apate mahali pa kuomba.
Ukimtolea nje utaona tu anahamia kwa mwingine.
Jana tu nimepata ujumbe ,ati mtoto ana birthday(si wangu). Mwingine anomba hela ya kodi ya nyumba. Mwingine anaomba ada ya watoto(si wangu)

Mwingine ndo kaniudhi, kaandika "we mwanaume naomba hela nina shida"

Wanawake sijui watajikomboa lini!
 
Back
Top Bottom