Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Yaani, umenena haswa.
Wanawake wamezidi.
Mizinga kwa wengine ndiyo sehemu ya maisha.
Huwezi kusema wanajiuza . lakini kwa mizinga hadi inakera.
Kabla ya Chrismas ilibidi nizime kabisa simu.
Mwanamke hata uliyewahi kumkonyeza analeta furushi la matatizo yake.
Mwingine anataka umlale hata kwa yeye bibie kukutongoza ili apate mahali pa kuomba.
Ukimtolea nje utaona tu anahmia kwa mwingine.
Jana tu nimepata ujumbe , mtoto ana birthday(si wangu)
Mwingine anomba hela ya kodi ya nyumba
Mwingine anaomba ada ya watoto(si wangu)

Mwingine ndo kaniudhi,kaandika "we mwanaume naomba hela nina shida"

Wanawake sijui watajikomboa lini!
Nawaoneeni huruma sana
 
Wewe ni wife material kabisa wallah..!
Ujengewe sanamu la kumbukumbu mlima Kilimanjaro.

Ila kwa bahati mbaya mara nyingi wanawake wingi mnakomaa kiakii wakati umri umekwenda, unakuta hata angani huendi tena.
I'm just 41. Nilianza biashara nikiwa ni ngali mdogo. Nimesha kuwa na dogs farm, nimefuga hadi nyuma sumu nikawa nauza nje hadi pale Corona ilipo strike.

Sasa nalima ufuta
 
Jana wana JF kadhaa wenye club yetu fulani hivi amazing tulikuwa tumekutana The Wine Coutry kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2023. Wanawake tulikuwa wawili tu, mimi na bidada mwingine na wanaume idadi yao ilikuwa kumi na kitu. Jamani miongoni mwa mambo ambayo wanaume wanayaona ni kero ni swala la kupiga mizinga. Wanawake tena mmetajwa kwa majina ambao mnashinda inbox mki zingalaizi. Mara mama anaumwa, mara dada kagongwa na bodaboda, mara nitumie hela ya kusuka nywele mara sina ada ya watoto. Jamani kwa kweli mnahoyafanya huko PM aibu nimeona mimi. Ukitongozwa ndio usiseme. Hata kama una kazi ya ajira, tena mwajiriwa wa serikali, unaomba kuanzia vocha hadi hela ya chupi. Wewe uko Dodoma mwanaume yuko Dar hajawahi hata kukulala zaidi ya kuonana mara moja na tena ulikuwa kwenye siku zako. Nimekutaja wewe dada wa Dodoma sababu umekuwa na tabia ya kuwatongoza wanaume na baadae unaanza kuwa kero kwao na mizinga unayowapiga. Jamani nawakaribisha Lindi tulime ufuta mbona kilimo poa tu, unapata hela ya kukukimu na huadhiriki. 2023 tubadilikeni jamani
 
Kuna muda unakutana na mdada mnajenga urafiki kabisa nakuwa naona huyu kwenye kazi zangu atanifaa ngoja niweke mambo Sawa kisha nitakaa nae mezani tuyajenge daaahh kabla hata ya kufka point ataanza kuomba omba pesa bila ya mpangilio kutaanza. Mara sijui mama mgonjwa, kodi inaisha nitarudi tuu kijijini na utanikosa, mtoto wangu anaumwa daaah kifupi Mnakatisha tamaa wadada na mnatuogopesha sana sisi wazee wa mishe.
 
Mimi juzi kuna yupo aliniomba 1000, nikamuuliza ya nini ,kasema ,
Ya kununulia mkaaa.

Kuna wanawake wanatia kichechefu balaa ,skujui hunijui unaomba 1000, alafu social media yupo active muda mwingi, hiii tabia sio nzuri ni kama kujidhalilisha tu.

Huyu mwanamke nilimnyima ni kama kumdekeza bila sababu, ndo kwanza januari.
 
Mimi juzi kuna yupo aliniomba 1000, nikamuuliza ya nini ,kasema ,
Ya kununulia mkaaa.

Kuna wanawake wanatia kichechefu balaa ,skujui hunijui unaomba 1000,alafu social media yupo active muda mwingi,hiii tabia sio nzuri ni kama kujidhalilisha tu.

Huyu mwanamke nilimnyima ni kama kumdekeza bila sababu,ndo kwanza januari.
Duh [emoji846]
Aisee wakati mwingine inabidi wajifunze kuvumilia kwa sababu hakuna jambo linalodumu.
 
Wadada left the chat🤣🤣🤣
Na nyie wababa msiombe mbususu🤣

Ila kuna wenzetu aisee ni kama viwete mtu anaomba elfu tatu. Jamani af tatu kweli? Nlivojitolea kuwatetea ila hapana kwa hili namimi nakaa pembeni. Mdada anacheza michezo na hana kazi. Ikifika siku ya rejesho keshategesha vizinga kama tisa hivi kote anaomba af mbili mbili aibu naonaga mimi
 
Iwe mwanamke au mwanaume, tabia ya kuomba omba hela kama huna mikono si nzuri.
Kwanza unajishusha hadhi yako, kijana una nguvu zako, kwanini umuombe mtu mwingine?
Umetongozwa unaanza mizinga!!! Kabla ya kukutongoza ulikuwa unaishije? akikupenda atakupa kama mpenzi wake, acheni umatonya.
Aisee!!!
 
Back
Top Bottom