Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Wadada tupunguze mizinga, inatudhalilisha sana

Uanaume sio umbo, ni matendo. Ukiombwa hela inbox au PM usitangaze. Binafsi sina hulka ya kuomba hela na kama yupo ambaye nimewahi kumuomba hela aweke screenshot nitamrudishia mara tatu.



Wanawake ombaomba hapa kweli wapo, wasemeni kwa upole na wala msiwaseme kwenye vikao vyenu vya kahawa.



NB:-

Wadada wote ombaomba, komeni mara moja
Wakisemwa kwa upole hawataacha,
Ungeshairi wasemwe kwa ukali
 
Badilikeni. Baada ya mimi kutoa uzi wa kuzinguana na mke wangu, kuna dada alinifuata PM kwamba ananionea huruma sana kwa hali ninayopitia.

Tukazoeana zoeana baadae akasema ninamvutia kwa ile profile picture yangu ya WhatsApp kwa hiyo kama vipi niwe naye, nikaona poa tu, aisee

Demu anapiga mizinga kichizi. Halafu akiomba vocha, ukimtumia voda ya buku 2 anakutukana, eti mi unanionaje? Mimi vocha ya buku 2 ya nini.
Mbombo ngafu😁😁
 
I'm just 41. Nilianza biashara nikiwa ni ngali mdogo. Nimesha kuwa na dogs farm, nimefuga hadi nyuma sumu nikawa nauza nje hadi pale Corona ilipo strike.

Sasa nalima ufuta
Niandalie ekarii kadhaa nije tulime ufuta
 
hivi jf kuna wanawake pia kumbe!!!!
hapa ndo napochoka, mtu unatongoza id aisee wana roho ngumuu au hua kuna meetings watu wanathaminisha?

kweli JF utapata ulichoijia, sasa ulimfata pm mwenywe unalalamika nn kupigwa kizinga? malipo ya shobo hayo af unakuta unatumia dume sasa
 
Huwa najiulizaga,,hivi hao wanaoomba pesa kama walemavu hawafanyikazi?
Kumbuka mmeumbwa kupewa, ila sasa isiwe too much, omba kwa wastani tena kwenye ishu serious.

Ila hizi za kwenda kusuka, mara kutengeneza nywele huwa naona ni kero kwa kweli.
 
Kumbuka mmeumbwa kupewa, ila sasa isiwe too much, omba kwa wastani tena kwenye ishu serious.

Ila hizi za kwenda kusuka, mara kutengeneza nywele huwa naona ni kero kwa kweli.
Ukiombwa milioni tano au kumi utatoa?

Nanyie muwe mnajiongeza sio mpka uombwe
 
Jana wana JF kadhaa wenye club yetu fulani hivi amazing tulikuwa tumekutana The Wine Coutry kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2023.

Wanawake tulikuwa wawili tu, mimi na bidada mwingine na wanaume idadi yao ilikuwa kumi na kitu.

Jamani miongoni mwa mambo ambayo wanaume wanayaona ni kero ni swala la kupiga mizinga.

Wanawake tena mmetajwa kwa majina ambao mnashinda inbox mki zingalaizi. Mara mama anaumwa, mara dada kagongwa na bodaboda, mara nitumie hela ya kusuka nywele mara sina ada ya watoto.

Jamani kwa kweli mnahoyafanya huko PM aibu nimeona mimi. Ukitongozwa ndio usiseme. Hata kama una kazi ya ajira, tena mwajiriwa wa serikali, unaomba kuanzia vocha hadi hela ya chupi.

Wewe uko Dodoma mwanaume yuko Dar hajawahi hata kukulala zaidi ya kuonana mara moja na tena ulikuwa kwenye siku zako.

Nimekutaja wewe dada wa Dodoma sababu umekuwa na tabia ya kuwatongoza wanaume na baadae unaanza kuwa kero kwao na mizinga unayowapiga.

Jamani nawakaribisha Lindi tulime ufuta mbona kilimo poa tu, unapata hela ya kukukimu na huadhiriki.

2023 tubadilikeni jamani
hahahahaha,dah
 
Back
Top Bottom