Wadada wa Dar na Visigino vyao

Wadada wa Dar na Visigino vyao

Mambo zenu jamani.

Nimeona tukumbushane tu madiva wa Dslam kuhusu Visigino vyetu jamani.Sio Siri Dar panaongoza wadada kuwa na miguu michafu yaani Hadi unashangaa huyu katoka kwenye vanga wapi?hii yote Ni Sababu ya kusingizia joto na kuendekeza hivi visendo vya kichina .Yaani mtu muda wote hana usafi,unakutana na dada mzuri kavaa nguo yake nzuri ukimuangalia chini anakukata stimu kabisa
Jamani hebu tusugueni hivyo Visigino yaani mtu kisigino hakieleweki,cheusi utasema alikuwa anasigina masizi🙄!Huyu mchina asitudanganye na slipper zake,na vile Sasa katoa hizo kopi za Tommy Hilfiger Basi yamefika wa wadada wa Dar es salaam,hebu tuwe tunavaa na viatu siku moja moja tutunze miguu hiyo.Hivi mbona Mbeya na Arusha wasafi tu wenzetu.

Unaajita Diva na kisigino kichafu wapi na wapi!Tubadilike
Na makwapa pia muyaweke safi wengine tunapenda kulapamba kwapa
 
Naomba dear loc ya kuipataaa, hiyo heavy niliwahi kuwa nayoo ila imeisha km mwezi m1, now navaa socks tyuuh.

Kila nikitafuta siipati. Plz kwa Dar napata wapi.

Nauza dear
Location
Kariakoo mafia na Jangwani
0655-155782
 
Kuna sehemu nilienda kuangalia mgonjwa. Kulikwa na sitting room za kiarabu (za kuaa chini, kuegemea mito). Aliingia binti mmoja mrembo hasa. Ila alipokuja kukaa na kunyoosha miguu ule uvundo uliotoka hapo ni Mungu tu ndio anajua. Haikujalisha kulikuwa na a/c na harufu ya oud.

Huyo ni mfano tu mmoja lakini wape kina dada wengi hasa wanaoshinda na viatu vya kufunika siku nzima huwa wananuka miguu mno.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna Mmoja alikuja Kwangu kwa Shughuli Maalum kumbe Miguuni alikuwa na Magaga na Kunichania Shuka langu Zuri la Urithi. Nilikereka mno.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naomba dear loc ya kuipataaa, hiyo heavy niliwahi kuwa nayoo ila imeisha km mwezi m1, now navaa socks tyuuh.

Kila nikitafuta siipati. Plz kwa Dar napata wapi.
Wakunyumba kumbe na wewe hupendi mguu mchafu au sio?
 
Back
Top Bottom