Wadada wa kazi tendeeni watoto wa wenzenu kama wa kwenu hata kama leo huna mtoto

howardlite

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2016
Posts
242
Reaction score
392
Wazazi na walezi wenye watoto hiki kinawahusu,baadhi ya wadada wanaotusaidia kazi nyumbani(house girls) wamekuwa na tabia za kufukuza bila kusubiri mwezi uishe kwa namna inavyo kera.

Nilikuja kukagua shughuli za mradi Geita,baada ya kumaliza siku tatu nikampigia simu rafiki yangu anayeishi nyuma kidogo ya Geita karibu na shule ya Wajas Secondary,akaniomba nisiondoke nipite kupaona wanapoishi then nisafiri.
Nikaona ni kweli tunaishi kama ndugu akanipa ramani nilipo karibia akaja kunipokea.

Nikiwa ndio nimefika dada mmoja ambaye baadae nilijua ni mdogo wa mke wake alitoa nguo nje kufua na sehemu ya nguo zilikuwa za watoto wa rafiki yangu,alikuwa na watoto wa kike na wa kiume wawili mmoja ana mwezi tangu azaliwe.

Ghafla yule dada akabaki anashangaa kwa taharuki akiwa na nguo mkononi,sisi wote wawili tukaelewa kuna kitu hakiko sawa.
Tukasogea alipo kujua ni nini, na yule rafiki yangu akamuita jina lake ni nini?Hakujibu badala yake tukawa tumefika karibu yake zaidi na kuona mkononi akiwa na nguo ya binti wa rafiki yangu ikiwa na damu.
Nafikiri unaweza kuelewa mawazo yanavyokuwa,baba akauliza hii si ni damu?
Mama mwenye nyumba akatoka ndani na binti wa kazi wakaja wote nje,jamani kurudi tena ndani zikakutwa nguo nyingine kwenye tenga zimewekwa chini na juu ziko nguo za dada wa kazi na harufu mbaya kwenye kile chumba anachokaa dada wa kazi.
Baada ya kumuliza dada alikiri kutumia nguo za watoto kama pads (pedi).
Mama wa mji akamuuliza sinilikuuliza umevunja ungo ukasema ndio,unatumia nini kujisitiri ukasema pedi na nikakwambia ukiona dalili niambie imekuwaje unafanyia watoto ukatili wa aina hii?Uliniambia nisikupe pedi?Hali ikawa hivyo na makofi juu, mwisho wakasema lazima uondoke inaonekana ni tabia yako ya siku nyingi,dada akasema ni mara ya kwanza na ndio imeanza na kunishtukizia ikaonekana ni muongo wakawasiliana na ndugu zake wakamrudisha kwao.
 
Waajiri wa Watoto wa Kazi: Watendeeni Watoto wa Kazi Kama Mnavyowatendea Watoto Wenu Hata Kama kwa Sasa Hawana Mbele Wala Nyuma
Ni kweli mkuu vice versa is true, ndio maana nimesema baadhi,wapo tena sio haba wabos wanavyowatendea wadada wa kazi ni unyama bila kuja what goes around comes around na tunavuna tunachokipanda.
Kuna stori za dada zetu walitendea vibaya na waajiri wao mmoja alichoka akamuweka mtoto mdogo kwenye frizer alikuja kukutwa ameganda.Mwingine alikuwa muathirika maskini akawapigisha mswaki wake watoto wote wa ile familia mmoja tu ndio alipona na maambukizi.
Ni somo kubwa na pana lenye tahadhari na Mwenyezi Mungu kuwasaidia kuishi kama ndugu na kwa upendo pande zote mbili bila kuacha mambo ya Ibada.
 
Jaman inasikitisha kwakweli , Hakawii Kuchambia jagi la maji ya kunywa huyo.Aende tu.
 
Lakini kitu kimoja mnasahau, Kuna wamama wanawatreat Hawa wadada so harsh, lugha ya mawasiliano inayotumika Kila haiko polite, hakuna ubinadamu kabisa kwenye a lot of treatments, hebu hii part nayo iangaliwe, Kuna nyumba ukiingia kukiwa na wadada watatu wako mbele Yako, househelper unaweza kumtambia kutokana na mavazi yake na nywele zake zilivyo na jinsi anavyokuwa treated na members of the family hasa wenye jinsia ya ke.

Watu wabadilike pia. Ni kweli househelpers wengine ni Vimeo lakini wengine ni visasi vya yale wanayotendewa na waajiri wao.
 
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…