Wadada wenye maumbo mazuri kwa asilimia kubwa wakikutana na mwanaume huhisi kutongozwa tu

Wadada wenye maumbo mazuri kwa asilimia kubwa wakikutana na mwanaume huhisi kutongozwa tu

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Kuna siku nilitembelea benki fulani, kwa ajili ya kupata utaratibu wa kupata mkopo kwa ajili ya biashara yangu. Kwa bahati nzuri nilipokelewa na mdada, ni mzuri na anashepu ya kuvutia, nyuma amejaziwa kweli. Akanihudumia, na akanipatia namba yake kwa ajili ya kufuatilia.

Cha ajabu, nilipokuwa nampigia simu inaweza kuita muda mrefu bila kupokelewa, na akipokea anaongea kwa mapozi kama vile nataka kumtongoza. Nikawa najiuliza, namba anipe mwenyewe kwa ajili ya mawasiliano ya kiofisi, sasa inakuwaje analeta manjonjo kwenye mawasiliano?

Nikahisi, inawezekana labda kutokana na alivyoumbika anahisi kila mwanaume anataka kula tunda kimasihara.

Nilivyofanikisha mzigo wangu, ikabidi nifute na namba yake.
 
Back
Top Bottom