Wadau mimba ya tarehe 17 mwezi wa 12 mtoto anazaliwa lini?

Wadau mimba ya tarehe 17 mwezi wa 12 mtoto anazaliwa lini?

Tarehe 17 mwezi wa 12 ndio siku ya kukutana na mwanaume, ila mpaka sasa hivi hajazaa yuko timamu au ni kawaida.

NB-habari ya kliniki sizijui kwahyo usiniulizee
Hapa ili kujua tarehe ya matazamio (EDD) kinachohitajika ni tarehe ya mwisho ya mama kuona siku zake (LNMP). Kuna formula ya kukokotoa hiyo tarehe.

Kama mama hakumbuki tarehe ya mwisho ya siku zake basi vipimo vingine hutumika kukadiria umri wa mimba mfano ultrasound ambayo pia hutumika kuangalia hali ya mtoto tumboni.

Baada ya kujua tarehe ya matazamio (EDD) basi kuna mambo matatu kuhusu mama kujifungua:

1. Anaweza akajifungua siku ya hiyo hiyo tarehe mfano kama EDD ni 16/09/2024.

2. Anaweza akajifungua wiki mbili kabla ya hiyo tarehe mfano kama EDD ni 16/09/2024 unakuta anajifungua tarehe 02/09/2024. Au tarehe yoyote katikati ya 02/09/2024 na 16/09/2024

3. Anaweza akajifungua wiki mbili baada ya hiyo tarehe mfano kama EDD ni 16/09/2024 anaweza akajifungua tarehe 30/09/2024. Au tarehe yoyote katikati ya 16/09/2024 na 30/09/2024

Pia kama EDD imekaribia au imepita mama awe anasikia mtoto akicheza tumboni wakati anasubiri uchungu kuanza. Kama wiki mbili zimepita toka tarehe ya matazamio (EDD) na uchungu haujaanza aende hospital kuonana na mtaalamu.
 
Umwpigwa. Inamaana amezaliwa na miezi 8 mtoto wa miezi 8 kupona Ni Nadra labda 7
Kuna mmoja nilkutana nae TAREHE 17/ 12/2023 na mpaka Sasa ameishajifungua na mtoto amefikisha 40 tayari nadhani nitakuwa nilipigwa Kwa kawaida mtoto angekuwa Bado hajazaliwa, akaamua kuniletea mauzauza kibao eti mtoto alizaliwa njiti na kilo 2.6 , kuuliza Kwa wataalamu wakanimbia huyo mtoto kazaliwa akiwa ametimiza MIEZI 9 huyo, baada ya majibizano mengi huyo mwanamke ameamua kukaa kimya ila nilishalipia badhi ya bill , nilivyoona anazidi kutaka Hela Kila siku nkaanza kuhoji kuhusu uhalali wa mtoto , ndio kanikaushia Sasa hivi , Hawa wanawake jamani acheni kutubambikia watoto
 
hio picha iliwahi kunitokea ila nilimsaidia kama mtu nimjuaye tu..kalenda hazikai swa hata kujaribu kusema tena ni wangu kashindwa baada ya kuzaliwa...ndugu zake tu ndio wanamleta eti kafanana nawe kaja hapa katulia ana amani....nikimchekiiiii nasema hiii...
 
Raha za muda mfupi zinaenda kumbebesha majukumu hakujipanga nayo...na labda majukumu yenyewe sio yake,kabambikiwa
Itakuwa ni manzi yake ya muda.
Kutumia rubber kwa partner ni by chance tu.
 
Itakuwa ni manzi yake ya muda.
Kutumia rubber kwa partner ni by chance tu.
 
Back
Top Bottom