Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣niliwahi kushikwa na hali hii na sio nilikula chakula cha kuvimbiwa.Hapa sina amani kabisa wala furaha kuanzia mida ya saa 3 baada ya kula. Nahemea juu juu huku macho yamenitoka kama mtu aliyeshikwa ugoni....hata kumeza mate tu nashindwa hali inazidi kuwa ya hatari sana kwangu.
Nimekula nyama choma,mishkaki,sausage na mtura. Hivyo vyote toka mchana leo nlikuwa nakula na ndizi za kuchoma. NIMEVIMBIWA NDUGU ZANGUNI. NIMEVIMBIWA SANA.
Naombeni msaada maana nipo mbali na maduka ya dawa. Ni mbali kiasi kikubwa. Lakini pia nichukue nafasi hii kuwaomba msamaha wote nliowakosea. Kama kuna sehemu tumepishana nikasema maneno yenye ukakasi basi mjue tu ni ubinadamu.yaishe please.
Mwili unanitetemeka na jasho linanitoka kwa wingi. Nimeishiwa nguvu na tumboni kuna nguruma sana. Nimejaribu kutapika tumetoka tuvipande twa nyama na sausages kama tulivyo kama vile vimelowekwa tu kwenye maji baada ya kupikwa.
Yaani napata shida wadau, siwezi hata kulala maana tumbo limejaa sana. Nimejawa na mawazo nini hatima ya hili tatizo usiku huu wa leo. Maana naumia sana.
Kuna dawa gani ya asili naweza pata kwa haraka ndani ya nyumba? Nisaidieni wandugu tuweke tofauti zetu kando tafadhali. Shingo,mabega na kichwa vimekosa nguvu kabisa na kupigwa ganzi. Nasikia nzeeeeeeeeeeeeeeee......sielewi wadau. Sielewi. Hapa nina masaa mawili nimekaa tu chooni haja haitoki kabisa.
Cha ajabu nilikula karanga chache na soda.
Nilikwamwa na kitu shingoni.
Nilikinywa maji halishuki.
Nilijaribu kukimbia wapi.
Naona nazidi kukabwa na tumbo limejaa.
Kuna mdau akanishauri niloweke majivu nisubirie yatuli na ninywe maji yake.
Kweli nikatii.
Baada ya kunywa hayo maji yake ndani ya dakika 15.
Kilichokwama kikapotea na tumbo likawa shwari lkn nilitokwa na vipele mwili mzima nilijikuna balaaa lkn nikapona mazima