Wadau, msaada haraka hali hii inatesa sana muda huu

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣niliwahi kushikwa na hali hii na sio nilikula chakula cha kuvimbiwa.
Cha ajabu nilikula karanga chache na soda.
Nilikwamwa na kitu shingoni.

Nilikinywa maji halishuki.

Nilijaribu kukimbia wapi.
Naona nazidi kukabwa na tumbo limejaa.

Kuna mdau akanishauri niloweke majivu nisubirie yatuli na ninywe maji yake.

Kweli nikatii.
Baada ya kunywa hayo maji yake ndani ya dakika 15.
Kilichokwama kikapotea na tumbo likawa shwari lkn nilitokwa na vipele mwili mzima nilijikuna balaaa lkn nikapona mazima
 
Pole utapona. Lakin Kuna watu wanaamini uchawi jaman yaan mtu Kasema kabsa sababu lakn bado hawaamini, umeshakuwa mtu mzima maana yake unajitambua lazma ujue saiz yako ya chakula hakuna raha yoyote ukishavimbewa, kula kias acha na nafas ya matunda au kinywaji sio unakula mpaka unakosa amani na unashindwa hata kufanya jambo lingine.
 
Sijui nguvu za ku type risala hii ulizipata wapi?
 
Ni majivu yoyote?

Kuna siku nilikua na kiungulia nikashauriwa kutumia majivu kwa kuyalamba. Basi nikachukua majivu kwenye jiko la mkaa kwa chini kule nikayatia kiganjani nikaanza kulamba.

Dakika 5 nyingi ulimi ukaanza kuuma sana kama vile nimeungua! Wakati nilihakikisha kabisa jiko la mkaa lilikua halijatumika zaidi ya wiki. Aisee niliumwa mno zaidi ya siku 3 au 4 sikuweza kula kwa raha ulimi ulikua unawaka moto. Mpaka leo sijajua ni nini kilitokea japo utafiti wangu unaonyesha kuna baadhi ya miti majivu yake ni sumu na yanaweza kuleta madhara.
 
Ka
Kabisa kabis kabisa ni bora ukajua ni mti upi umechoma ukapata majivu
 
Mwanadamu buana, akishiba tabu na akiwa na njaa tabu pia...
 
Menya vitunguu swaumu 6, kisha vikate Kate then meza na maji , kama unakunywa kama dawa.

Au ndizi mbovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…