Wadau na wajasiriamali, naomba kujuzwa kuhusu Mr. Kuku Farms na uhalisia wa aina ile ya biashara

Wadau na wajasiriamali, naomba kujuzwa kuhusu Mr. Kuku Farms na uhalisia wa aina ile ya biashara

Sikia watoto wa mjini ikitokea mishe kama hii huwa wanajiunga ikiwa bado mbichiii ikiwa bado mpya wakati huo wanajaribubkuaminisha watu kwamba ni real so wana act real mipungabnjenje wanamwagabpesa balaa ili nyie muite wengine kwa ushuuda etcetc sasa basi ukishaona watu washakuwa wengiiii na watu kibao wanajiunga ujue wanakaribia kusepa so mm kama mshikaji wako nakwambiaje umeshachelewa miaka mitatu yote iliopita ulipaswa uwe umeshaingia saiv bomu linakaribia kuripuka mda sio mrefuu watasepa na kijiji cha watu wanasubiria tu mazuzu yajaee

Sent using Jamii Forums mobile app
Babu niko na maseke kinoma. Siez jiunga now. Nahisi watu watafyatuliwa soon 😂😂😂
 
HAWA WATU KAMWE HAWATAKUJA KUISHA MAADAM KUNA SOKO KUBWA, SOKO LA WATU WENYE KIU YA HIARI YA KUTAPELIWA.NAAM MATAPELI WATAKUJA KWA NJIA NYINGI NA NYINGINEZO ZINAONEKANA NI HALALI HIVI. ENZI ZA DECI WATU WALIKUWA WANAANZA NA MAOMBI NA KUMKEMEA SHETANI!!

WALIANZA DECI, NAMAINGO, HATA VYAMA VYA KUWEKA NA KUKOPA BADO WATU WANATAPELIWA, NDIO HAWA SASA. JE UNA NYOTA YA KUTAPELIWA? BASI JIUNGE NAO.

There are no shortcuts to success.........
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 sista angu alipigwa huko Deci
 
Kwanini usimpe hela akafuga hapo nyumbani, na Uzuri wa Dar soko lipo
Utawaweza hawa wazazi wetu?nilimpa hela awamu ya kwanza.alijenga mabanda akanunua na vifaa kutahamaki hela imeisha.hapo hakuna kilichoendelea.awamu ya pili nikatuma tena hela akaiweka vifaranga 600.mabanda matatu@vifaranga 200.na walipishana wiki tatu.nusura wamuue kwa presha.bado akang'ang'ania tuu na kuku.hii safari kaja na habari ya kuku bila kufuga.namuangalia tu maana ukijikausha anaanza kusemasema vimaneno vya kukera. NA unajua wazazi wetu hakuna namna nitamwambia anisikie.naamua kuacha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekumbuka ,,,Bunge la Uchumi,,,,Kijani kibichi NK...ukiona waitiwa fursa tambua fursa ni wewe mwenyewe
 
Utawaweza hawa wazazi wetu?nilimpa hela awamu ya kwanza.alijenga mabanda akanunua na vifaa kutahamaki hela imeisha.hapo hakuna kilichoendelea.awamu ya pili nikatuma tena hela akaiweka vifaranga 600.mabanda matatu@vifaranga 200.na walipishana wiki tatu.nusura wamuue kwa presha.bado akang'ang'ania tuu na kuku.hii safari kaja na habari ya kuku bila kufuga.namuangalia tu maana ukijikausha anaanza kusemasema vimaneno vya kukera. NA unajua wazazi wetu hakuna namna nitamwambia anisikie.naamua kuacha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi mwaka jana kidogo kuku waniue kwa presha walikufa karibu wote nilikaa sana bila kuku, kwa hiyo kila biashara ina Changamoto zake
 
Juzi kuna jamaa yangu kanipigia simu akawa ananieleza vitu sivielewi elewi.

Ni kitu kinaitwa Mr. Kuku Farms akidai ni mradi mkubwa wa ufugaji kuku una physical presence na ni kampuni iliosajiliwa ndio inaendesha huo mradi.

Yeye ameshawishika kuwekeza huko kwamba kuna faida nzuri compared na kuweka hela benki tu ikiwa baada ya miezi 3 unaweza draw 70% ya ulichowekeza na baada ya miezi sita una uwezo wa kuchota 100% ya pesa yako.

Kama tujuavyo kwamba mtu alieng'atwa na nyoka huwa haishi maseke hata anapotambaliwa na jani, basi lazma atarusha miguu tu.

Naomba kwa heshima na taadhima niambiwe na wadau wenzangu wajasiriamali kwa wafanyabiashara. Je, huu mradi ni halisi?

Ni business model gani wanatumia? Na je, kuna hiyo leverage ya kupelekea kutoa gawio kwa rates hizo kwa muda wanaodai wanaweza?

Kama kuna ambaye amepiga hela kupitia hao jamaa aje amwage terms zao na ushuhuda kuwa kapiga dough kweli.
Another DECi, D9. Mr. Kuku Wizi huu.
 
Unafikiri wa mwanzo walifaidi? Shida ya pesa ni kila ukipata ndo unaongeza mtaji ili safari ijayo upate zaidi,Sasa utajikuta ulianza kuweka laki,ukipokea unaongeza laki na nusu,hivyo hivyo mpaka mwisho wa siku unajikuta unaibiwa laki tano
Deci kiukweli kabisa wale wa mwanzo ndio waliifaidi watu wa mwishoni ndio waliishia kupigwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hawa jamaa niliwekeza nikapiga hela yangu ila sijarudia tena. Uzoefu wangu najua aina hizi ya fursa zikikolea ndiyo muelekeo wa kupigwa. Nashukuru kupitia hawa jamaa niliposhika mshiko fasta nikanunua plot.

Hizi mambo wanalia wengi sio wabongo tu. Hata Kenya na Uganda hizi ponzi scheme zinakula sana vichwa ya watu. Waafrika wengi tunapenda hela rahisi situation ni tofauti kwa West Africans janja sana wale.
 
Juzi kuna jamaa yangu kanipigia simu akawa ananieleza vitu sivielewi elewi.

Ni kitu kinaitwa Mr. Kuku Farms akidai ni mradi mkubwa wa ufugaji kuku una physical presence na ni kampuni iliosajiliwa ndio inaendesha huo mradi.

Yeye ameshawishika kuwekeza huko kwamba kuna faida nzuri compared na kuweka hela benki tu ikiwa baada ya miezi 3 unaweza draw 70% ya ulichowekeza na baada ya miezi sita una uwezo wa kuchota 100% ya pesa yako.

Kama tujuavyo kwamba mtu alieng'atwa na nyoka huwa haishi maseke hata anapotambaliwa na jani, basi lazma atarusha miguu tu.

Naomba kwa heshima na taadhima niambiwe na wadau wenzangu wajasiriamali kwa wafanyabiashara. Je, huu mradi ni halisi?

Ni business model gani wanatumia? Na je, kuna hiyo leverage ya kupelekea kutoa gawio kwa rates hizo kwa muda wanaodai wanaweza?

Kama kuna ambaye amepiga hela kupitia hao jamaa aje amwage terms zao na ushuhuda kuwa kapiga dough kweli.
Huhitaji akili kubwa kujua kwamba hii ni deci mpya.
Siku zote watakuwepo wapumbavu wa kudanganya.
Hizo bidhaa zake za kuku anauza Dunia ipi?
Kawazidi nini wafugaji wetu wa mitaani?

Kuna watu wanahangaika hilo soko liko wapi. Akishakusanya za kutosha atapotea tu
 
Wajinga ndo waliwao. Nakumbuka tulivyotapeliwa forex na Pimbi
Usiseme pimbi 😄😄😄,,,Sema mnyamakazi "ONTAFEX" aka "ONTARIO" kijana machachari kabisa aliekuja na hekaya zake za kumiliki mashamba makubwa na ndoto kubwa za kimaisha dunia nzima.

Akawahadaa na Motivational speaking talent alionayo na kuteka hisia za wana JF "Wanyonge" na kuweza kuwapiga 130K zenu kwa ukali na Program yake darasa la forex nchi nzima akiwa na genge la matapeli wenzie wa kikaburu, kumbe anawanyawisha na signal za kununua yani 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom