Wadau na wajasiriamali, naomba kujuzwa kuhusu Mr. Kuku Farms na uhalisia wa aina ile ya biashara

Wadau na wajasiriamali, naomba kujuzwa kuhusu Mr. Kuku Farms na uhalisia wa aina ile ya biashara

Watu ebu muwe na mawazo chanya au hoja za msingi, ... tuanzie hapa. Biashara ya ufugaji na kilimo ni biashara nzuri ila zina risk kwny production na sio asset so hao wamewekeza kwny miundombinu ya kufanya huo mladi kwa maana ya vifaa mashamba na wafanyakazi so kinachotokea ni ww unatoa hela yako wanakuuzia vifaranga wanavyozalisha wenyewe na wanavifuga wenyewe apo apo kwao then vikikua wao watauza kuku wakishirikiana na ww ila mtagawana faida. Wao watafaidika katika kukuuzia vifaranga, kukuuzia chakula cha kukuza hao kuku ad wanakua na mwshon wanafaidika ktk faida ya mauzo ya kuku so apo ww unaokolewa gharama za kua na eneo na kujenga mabanda na kulipa wafanyakazi. Instort bajet yako ndio ndio ina cover idadi ya vifaranga na chakula chao ad wakikua na kuuzika


Sent from my iPhone using JamiiForums
.
Screenshot_20200328-122235.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimewaona instagram lakini nilivyoona WAMEFUNGA COMMENT.
nikajua hawa ni matapeli.
kuku hawajawahi kulipa kiasi hicho.
Hawa jamaa sijui wanapataje faida

Wanadai wanatoa 70% baada ya 4 month's, Halafu ukisubiri tena baada ya miezi 6 unapata 100% kama profit

Ukijumlisha hapo ni 170% faida kwa miezi 10 hiki ni kiasi kikubwa sana cha faida ukilinganisha na biashara yenyewe tena ya ufugaji kuku + Muda wa investment

Yaani mfano niwekeze million 10 ndani ya muda wa miezi 4 nitakuwa na million 17 nikiacha tena hiyo million 17 baada ya miezi 6 nitakuwa ninetengeneza million 34

Pia Instagram kule watu wanalalamika kuwa wana hide comment za baadhi ya watu, inaonekana kuna jambo hawataki kuliweka wazi.

Pia kwa experience yangu kwenye mambo kama haya wanaofaidika ni wale wanaowekeza mapema sana sana yaani sana kabla mambo hayajaharibika, ule muda ambao kampuni haijatengeneza faida kubwa ianze janja janja, ule muda kampuni inahangaika kutafuta watu unakuta wajanja wamewekeza wanakula faida.

Mpaka sasa Mr kuku ina miaka 3 na ukiangalia vizuri bado hawajapata faida kubwa ya kusema wakimbie ndio wako katika harakati za kupanua kampuni hii ni wazi kwamba wale waliowekeza miaka 2 nyuma bado wanapiga profit inaweza kuwachukua miaka 4 mbele mpaka kampuni kufirisika unaweza kuona jinsi gani profit watakayo tengeneza waliowahi kuiona fursa

Ukiona watu wamejaa sana ujue puto limejaa upepo linakaribia kupasuka huo muda ndio nyumbu unakuta wamejazana balaa wajanja wameshajitoa hapo ndio unasikia mara kampuni imefirisika wajanja wamekimbia na pesa.

Pia kwa wale watakao enda kuwekeza nawashauri someni mikataba vizuri maana wabongo wengi hawapendi kusoma pengine wengine hawajui umuhimu wa mikataba. Kunauwezekani mkubwa mikataba yao imejaa uhuni sana wa kulinda kampuni yao.










Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuku tunafuga huku miaka na miaka hao kuku wao wanauza wapi asee ha ha ha hapo watawapata wasiowahi kufugA kuku tu..

Aliye wahi kufuga kuku hawezi peleka hela yake huko
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kuna ma Motivator wanasema "Work smart. Not Hard!" nadhani muelekeo uko huku kwa sasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hunajua haya maswala yamenifungua akili na kuona kumbe kuna uwezekano ukabuni mradi worth a million of bucks na ukafanya fund raising kwa kigezo cha "wekeza uvune faida mara mbili"

Thats very possible...Nadhani kwa kutumia mwamvuli wa Mwanasheria tunaweza buni kitu aisee. Tukabuni mradi wenye loopholes za sisi kuchomoka hata ikibidi kwa kusingizia Bima flani au vipengele vya mkataba then unaenda launch kitu. There are alot of lazy guys with money that can easily be fetched through proper plans.
 
Dah umeshusha points mkuu sio mchezo
Watu bana, yaani jambo linaonekana tu kwa macho ya kawaida kua hii ni Ponzi Scheme au Pyramid Scheme mtu bado unajiuliza maswali mara mbili mbili?

Hao wenye hiyo kuku farm kwa nini wasiuze kila walichonacho na wawashawishi ndugu zao wauze kila walichonacho wawekeze kwenye hiyo project wapige hela wawe familia tajiri zaidi? Au unadhani hao jamaa wa kuku farm wanawapenda sana kuliko wanavyowapenda ndugu zao? Kwamba waone fursa wasiwaambie ndugu zao waje kuwambia nyie? Uliwahi kuona wapi?

Kila siku humu tunatahadharisha kua ukiona unaitwa kwenye deal ujue wewe ndie deal, ukiona unaitwa kwenye fursa ujue wewe ndie fursa. Wazungu husema when the deal is too good think twice. Hakuna hela inapatikana kwa haraka hivyo.

Ilikuja D9, Deci, Qnet, One coin, sijui vitu gani watu wanapigwa kila siku lakini hawajifunzi.

Hao wa kuku farm wape muda mfupi utaona mada zao humu, ni jambo la muda tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom