Business as usual. It seems there is a systemic abuse of police power mkoa wa Simiyu.
Less than 2 weeks ago askari wa huo huo mkoa wa Simiyu, makao makuu yao Bariadi, waligeuza simple traffic offence - fender bender ya parking - kuwa kipigo kizito, wakanijeruhi, mixer kunikalia kooni nilipotaka kusimama ili tuendelee na mazungumzo. Mwishowe waliniweka ndani, na ilitumika backup ya mwenyeji wangu, mtu mzito hapo wilayani ili mimi kutoka.
Nakumbuka vizuri askari aliyekuwa mstari wa mbele kunipiga kesho yake aliniambia "yani wewe una bahati, sisi huwa tunapiga sana bro"
Nilieleza kituoni kwa mkubwa wao kuwa tukio zima limerekodiwa video na sauti kwenye dashcam za gari yangu, kama wakitaka tu open up evidence. Niliachiwa bila masharti, nikabaki na majeraha yangu. Jicho, mdomo, shingo, na visigino vya miguu yote miwili. Mguu wa kushoto ulipata 'pitting edema', and As I write this, bado unatoa usaha na damu kwa mbali.
Sishangai askari hao hao kumuua huyu kijana, kwani kwa maneno yao ni fahari wao kupiga watu pale wanapojiskia.
Twisting ya maneno niliyoishuhudia pale, sidhani kama nitakuja kuamini lolote askari wanalosema.