Wadau wapendekeza Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6

Wadau wapendekeza Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6

Hii hatua sijui itasaidia vipi kukuza elimu yetu ikiwa baadhi ya hao wanaomaliza darasa la saba huwa hawajui kusoma na kuandika, hapa naona ni kama vile kuwahisha wajinga kumaliza shule.

Naona itakuwa na nafuu kwa shule za mijini na zile english medium, lakini kwa zile shule za vijijini kazi ipo.
 
What is the Advantage of this education system compared over the current one we have.
Lots and lots of advantage!,
  1. Kwanza Tanzania tunaingia kwenye mapinduzi ya Elimu, hakuna tena daasa 7, bacic education inakuwa ni elimu ya form 4!.
  2. Watoto wanaanza shule wadogo na kufundishwa kujitambua mapema, samaki mkunje angali mbichi. Darasa la kwanza ni akiwa miaka 6 na kumaliza primary at 12!.
  3. Hakuna mimba za utotoni kwa primary school, hivyo sasa watapevukia sekondari na somo la sex education ndio somo la kwanza sekondari.
  4. Mtoto akiwa primary anapimwa amplitude tests za kuangalia brain ppwer yake kipaji chake anaweza nini na sio tuu anapenda nini, anapendeshwa kile anachoweza na hii itapunguza sana watu kutaga!.
  5. Specialization inaanzia form I. Hivyo wanafunzi tangu anasoma sekondari anajua anakwenda kuwa nani, sio mtu anauwezo na sheria, halafu kwenye HDD yake umzamishie Abbot na Nelkon na kujaza bure savers zake na kumpotea muda
By the way:
Pascal Leo tuongee kirafiki maana huwa nakubomu Sana.
1. Unaonaje video clips za Ansbert Ngurumo, zinaonesha weledi wa uhandishi wa habari of the highest caliber ever au Ni sawa na makala zako?
Japo wote ni waandishi wa habari, mimi ni broadcast journalist ambaye sasa naandika, yeye ni print journalist ambaye sasa anajaribu kutangaza. Huyu ni mmoja wa waandishi vichwa kwenye tasnia ila ana tatizo moja tuu, ana impaired vision ya light kwa kuona one sided only, jicho lake linaona only the dark side, lakini halioni the bright side, hivyo anaona mabaya tuu!, haoni jema lolote. Mimi nina ona both sides, the bright side and the dark.
2. Unampa credit gani kwa maswali yake magumu? (Maswali magumu)
Nampaga credits sana na kuna group la wahariri niko nae, alitimuliwa mimi ndio nikamuombea msamaha akarudishwa.

Hata humu jf, namfagilia sana tuu Ansbert Ngurumo awamwagia Pongezi za ushindi kwa Makamanda wa CHADEMA!

Angalia hii Taifa linahangaika na wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu! Je, ni hawa?! Mhe. Mwigulu, IGP, anzieni hapa!
Na hapa Fungia Fungia Magazeti: Ni Udikteta wa Serikali Magufuli, yalaaniwa na yasulubiwa - Jicho Letu Ndani ya Habari
P
 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amesema kuwa katika sera mpya inayotarajiwa kuzinduliwa hapo baadaye elimu ya msingi itakomea darasa la 6.

Kauli hiyo ameisema hii leo Oktoba 20, 2022, na kuongeza kwamba sera mpya ya elimu itakapozinduliwa hakutakuwa na mtihani wa mwisho wa elimu ya msingi na kwamba mtihani utakuwa ni wa kidato cha nne tu, huku akisema mwanafunzi akianza kidato cha kwanza atakuwa tayari ameshajiweka kwenye mchepuo maalum hadi kidato cha nne.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga amesema kuwa serikali inatazamia kuzindua sera mpya ya elimu kufikia mwezi Desemba, 2022 ili kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu na kwamba mabadiliko yataanzia elimu ya msingi.

Baada ya Serikali yaridhia Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6, sasa ifute idara ya elimu msingi na kuundwe idara ya elimu ambayo itasimamia elimu ya msingi na ya sekondari​

Mimi nashauri watoto wetu wasisome kabisa.

Tuwape vyeti tu kwa kuwakadiria umri.

Hawa viongozi wetu wanachezea maisha ya watoto wa walala hoi kwakua watoto wao hawaendi hizo shule.

Watoto wa wenzao ndio wa kuwafanyia majaribio.

Mtu ukiwa na uwezo peleka tu mtoto wako nje ya nchi ili kuepukana na hizi drama za matamko ya kila siku mtu akilala akiamka anaibuka na tamko.
 
Hii mimi nadhani hatua nzuri na tumechelewa sana kwa kweli, Baada ya darasa la 6 mwanafunzi anachagua nini cha kusoma hiyo inakuwa ni direction ya chagua anataka kuwa nini mbele ya safari. Hii mitihani ya darasa la saba kuna watoto wanaachwa sio kwamba hawana uwezo kuna watu ni ile pressure na hofu wengine toka family au ndugu lakini wakiwa wame relax anaweza kuchagua anataka kuwa nani sasa huko mbele ya safari ni juhudi zake anaweza au ataishia njiani lakini hakosi elimu kutakuwa na ile kuzidiana tu watajichuja wenyewe mbele ya safari. Kama wa Tanzania tuunge mkono mabadiliko kwa maana hii system haijatupa matokeo chanya ni wakatu wa kubadilika na hata ikibidi mbele ya safari kubadilika kuboresha mapungufu ni sawa tu, hatuwezi kuwa mfumo kwa miaka 50 dunia inabadilika tech imetawala sisi bado tuko darasa la saba tunasoma vita vya maji maji story za kuunga tu.
Watu wangu wanaangamia kwa kukos maarifa,mtoto wa darasa la sita atachagua nini,mnataka kuiua nchi ili wenye nacho waendelee kutamba.
 
Hili swala ni muhimu sana. Fulsa nyingi sana vijana wanapishana nazo kwa sababu ya kutozungumza Lugha ya Kiingereza.
Serikali ikifanikiwa kwenye hili, miaka kumi ijayo vijana wengi watakua wamejiajir kwenye sekta rasmi na zisizo rasmi nyingi.
Tatizo hakuna walimu wa shule za serikali wanaojua kiingereza fasaha mkuu.

Amini hili maana tunawajua vizuri. Somo la kiingereza ukimfuatilia mwanao mfano mwalimu anavyosahihisha kazi ni kituko.
 
Naomba Kujua,Sijaelewa,
Mtoto akishafika Darasa La 6 anakwendaje Form-1?
Sababu Nimesoma Kuwa Hakutakiwa na Mitihani Shule ya Msingi,Kutakuwa tuu na Mtihani wa form 4!
Sasa Mtoto akimaliza Darasa la 6 Watajiunga Vipi na Sekondary,Na Sekondary Maalum Pia?
Then Atafanya Mtihani form 4 na Kwenda Form 5!
Form 4 ndo itakuwa elimu ya msingi kwa kila Mtanzania. Kwa maana yeyote anayefika darasa la 6 ana fursa ya kwenda form one ili akakutane na mtihani wa form four.
 
Hii hatua sijui itasaidia vipi kukuza elimu yetu ikiwa hata hao wanaomaliza darasa la saba huwa hawajui kusoma na kuandika, hapa naona ni kama vile kuwahisha wajinga kumaliza shule.
Tunapoteza badala ya kuboresha yote ni matokeo ya chaguzi za 2019 na 2020,hapo ndiyo matatizo yote haya yalianzia na sijui yatamalizika lini,inasikitisha kwa kweli.
 
Binafsi sitarajii jema katika utaratibu huu mpya. Laiti watoto wa hao wakubwa nao wangesoma katika utaratibu huo, ningejua wana nia njema!
Kwahiyo wewe kupoteza muda mwingi darasani ndo unaona la maana?

Halafu ni shule zote za serikali na binafsi wataishia darasa la 6 kama elimu ya msingi.

Sasa kuna nia gani mbaya hapo?
 
Wazo zuri sana hili na naliunga mkono na mguu

Swali langu ni Je,Hao walimu wa kuendana na haya mabadiliko wameshaandaliwMimo

Tatizo hakuna walimu wa shule za serikali wanaojua kiingereza fasaha mkuu.

Amini hili maana tunawajua vizuri. Somo la kiingereza ukimfuatilia mwanao mfano mwalimu anavyosahihisha kazi ni kituko.
Utafiti unaonyesha asilimia 90 ya walimu wa sekonari hawajui kiingereza vizuri hapa nchini, hivyo Basi, mm naona kiswahili ndio iwe lugha ya kujigunzia na kiingereza mtu ajifunze Kama somo na lugha.
 
Sera hii ni nzuri iwapo itapitishwa, na wangepunguza pia muda wa kuanza darasa la kwanza.

Muhimu kuliko yote isije serikali nyingine ikabadilisha kama ambavyo imekua ikionekana kwenye mambo mengine, leo linapitishwa hili kesho anakuja mwingine kupangua.
 
Hatua nzuri sana kwa sababu ,hataachwa mwanafunzi yeyote yule kwani mtoto mwenye uelewa mdogo ataenda ufundi na mwenye uelewa mkubwa atachugua mwenyewe aende ufundi au aendelee na masomo ya juu.

Tatizo naliona hapo kutoka darasa la sita kwenda ufundi au sekondari bila kufanya mtihani.tunampimaje huyo mtoto Kama ataweza kumudu masomo ya sekondari au ufundi?.

Mtihani ungekuepo tu ili kujiridhisha kwa usahihi uelewa wa mtoto kabla ya kumpeleka mbele
 
Lots and lots of advantage!,
  1. Kwanza Tanzania tunaingia kwenye mapinduzi ya Elimu, hakuna tena daasa 7, bacic education inakuwa ni elimu ya form 4!.
  2. Watoto wanaanza shule wadogo na kufundishwa kujitambua mapema, samaki mkunje angali mbichi. Darasa la kwanza ni akiwa miaka 6 na kumaliza primary at 12!.
  3. Hakuna mimba za utotoni kwa primary school, hivyo sasa watapevukia sekondari na somo la sex education ndio somo la kwanza sekondari.
  4. Mtoto akiwa primary anapimwa amplitude tests za kuangalia brain ppwer yake kipaji chake anaweza nini na sio tuu anapenda nini, anapendeshwa kile anachoweza na hii itapunguza sana watu kutaga!.
  5. Specialization inaanzia form I. Hivyo wanafunzi tangu anasoma sekondari anajua anakwenda kuwa nani, sio mtu anauwezo na sheria, halafu kwenye HDD yake umzamishie Abbot na Nelkon na kujaza bure savers zake na kumpotea muda

Japo wote ni waandishi wa habari, mimi ni broadcast journalist ambaye sasa naandika, yeye ni print journalist ambaye sasa anajaribu kutangaza. Huyu ni mmoja wa waandishi vichwa kwenye tasnia ila ana tatizo moja tuu, ana impaired vision ya light kwa kuona one sided only, jicho lake linaona only the dark side, lakini halioni the bright side, hivyo anaona mabaya tuu!, haoni jema lolote. Mimi nina ona both sides, the bright side and the dark.

Nampaga credits sana na kuna group la wahariri niko nae, alitimuliwa mimi ndio nikamuombea msamaha akarudishwa.

Hata humu jf, namfagilia sana tuu Ansbert Ngurumo awamwagia Pongezi za ushindi kwa Makamanda wa CHADEMA!

Angalia hii Taifa linahangaika na wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu! Je, ni hawa?! Mhe. Mwigulu, IGP, anzieni hapa!
P
Boss uko kinadharia zaidi yaaani maono ambayo asilimia 80% ni ndoto,Kigwendu aliwahi kusema," Mipango si matumizi". Hii nadharia yetu ni hatari sana,sijabahatika kuzunguka duniani ila mifano michache ya elimu kwa majirani zetu Kenya na Zambia,siungi mkono hiyo hoja.
Ukienda Kenya wasomi ni wengi ila ni jobless na useless people,wengi wanazama sana kwenye mambo ya ndoa za jinsia moja na ufuska kwao ni kitu cha kawaida.Ukienda Zambia mtu akifika darasa la 9 anakuwa taabu mtaani kuwa amesoma kumbe ni empty kabisa.Ndiyo maana ukiona hawa majirani zetu baada ya uhuru walitupiga bao sana kwa mambo mengi,lakini kwa mfumo huu huu wa elimu tumewapiga sana.
Tatizo tu tulilobaki nalo ni mfumo mbovu wa siasa.Hizi sera za kuwaiga Waingereza au Wamarekani zinatumaliza.
 
Uharibifu umezidi kila awamu wanajiamulia tu kuibomoa elimu
Tatizo ni kwamba mawaziri wana nguvu kubwa kwenye maamuzi ya elimu. Wakati huo huo mawaziri wa elimu siyo watu bora kielimu. Ni watu misheni-misheni tu! Hata Kilango Malechela na Muhagama walishaishika elimu kwa uduni wao. Tunakwisha kabisa!!! Mungai na yake, Kawambwa na yake, ............. Leo ni Mkenda na upuuzi huu!
 
Back
Top Bottom