Hizi sera ambazo kila waziri akija anakuja kivuake ni "supply driven" ndiyo hizi ambazo hata wadau muhimu huwezi kusikia wakishirikishwa katika kuziandaa. Sera nzuri ni lazima ziwe "demand driven" kwa kuwa wadau muhimu hutambua "missing gaps" zilizopo katika mfumo wa elimu uliopo hivi sasa.
Ili tupate sera nzuri ya elimu hapa nchini, ni vyema kushirikisha wadau muhimu kama vile wataalamu, watafiti na wanataaluma kutoka fani mbalimbali ili kuweka vigezo vizuri vya kuzingatia wakati wa ufundishaji, wakufunzi, walimu, wazazi, walezi, n.k. ili kupitia katika majukwaa yao maoni muhimu yaweze kukusanywa na kufanyiwa kazi kabla ya kuiandaa sera husika ya elimu.
Serikali isiishi kwa "trial & error" bali ifanye tafiti nyingi na za uhakika ili iweze kuthibitisha uamuzi wake. Mzee Mwinyi aliwahi kugusia kuhusu sifa ya mtu kuwa "kichwa cha mwendawazimu"