Wadau wapendekeza Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6

Wadau wapendekeza Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6

Haya , bado unaonyesha madhara ya elimu yetu ya kukariri. Unyesha niliposema tunatakiwa tufanye mchakato kama wa Warioba wa katiba! Kusema kuwashirikisha wananchi ndiyo kuwa kama mchakato wa katiba? Na wewe unaona kabisa wataalam wachache kujifungia na kujaribu kuja na solution bila kushirikisha makundi mengine ni sawa? Pole sana.
Hiyo elimu tunayotaka tuifanyie mabadiliko ndio imezalisha hao wataalamu unaotaka washauri kuhusu mabadiliko, na unategemea maajabu. Lol 😛 😛 😛 😛
 
Pia hili suala ni la kisera la serikali kufanya elimu ya sekondari iwe elimu ya msingi kwa watanzania wote. Dunia imebadilika sana. Tusiogope changes bali tujiandae kwenda na mabadiliko hayo.
 
Sema Mh. jumanne Kishimba anaongeaga points Sana pale Bungeni. Tatizo serikali haimchukuliagi kama Yuko serious,badala yake anaonekana Kama ni mtu wa comedy. Kuna kipindi Mh. Rais alimsapoti.
 
Yaleyaoe ya mungai aliyekurupuka kufuta masomo ya biashara na Bado tukapigishwa mtiani
 
Serikali inapeleka mapendekezo ya kutunga, kubali au kuleta mapendekezo ya kubadili sheria, bunge kazi yake kujadili na sheria hazipiti kama bunge limekataa na wakikubali haiwi sheria mpaka Rais atie wino. Hata tozo zilienda bungeni wakapitisha lakini kuja kushtuka wamepitisha kitu bila kujuwa au makusudi sababu ni serikali yao ya chama chao kupinga hawawezi au hawana uelewa hawako serious kujadili mambo muhimu au kikubwa uwezo wao wa kuchambua mambo ni mdogo kama elimu yetu ilivyo.
Samahani kwa lugha yangu kali.
Hapo unaongea blah blah zilizopandikizwa kwenye akili zwtu kwa makusudi.

Hapo umeongelea kinachofanyika na sivyo inavyotakiwa.
Serikali inapaswa kupeleka mapendekezo ya kutungwa sheria Bungeni na kupitia Chief Draftsman Bunge linapaswa kuainisha taratibu namna sheria hiyo inavyopaswa kutungwa na kuwapa nafasi wawakilishi wa wananchi kutimiza wajibu wao.

Unajua hii kuiacha serikali itunge sheria kisha kuipeleka Bungeni for approval ndo ujinga tunaopaswa kuachana nao kupitia Katiba Mpya..

Tuepuke kuishi ktk ujima
 
Siyo suala la wazee wa kupinga. Ni suala la watu wenye akili ya kuhoji mabadiliko yanayofanywa na wanasiasa kwa njia ya zimamoto. Wewe unaona wanasiasa wachache kujifungia na kujaribu kuja na solution bila kuwashirikisha wataalam na wananchi ni sahihi? Wengine mmeathiriwa na elimu ya kukariri ndiyo maana mnadhani kuhoji jambo ni kupinga.
Miaka yote wanasiasa ndio wamekuwa wakifanya changes katika mfumo wa elimu yetu bila kuzingatia maoni ya wadau,wataalamu wanaotoka katika kada ya elimu n.k. Sasa Kuna haja ya wadau,watetezi wa haki za elimu na experts kupinga jambo hili, maana linazidi kuua elimu yetu.
 
Hatukatai kuwa wao ndio watungaji wa Sheria na viongozi wa nchi, lakini katika suala la muhimu Kama elimu lazima wawashirikishe wananchi na wataalam mbalimbali
 
6 bado mingi ila honera sana wizara mwanzo mzurii. Pia elimu ya secondari miaka miwili inatosha m4 mingi sana.
 
Ni muda Sasa serikali kukubali mpango wa kuifanya lugha ya kiingereza kuwa lugha rasmi ya kufundishia kuanzia shule ya msingi.
Hili nalo neno, na uundwe mkakati wakuwapata walimu ambao wako competitive katika lugha zote kiingereza huku kiswahili likibaki kama somo.
 
Haya ndio maendeleo, ila tulipaswa tuwe kama US, 8-4-4 .
Primary miaka 4
Mtoto anaanza la kwanza akiwa na miaka 4 na kumaliza elementary akiwa 12 anakwenda sekondari at 13 years for 4 years na kumaliza at 16
Anaingia college at 17 years for 4 years na degree zao ni masters!.

US mtu haruhusiwi kusomea sheria kama hana degree nyingine, hivyo kule kwenye sheria, sciences na udakitari wa binadamu, hakuna kilaza atapenya!. Sio hapa vilaza wanakimbilia LL.B na kupewa degree za michongo!, kufika LST wana stopishwa basi ni kelele mwanzo mwisho!.

Kule hawana A level!.

P.
Huo mfumo mzuri sana kongoree kwa waliotoa mawazo wadau tunamsubilia kwa hamu sana na mifano ipo wazi

Kabla serikali aijaanza kukazia mambo ya prem number wazazi wengi waliowapeleka watoto zao english media walikuwa wanaishia darasa la tano tu baada ya hapo mzazi anamtafutia mtoto shule anaend kufanya mitihani ya kujipima kuzingia kidato cha kwanza katika watoto wengi walifauru na kuanzia kidato cha kwanza na kuhitimu kidato cha nne kwa ufauru mzuri tu mpaka serikali ilipokaza mambo ya prem number hapo ndio wazazi wameqcha watoto wamalize darasa la saba
 
Kikubwa ni kuangalia vitu vilivyopitwa na wakati viondolewe na muda wa kukaa shuleni upungue, tumepoteza muda mwingi sana shule kusoma vitu ambavyo havitusaidii.
 
Hao Wa private wamesomea wapi? Ni commetment. Serikalin kupo loose sana
Tatizo hakuna walimu wa shule za serikali wanaojua kiingereza fasaha mkuu.

Amini hili maana tunawajua vizuri. Somo la kiingereza ukimfuatilia mwanao mfano mwalimu anavyosahihisha kazi ni kituko.
 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amesema kuwa katika sera mpya inayotarajiwa kuzinduliwa hapo baadaye elimu ya msingi itakomea darasa la 6.

Kauli hiyo ameisema hii leo Oktoba 20, 2022, na kuongeza kwamba sera mpya ya elimu itakapozinduliwa hakutakuwa na mtihani wa mwisho wa elimu ya msingi na kwamba mtihani utakuwa ni wa kidato cha nne tu, huku akisema mwanafunzi akianza kidato cha kwanza atakuwa tayari ameshajiweka kwenye mchepuo maalum hadi kidato cha nne.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga amesema kuwa serikali inatazamia kuzindua sera mpya ya elimu kufikia mwezi Desemba, 2022 ili kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu na kwamba mabadiliko yataanzia elimu ya msingi.
wazee wakupinga kila kitu mpo kumbe
Unasikia ndugu, hayo ni maamuzi ya huyo waziri tu, akiondolewa hata kesho anaekuja naye anaweka utaratibu wake. Huoni kuwa ni ujinga uliokithiri, nchi haina misingi maalumu, Banana Republic!
 
Sasa hapo wametuharibia sisi Walimu na Polisi kupata posho za kusimamia mitihani ya darasa la 7 ujue 😂😂
 
Back
Top Bottom