Wadau wapendekeza Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6

Wadau wapendekeza Elimu ya Msingi kuishia darasa la 6

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amesema kuwa katika sera mpya inayotarajiwa kuzinduliwa hapo baadaye elimu ya msingi itakomea darasa la 6.

Kauli hiyo ameisema hii leo Oktoba 20, 2022, na kuongeza kwamba sera mpya ya elimu itakapozinduliwa hakutakuwa na mtihani wa mwisho wa elimu ya msingi na kwamba mtihani utakuwa ni wa kidato cha nne tu, huku akisema mwanafunzi akianza kidato cha kwanza atakuwa tayari ameshajiweka kwenye mchepuo maalum hadi kidato cha nne.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga amesema kuwa serikali inatazamia kuzindua sera mpya ya elimu kufikia mwezi Desemba, 2022 ili kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu na kwamba mabadiliko yataanzia elimu ya msingi.
Lugha ya kufundisha itakuwaje?!!
 
Tatizo wataalam hatuna hatujaandaa waalimu kuendana na kasi hio mpya natamani waajiriwe waalimu wa degree kufundisha primary tena lugha iwe english. Kinachotusumbua ni lugha na miundombinu ya elimu. Mkuu ukipata muda tembelea shule zetu,zinatia huruma sana anzia madawati hadi vitabu,hakuna library. Enzi zile kulikua na somo la sayansi kimu ila mungai alipoupata uwazori tu akalifutilia mbali. Lile somo lilikua zuri sana
Elimu tuliyo nayo iliishapitwa na wakati, haimsaidii mwanafunzi kumudu/ kupambana na maisha napenda transition/ revolution. Tusipoteze muda wa vijana kusoma vitu visivyokuwa na msaada. Waache watu wamalize shule mapema wakiwa vijana na wapate nafasi ya kusoma/practice skills nyingine za maisha.

Kwa elimu tuliyonayo mtu anamaliza degree na hata uwezo wa kujiajiri hana.
 
kwang me kiingereza liwe somo la kujifunzia kiswahili iwe lugha ya kufundishia.
sasa kiongozi huo utaratibu wa kufundisha kwa lugha mbili tofauti huoni ni mkanganyiko ambao unachangia kuzorotesha elimu yetu
Naona lugha inatakiwa iwe moja tu kwenye kufundisha either eng au kiswa
 
Haya ndio maendeleo, ila tulipaswa tuwe kama US, 8-4-4 .
Primary miaka 4
Mtoto anaanza la kwanza akiwa na miaka 4 na kumaliza elementary akiwa 12 anakwenda sekondari at 13 years for 4 years na kumaliza at 16
Anaingia college at 17 years for 4 years na degree zao ni masters!.

US mtu haruhusiwi kusomea sheria kama hana degree nyingine, hivyo kule kwenye sheria, sciences na udakitari wa binadamu, hakuna kilaza atapenya!. Sio hapa vilaza wanakimbilia LL.B na kupewa degree za michongo!, kufika LST wana stopishwa basi ni kelele mwanzo mwisho!.

Kule hawana A level!.

P.

Mkuu umeandika kwa haraka na hisia kubwa mno.

Je ni sahihi kwa wahitimu kutokufanya mtihani wa kuhitimu shule ya msingi?
 
Naibu waziri wa Elimu ameeleza kuwa kutokana na Sera iliyo pendekezwa kuwa kuanzia siku zijazo Elimu ya Msingi itaishia Darasa la Sita na sio la saba tena.
Pia hakuto kuwa na mtihani wa kumaliza darasa la sita zaidi ya kufanya "assessment".

kwanza naipongeza wizara kwa kuja na mapendezo mazuri ya mfumo wa Elimu yetu, hivyo nashauri sera hii ianze kutumika haraka iwezekanavyo.
 
What difference will it bring to the current one...!??
 
Hawa hawa tunaowajua au watatolewa nchi jirani
Maana elimu ya juu tu notes za kiingereza ila lecturer anaongea kiswahili 😆
Mkuu niamini mimi,Watanzania wengi waliopita o level hadi chuo wanajua kiingereza,ila kwa vile awaongei mara kwa mara wanakosa kujiamini,mfano kama umepitia huko unapoangalia movie wanazoongea kiingereza uelewi?kinachotakiwa kuwapa watu kujiamini na kutokana na mazingira yaliyopo basi kiingereza kianzie huko std 1
 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amesema kuwa katika sera mpya inayotarajiwa kuzinduliwa hapo baadaye elimu ya msingi itakomea darasa la 6.

Kauli hiyo ameisema hii leo Oktoba 20, 2022, na kuongeza kwamba sera mpya ya elimu itakapozinduliwa hakutakuwa na mtihani wa mwisho wa elimu ya msingi na kwamba mtihani utakuwa ni wa kidato cha nne tu, huku akisema mwanafunzi akianza kidato cha kwanza atakuwa tayari ameshajiweka kwenye mchepuo maalum hadi kidato cha nne.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga amesema kuwa serikali inatazamia kuzindua sera mpya ya elimu kufikia mwezi Desemba, 2022 ili kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu na kwamba mabadiliko yataanzia elimu ya msingi.
Kichwa cha habari kinapotosha! Serikali IMERIDHIA - kwani huo mfumo mpya ni ombi la nani?
 
Mkuu niamini mimi,Watanzania wengi waliopita o level hadi chuo wanajua kiingereza,ila kwa vile awaongei mara kwa mara wanakosa kujiamini,mfano kama umepitia huko unapoangalia movie wanazoongea kiingereza uelewi?kinachotakiwa kuwapa watu kujiamini na kutokana na mazingira yaliyopo basi kiingereza kianzie huko std 1
Walimu hawa wa nacte hamna wa kufundisha kieng kwa ufasaha bruh
Labda waanze kuandaliwa sasa hv niamini mimi primary nimefundishwa na walimu asilimia kubwa kutoka kenya
Mwalimu wa kibongo akija kufundisha akiongea darasa zima tunacheka jinsi anavyoongea kieng mpasuko 😆
 
Back
Top Bottom