Wadau wapinga Rais Samia na Makamu wake kuingia na Viti binafsi Kanisani, yadaiwa ni kujikweza

Wadau wapinga Rais Samia na Makamu wake kuingia na Viti binafsi Kanisani, yadaiwa ni kujikweza

Queen+Duke+Edinburgh+Visit+St+Columba+Church+ip-afaxjhe-x.jpg

Waumini wote kanisani tunakalia mabenchi ya mbao

Hata wafalme na malkia wa himaya zilizotawala dunia wanajinyenyekeza mbele za Mungu

Japo wanaweza kutandaza makochi ya ngozi na sufi kanisa zima lakini wanajishusha mbele ya madhabahu ya Mungu kwa sababu wanajua Yesu Kristo alizaliwa kwenye josho la kulishia ng'ombe akiwa ni mtoto wa muweza wa yote.
Nyerere & Ben Mkapa walikuwa wakatoliki wazuri sana...

Sina hakika kama kuna siku walikwenda kuabudu kanisani huku wakiwa wamebeba na makochi yao ya kifalme ili wakalie ndani ya kanisa wakati huohuo kanisa likiwa na viti vya kutosha kwa kila mtu...!!
 
Kwa hiyo wanajiona wako juu ya Kuhani Mkuu, hadi mpango naye hajui taratibu za kanisa.......hajui kwamba anayekalia kiti maalumu na kuvaa mavazi maalumu hekaluni ni Kuhani Mkuu, wanafuatia makuhani na watumishi wengine wa hekalu na baadaye waumini.
 
Kwenye Ibada Maalum ya kumbukumbu ya miaka 23 ya kifo cha Mwalimu Nyerere , iliyofanyika huko Mkoani Kagera , Viongozi kadhaa wa Kitaifa wamehudhuria, akiwemo Mh Rais Samia Suluhu na Makamu wake , Dr Philipo Mpango , Tunawapongeza kwa jambo hilo .

Sitaki kurudia yaliyotokea ili nisiwachoshe , lakini Kitendo cha Rais na Makamu wake kuingia na Viti vyao vya enzi ndani ya kanisa kimepingwa na wadau wengi , huku wakitahadharisha viongozi kuacha kujiona ni wa kipekee , Ukweli ni kwamba HAWANA UPEKEE WOWOTE , ukiachilia mbali vyeo walivyo navyo hawana tofauti yoyote nyingine na sisi wengine .

Kitendo cha kuingia na Masofa yao Kanisani ni DHARAU KWA WAUMINI na Kanisa kwa ujumla , na kinapaswa kukemewa ili kisirudiwe tena , kama hawataki kukaa kwenye mabenchi ya kanisa , basi wasiingie kwenye Makanisa , waishie nje na hotuba zao .

Ziko Picha kadhaa zikiwaonyesha Joe Biden wa Marekani na Haikainde Hichilema wa Zambia wakiwa wameheshimu madhabau na kukalia Mabenchi ya kanisa , mbona walishiriki ibada na wakamaliza kwa amani tu , Hawa viongozi wetu wana upekee gani hawa ?

View attachment 2387287

Angalizo : Sina chuki yoyote na viongozi hawa .
Angalizo limetufumbua macho.
 
Mada nyepesi sana. JPM alikalia kiti cha kwake alicholetewa na wasaidizi wake siku ile alipokwenda chuo kikuu na kuongea na wasomi hakuna aliyekuja na uzi kabisa.
Hata microphone alikuwa hatumii ya pata sote.

Na mwanafunzi wake Mwinyi Junior akiingia msikitini anaingia na zulia lake anatandikiwa juu ya lililopo. Na Safu ya mwanzo yote anaekewa yeye na wasaidizi wake.
 
Hata microphone alikuwa hatumii ya pata sote.

Na mwanafunzi wake Mwinyi Junior akiingia msikitini anaingia na zulia lake anatandikiwa juu ya lililopo. Na Safu ya mwanzo yote anaekewa yeye na wasaidizi wake.
ili wawe karibu na Mungu !
 
Back
Top Bottom