Mnywani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2020
- 774
- 898
Dr. Philip Mpango ni mkatoliki na amesali hapo bukoba cathedral mara kadhaa na makanisa mengine anapokua ziarani hatujawahi kuona akiletewa kiti chake. Hapo aliyefanya viletwe viti "vya wageni" ni Mama. Hoja za kiusalama, usafi, ukubwa nk...sizikatai Ila pia sizikubali, sana sana ni hoja ya Mila na desturi za wahaya, mgeni uhayani anapewa heshima iliyopitiliza tena hasa kama ni kiongozi au mtu mwenye mafanikio kimaisha (wahaya wanaelewa ninachozungumza) na hivyo hawatamruhusi kamwe kukaa kama wanavyokaa wao Wala kula wanachokula wao, watamwandalia kila kitu chake Cha tofauti, kizuri na kwa heshima na hofu kubwa. Kuna simulizi za zamani kuwa "abakama" yaani machifu wa kihaya walipokwenda mahala kutembea hawakuruhusiwa hata kukanyaga ardhi, walichukiliwa vijana wa kiume na kulala barabarani ambapo wakubwa wale walikanyaga migongo yao kwenda mahala palipoandaliwa kutoa hotuba. Kama Hilo halitoshi, wakati wa hotuba simulizi zinasema Omkama alisimika mkuki wake kwa kuuchoma kwenye mguu wa kijana ambaye badae alipewa ng'ombe na mke mzuri. Hata hivyo, hoja yangu inapata maana kama vile viti viliandaliwa na kanisa kwani viongozi na waamini wengi wa bukoba karibu wote ni wahaya. Kama ni viongozi wa mkoa wakiongozwa na mkuu wa mkoa kwamba ndo waliomba walete viti maalum kwa ajiri ya viongozi wakuu wa kitaifa, kanisa lisingeweza kukataa maana ibada haiwezi kuathirika kwa namna yoyote Ile, sasa labda kama ni hoja ya uchawa, itakua kwa hao waliovileta. Mimi hata hivyo bado nampongeza mama kwa kushiriki ibada ile na kukubali kuingia kanisani na kufuata matendo yote ya ibada ya kikristo, zamani ilikua kama raisi sio mkristo, ibada ziliandaliwa nje ya kanisa...huu ni unyenyekevu wa aina yake unapaswa kupongezwa sio tuangalie mambo madogo madogo yasiyokua na maana. Mkisema mbona kiongozi fulani alikua anaenda msikitini wakati ni mkristo, mkumbuke wakristo hawana katazo la moja kwa moja kwenda nyumba za ibada za wengine kama ndugu zao wale, kwa hiyo mama mpaka anakaa pale mbele na kusikiliza mahubiri ya askofu kilaini ujue amevuka vihunzi vingi sana., mama mitano tena.