Wadau wapinga Rais Samia na Makamu wake kuingia na Viti binafsi Kanisani, yadaiwa ni kujikweza

Wadau wapinga Rais Samia na Makamu wake kuingia na Viti binafsi Kanisani, yadaiwa ni kujikweza

Nakumbuka JPM alihuduria Ibada katka Kanisa Kuu la Mt.Mathias Mulumba Kalemba Songea mjini na alikalia mabenchi kama waamini wengine
 
Hao ni marais wa nchi kuna suala zima la ulinzi. Vipi kama viti vya hapo hapo kanisani vikawekewa mabomu na yakawamaliza?. Huoni kama huo ni uzembe wa ulinzi.

Hii amani inatudanganya sana, tunashindwa kufikiria kwa kina.
Kwa hiyo Bomu likipigwa Kiti kitamsaidia???
 
Kwenye hii hoja, wewe ndio hujafikiria kwa kina! Kwamba waweke mabomu kwenye mabenchi au viti vya kanisani ?

Ina maana usalama wa taifa hawana vifaa vya kutambua hivyo viashiria?

Kama wana nia ya kumdhuru, watashindwa kutumia vitu vingine kama mic, podium, nk ikiwa watawaza kuweka kwenye hivyo viti??

Kwa kifupi, huo ni ukoloni usio na maana yoyote! Protocol nyingine ni za kitumwa ndio maana hata baadhi ya marais ya nchi nyingine wanazipotezea kama hazina tija yoyote!

Kubeba kiti maalum hadi kwenye nyumba za ibada, wakati viti vingine vipo, huo ni u-tu-mwa!
Mkuu huyo ni rais, labda umri tunatofautiana sana. Usalama wa taifa wamefuata mtiririko wa kanuni za ulinzi na ikaonekana ni heri atumie kiti cha kiofisi kuliko hivyo vya hapo kanisani.
 
Nilikuwa nakuona una akili kumbe takataka kabisa.
Takataka ni wewe unayemuweka rais kundi moja na maadmini wa makundi sogozi ya shule mnazosoma.

Huyo ni alama ya nchi ni nembo ya Taifa (kwa mujibu ya Kabudi) sio mtu tu fulani mdogo.
 
JPM alikwenda chuo kikuu katika official capacity yake.

Kiongozi akienda kanisani anakwenda kama muumini, haendi kama kiongozi wa Serikali.
JPM alipokuwa anahutubia ndani ya kanisa mpaka wiki chache kabla hajafariki dunia na kutoa maagizo alikuwa akifanya hivyo kwa mamlaka gani?.
 
Lakini JPM hakuwahi kukalia kiti tofauti na mabench ya kanisani!
Hajawahi kupelekewa kiti na wasaidizi wake kanisani, aliheshimu sana madhabahu ukiacha mapungufu yake mengine!
Angefanya kama hawa ungeona, jinsi magazeti yangepambwa!
Kwani Samia ni mkristo mpaka alazimike kufuata mila na tamaduni za kikristo?.
 
JPM alipokuwa anahutubia ndani ya kanisa mpaka wiki chache kabla hajafariki dunia na kutoa maagizo alikuwa akifanya hivyo kwa mamlaka gani?.
Huna adabu wewe! Tupe agizo alilowahi kulitoa kanisani. Kumbuka Kuna kuzungumza na waumini na sio maagizo. Shwaini wewe!
 
Huna adabu wewe! Tupe agizo alilowahi kulitoa kanisani. Kumbuka Kuna kuzungumza na waumini na sio maagizo. Shwaini wewe!
Mramba aliyekuwa bosi wa TANESCO alifukuzwa kazi na JPM ndani ya kanisa tena akiwa na kipaza sauti mkononi na kamera zikimrekodi mbele yake.
 
Kwenye Ibada Maalum ya kumbukumbu ya miaka 23 ya kifo cha Mwalimu Nyerere , iliyofanyika huko Mkoani Kagera , Viongozi kadhaa wa Kitaifa wamehudhuria, akiwemo Mh Rais Samia Suluhu na Makamu wake , Dr Philipo Mpango , Tunawapongeza kwa jambo hilo .

Sitaki kurudia yaliyotokea ili nisiwachoshe , lakini Kitendo cha Rais na Makamu wake kuingia na Viti vyao vya enzi ndani ya kanisa kimepingwa na wadau wengi , huku wakitahadharisha viongozi kuacha kujiona ni wa kipekee , Ukweli ni kwamba HAWANA UPEKEE WOWOTE , ukiachilia mbali vyeo walivyo navyo hawana tofauti yoyote nyingine na sisi wengine .

Kitendo cha kuingia na Masofa yao Kanisani ni DHARAU KWA WAUMINI na Kanisa kwa ujumla , na kinapaswa kukemewa ili kisirudiwe tena , kama hawataki kukaa kwenye mabenchi ya kanisa , basi wasiingie kwenye Makanisa , waishie nje na hotuba zao .

Ziko Picha kadhaa zikiwaonyesha Joe Biden wa Marekani na Haikainde Hichilema wa Zambia wakiwa wameheshimu madhabau na kukalia Mabenchi ya kanisa , mbona walishiriki ibada na wakamaliza kwa amani tu , Hawa viongozi wetu wana upekee gani hawa ?

View attachment 2387287

Angalizo : Sina chuki yoyote na viongozi hawa .
Tukumbuke kuwa SSH ni muislam, kuingia kwake kanisani ni kwa heshima tu na kwa kuzingatia maadili ya waliomtangulia.

Hapaswi kupangiwa akae kiti kipi. Kuna marais wa afrika hii hii hawaingii ndani ya nyumba za ibada zisizokuwa za dini zao.
 
Mingi tu, Hata pale Jerusalem kwenye msikiti wa Nabiii suleiman waliswali
Ww tangu lini suleiman alikua muislam ww hebu jamani tuwe tunasoma maana hunidanganyi hata kidogo history na vitabu vya dini nimevisoma sana
 
Msikitini huwa anakaa chini na wengine ukiona kaingiza kiti kanisani ujue mazingira yaliruhusu iwe hivyo
 
Kwani Maaskofu nao uwa wanakaa kwenye mabench?. Si wana viti vyao vya utukufu hivyo ndio ukristo ulivyo huwezi kuona hayo mambo mskitini wote mtakaa kwenye mswala iwei mamu iwe sheikhe iwe Raisi.
 
Back
Top Bottom