Wadau wapinga Rais Samia na Makamu wake kuingia na Viti binafsi Kanisani, yadaiwa ni kujikweza

Wadau wapinga Rais Samia na Makamu wake kuingia na Viti binafsi Kanisani, yadaiwa ni kujikweza

Erythrocyte ni kama amesahau roles ya PSU. Viongozi wameingia na kuelekezwa sehemu ya kukaa, alitaka wakatae na wakati tayari wako ndani ya kanisa!

Nadhani maelezo/ malalamiko yangejikita kwenye ushauri kuwa wakati mwingine jambo hilo lisijirudie kwakuwa halileti picha nzuri kwenye jamii .
Shida ya PSU ya Sasa ni ya kujipendekeza sana, wamejaa Wapemba watupu Advance Team.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Inaonesha una chuki binafsi tu na huu uongozi, maana haina maana kulalamikia viti badala ya kuandika nyuzi zinazolenga maendeleo.
 
Inaonesha una chuki binafsi tu na huu uongozi, maana haina maana kulalamikia viti badala ya kuandika nyuzi zinazolenga maendeleo.
Mleta Mada Anapinga watawala Wa Sasa kuvunja tatatibu za Kanisa Wakati utaratibu wanaujua. Mbwembwe Zao wazifanyie Huko Nje ya madhabau. Halafu namshangaa Kilaini kukubali Huo Ujinga uliofanywa Hapo Kanisani

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mada nyepesi sana. JPM alikalia kiti cha kwake alicholetewa na wasaidizi wake siku ile alipokwenda chuo kikuu na kuongea na wasomi hakuna aliyekuja na uzi kabisa.

Lakini JPM hakuwahi kukalia kiti tofauti na mabench ya kanisani!
Hajawahi kupelekewa kiti na wasaidizi wake kanisani, aliheshimu sana madhabahu ukiacha mapungufu yake mengine!
Angefanya kama hawa ungeona, jinsi magazeti yangepambwa!
 
Wewe hupaswi kuwalaumu hao viongozi moja kwa moja.

Erythrocyte!
Umeandika as if walikuja wamebeba viti vyao,wakati ukweli ni kwamba kama ni kasoro imetokea.na kama ni kulaumiwa ni hao waliokuwa na jukumu la maandalizi na sidhani kama ni maagizo ya Mheshimiwa Rais wala Makamu wake.
Wao wameingia na kuelekezwa mahali walipoandaliwa kukaa.

Baadhi ya vitu sio lazima uvipinge kwa sababu havina tija kwa maendeleo chanya wala havitowi fundisho lolote kwa jamii.
Pia kuwa pingapinga sio alama ya elimu bali ni dalili za ubishi usio na tija pia.

Rais akipanda basi mnasema kadharauliwa,je kipi afanye ili awafurahishe?

Mtaendeleza bifu la kukaa benchi mpaka 2025?

Si mtafika mmechoka Sana?

Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe.

NENO walahi!
Rais wa nchi huwezi kumfananisha na raia, sasa hivi kuna kila aina ya sumu ya kuwwangamiza hawa marais wetu wa AFRIKA haswa wanapoona kazi vizuri!
Tuwa heshima viongozi wetu kwa maana hata neno la Mwenye Enzi Mungu linatuagiza hivyo!
Remain blessed!
Acha hasira utakosa baraka zako!
 
Mleta Mada Anapinga watawala Wa Sasa kuvunja tatatibu za Kanisa Wakati utaratibu wanaujua. Mbwembwe Zao wazifanyie Huko Nje ya madhabau. Halafu namshangaa Kilaini kukubali Huo Ujinga uliofanywa Hapo Kanisani

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kwani utaratibu wa kanisa unataka kila mtu akalie benchi?

Kanisa lilishiriki katika maandalizi yote ya misa na kufuata protocal stahiki ikiwemo kuandaa sehem Rais atakayokaa! kwanini mumlaumu Huyu Rais na siyo Jimbo husika?

Mbona watanzania tuna kuza vitu vidogo vidogo visivyo na maana! mimi pamoja na Kuwa muumini wa kanisa, jambo hili tunalikuza tuu, wakati halina impact yoyote kwenye imani!

Wakatolik sio watu wa kumind kitu kama icho, watu mnakuza tu huu mjadala lionekane ni jambo kuuubwa!
 
Lakini JPM hakuwahi kukalia kiti tofauti na mabench ya kanisani!
Hajawahi kupelekewa kiti na wasaidizi wake kanisani, aliheshimu sana madhabahu ukiacha mapungufu yake mengine!
Angefanya kama hawa ungeona, jinsi magazeti yangepambwa!
Kwani kupeleka kiti kanisani ni kudharau madhabahu?

Jambo hili linanishangaza sana!
 
Kwenye Ibada Maalum ya kumbukumbu ya miaka 23 ya kifo cha Mwalimu Nyerere , iliyofanyika huko Mkoani Kagera , Viongozi kadhaa wa Kitaifa wamehudhuria, akiwemo Mh Rais Samia Suluhu na Makamu wake , Dr Philipo Mpango , Tunawapongeza kwa jambo hilo .

Sitaki kurudia yaliyotokea ili nisiwachoshe , lakini Kitendo cha Rais na Makamu wake kuingia na Viti vyao vya enzi ndani ya kanisa kimepingwa na wadau wengi , huku wakitahadharisha viongozi kuacha kujiona ni wa kipekee , Ukweli ni kwamba HAWANA UPEKEE WOWOTE , ukiachilia mbali vyeo walivyo navyo hawana tofauti yoyote nyingine na sisi wengine .

Kitendo cha kuingia na Masofa yao Kanisani ni DHARAU KWA WAUMINI na Kanisa kwa ujumla , na kinapaswa kukemewa ili kisirudiwe tena , kama hawataki kukaa kwenye mabenchi ya kanisa , basi wasiingie kwenye Makanisa , waishie nje na hotuba zao .

Ziko Picha kadhaa zikiwaonyesha Joe Biden wa Marekani na Haikainde Hichilema wa Zambia wakiwa wameheshimu madhabau na kukalia Mabenchi ya kanisa , mbona walishiriki ibada na wakamaliza kwa amani tu , Hawa viongozi wetu wana upekee gani hawa ?

View attachment 2387287

Angalizo : Sina chuki yoyote na viongozi hawa .
Wamuulize Magufuli leo amekalia kiti gani
 
Siku Samia akiingia na Kiti kwenye msikiti wangu huu wa Temeke.

Mimi
hkA5GJr.gif
 
Wasiingie tena kwenye makanisa yetu.

Hivi huko msikitini pia anaingia na kiti chake??
 
Wasiingie tena kwenye makanisa yetu.

Hivi huko msikitini pia anaingia na kiti chake??
Sidhani kama ni Big deal, mimi namkaribisha aje hata na Meza yake hapa Msikitini Temeke Sudani.
 
Wewe hupaswi kuwalaumu hao viongozi moja kwa moja.

Erythrocyte!
Umeandika as if walikuja wamebeba viti vyao,wakati ukweli ni kwamba kama ni kasoro imetokea.na kama ni kulaumiwa ni hao waliokuwa na jukumu la maandalizi na sidhani kama ni maagizo ya Mheshimiwa Rais wala Makamu wake.
Wao wameingia na kuelekezwa mahali walipoandaliwa kukaa.

Baadhi ya vitu sio lazima uvipinge kwa sababu havina tija kwa maendeleo chanya wala havitowi fundisho lolote kwa jamii.
Pia kuwa pingapinga sio alama ya elimu bali ni dalili za ubishi usio na tija pia.

Rais akipanda basi mnasema kadharauliwa,je kipi afanye ili awafurahishe?

Mtaendeleza bifu la kukaa benchi mpaka 2025?

Si mtafika mmechoka Sana?

Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe.
Wanaangalia na mtu.

Nyerere angekubali kukalia kiti kile hata kama kaletewa???
 
Back
Top Bottom